Angalao ina ladha ya nyama!
Professor Mark Post pichani wa Maastricht University Netherlands. |
Jarida lenyewe lilikuwa ni hili hapa chini na habari yenyewe ilisomeka hivi;
Timu ya kimataifa ya watafiti imependekeza teknolojia mpya
ambayo itaweza kufanikisha utengenezaji wa nyama kwa kiasi kikubwa. Ukuzaji huo
wa nyama siyo kama ule uliozoeleka wa
kufuga mifugo kama ngombe bali ni kwa njia ya kimaabara.
Wataalamu hao wanasema
kulingana na maendeleo katika uhandisi wa tishu (Tissue engineering)
chembechembe hai (cells) za mnyama huchukuliwa
na “kuoteshwa” maabara, seli hizo hatimae hukua na kuwa nyama.
Teknolojia hiyo itakuwa na faida kwa binadamu na vilevile
kwa mazingira. “Kinadharia, seli moja tu inaweza kutengeneza nyama inayoweza
kuliwa na watu dunia nzima na jambo hilo linaweza kufanyika pasipo kuharibu
mazingira, hili ni wazo zuri sana” alisema Jason Mathey wa chuo kikuu cha
Marryland na mmoja wa mainjinia waliochapisha utafiti huo kwenye jarida moja
liitwalo “Engineering ajaournal”
Kuotesha nyama maabara kunaweza kuondoa ule umuhimu wa
kufuga mamilioni ya mifugo katika mazingira duni na itasaidia kupunguza
uharibifu wa mazingira. Nyama hiyo pia inaweza kuwa bora na safi zaidi ya ile
ya kawaida. Teknolojia hiyo hapo kabla ilikuwa ikitumika kwa ajili ya utafiti
wa kitabibu pekee, ni nyama kidogo tu kwa ajili ya kula iliyowahi kutengenezwa
na watafiti wa shirika la mambo ya anga la Marekani NASA;
Lakini pia teknolojia hiyo inaweza kuzusha upinzani na
ubishani mkubwa kimaadili kwa makundi mbalimbali ya kidini na kijamii. Inaweza
pia ikawa ni suluhisho kwa wale wasiopenda kula nyama iliyotokana na mnyama
aliyechinjwa.
Habari na shirika la (AP)
Sasa miaka zaidi ya 8 imepita utafiti huo umezaa matunda baada ya nyama hiyo kuanza kuliwa rasmi siku ya tarehe 5, mwezi huu. Kati ya watu wa mwanzo kuionja alikuwa ni mtafiti wa chakula Hanni Rutzier aliyetamka hivi, “Nilitegemea mnofu wake kuwa laini zadi ……..inakaribiana sana na nyama ya kawaida lakini siyo laini hivyo”
Mwingine ni
John Schonwald , mwandishi wa maswala ya chakula aliyesema, “Kilichopungua ni
mafuta lakini ni sawa na hambaga ya kawaida, kilichoonekana tofauti ilikuwa ni
ladha yake”
Wakati
akiionja, alipoulizwa ikiwa atawalisha wanawe nyama hiyo, mtaalamu huyo alijibu
kwamba amewawekea wanawe hao nyama kidogo na baadaye angekwenda kuwapa nao
waonje.
Hatua nyama inazopitia. |
Pia imebainika kwamba mmoja wa wafadhili wakubwa wa mradi huu ni mwanasayansi wa kompyuta wa Kimarekani, Sergey Brin na ambaye pia ndiyo mwanzilishi mwenza wa kampuni la Google. Mwenzake ni Larry Page.
Sergey Brin
anamiliki asilimia 16 katika kampuni hili kubwa kabisa la mtandao (Internate search giant). Utajiri wake
unakaribia kufikia Pauni billion 13.6 mwaka 2012. Inakadiriwa kwamba katika
mradi huu wa barger za nyama zinazotengenezwa maabara, aliwekeza kiasi cha
pauni 215 elfu.
Amewahi
kuwekeza pia katika mradi wa safari binafsi za anga za juu hususani mwezini. Mradi mwingine ni utafiti wa nishati na madini katika sayari
na maumbo mengine kama vimondo nje ya sayari hii ya dunia katika juhudi za
kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira na upungufu wa nishati katika sayari ya
Dunia.
CHNZO : MAIL ONLINE.
CHNZO : MAIL ONLINE.
0 Response to "HATIMAE ILE NYAMA YA KUTENGENEZA MAABARA YAANZA KULIWA."
Post a Comment