Kwenye baiskeli haipo, wala pikipiki wala gari.
"Bajaji popo" |
Mark Stewart
akikatiza mitaa huku akiwa amepanda baiskeli-pikipiki yake inayotumia mwanga wa
jua anawaacha watu wakizigeuza shingo zao kumtazama.Kila pedali anayopiga,
miguu inazunguka kuanzia chini wakati muungurumo wa mota ya umeme-jua ukisikika
kwa mbali.
Kile
anachoendesha kinaonekana kama chotara ya baiskeli na gari, kikiwa na paneli za
jua pekee pamoja na umbo la kisasa. “Ni kijani, chaguo la abiria wa kisasa”. Stewart
mwenye umri wa miaka 65 , mtaalamu wa tiba za mionzi na mwanasaikolojia kutoka
Camridge aliamua kwenda likizo yake ya majira ya joto kwa usafiri wa baiskeli
yake mpya ya ELF badala ya usafiri wa kawaida wa treni na mabasi.
Safari yake
nzima kutoka Durhan mpaka Reston ilimchukua siku 5, na maili zipatazo 60. Baiskeli hizi za EFL
hufikisha mpaka maili 30 kwa saa (30mph) kwa kutumia pedali pamoja na mota ya
umemejua. Na maili 20 kwa saa kwa kutumia umemejua peke yake.
Kwa hakika njiani anakumbana na maswali mengi, lakini Stewart anasema hizo ni changamoto za za kawaida “Sijali namaana kuwa huwa nafurahi watu wanapoizungumzia. Baiskeli-pikipiki hii, inao uwezo wa kusafiri maili 1800 sawa na galoni moja ya petrol, haihitaji bima wala gharama za matengenezo ukilinganisha na gari la kawaida. Na zaidi gharama za matairi pia ni kidogo pia.
‘Teknolojia
ya utengenezaji wa hizi baiskeli ilichotwa kutoka teknolojia ya utengenezaji wa
ndege,maboti na baiskeli za kawaida’ anasema afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya
Organic Transit inayozitengeneza.
Mchanganyiko
wamajanga ya kimazingira , bei kubwa ya mafuta, mabadiliko ya hali ya hewa na
uhamiajiwa watu mijini, vyote huchangia muelekeo wa watu kuhitaji usafiri
mbadala, lakini siyo kila mtu atapenda baiskeli ya kawaida ya pedali. Cotter
alisema baiskeli-pikipiki hizi
zimetengenezwa mahsusi
kukabiliana na majanga yaliyotajwa.
Lakini
wakati EFL zinawekwa katika kundi la baiskeli na kampuni ya Organic Transit,
sheria mbalimbali zinasema hii siyo baiskeli bali gari na haitaruhusiwa kupita
katika barabara za baiskeli za kawaida.
Kiwanda
kinakuwa, kwa siku hutengeneza wastani wa baiskeli 1. Kwa sasa wameshazalisha baiskeli 75 na wana oda zaidi ya 200 ambazo
tayari wmeshachukua advansi. Matarajio ni kutengeneza baiskeli 4 kwa siku.
CHANZO : Associated Press, MWANDISHI, Shaquille Brewster
0 Response to "BAJAJI ILIYOUNDWA KAMA POPO !"
Post a Comment