Wakati mwingine mimi hawa wazungu huwa wananishangaza sana, kabla ya mapinduzi walikuwa hawaishi kupiga kelele, “demokrasia
demokrasia”…..sijui haki za binadamu, uhuru wa kuabudu na mambo chungu nzima
yanayofanana na hayo. Hatimaye Sadamu Hussein alingoka tena kama haikutosha
wakamtia na kitanzi juu. Vivyo hivyo ikafuatia na kwa Muamar Ghadafi na swahiba
yake Mubarak wa masri.
Hayati Muamar Ghadafi |
Hayati Saddam Hussein |
Mohamed Mursi alipoingia madarakani nilishuhudia Wazungu hao
hao walioshangilia kungonga kwa aliyekuwa kipenzi chao wakati fulani Hussein Mubarak wakiupokea ujio huo kwa
tashwishi ya hali ya juu kwa kuwa hawakutegemea hata kidogo kwamba chama cha
kiislamu kingeshinda uchaguzi, walijutia kuondolewa Mubarak. Kipindi kifupi
Mursi alichokuwa madarakani tukashuhudia vitimbi kibao, vyombo vya habari nya
Magharibi kama kawaida ya vikaanza kuchimb chimba kila kona Misri wakilalama Chama
cha Udugu wa kiislamu kilikuwa kinaminya uhuru wa wachache na kilikuwa na njama
za kuigeuza Misri kuwa Taifa la Kiislamu kama Iran.
Madai hayo yalilipa jeshi nguvu ya kumngoa Musri, na badala
ya kuliunga tena mkono, wamenishangaza tena juzi wakiwalaani wanajeshi. Sasa
Wazungu hawa wanachokitaka ni nini? Hawataki moto wala baridi, lakini pia cha ajabu hata uvuguvugu pia
inaonekana hawapendi. Tatizo kubwa kwa nchi za Kimagharibi ni kutaka
kushinikiza aina yao ya demokrasia kwa mataifa mengine pasipo kuelewa kuwa Nchi
hasa za Kiafrika na zile Za Kiarabu zina tamaduni zao tofauti kabisa na zile za
kwao.
Kabla ya mapinduzi nchi za Libya, Irak, Misri, Tunisia na sasa
Syria wananchi wake walikuwa wakiishi maisha mazuri na ya amani, inasadikiwa kama Libya ilikuwa hata
mtu ukitaka kuoa serikali ilikuwa
ikikugharamia kila kitu. Sasa hivi kila mtu anashangaa ! , yale maziwa na asali
viko wapi tena?
0 Response to "MAZIWA NA ASALI VYA GADAFI, MUBARAK, NA SADAM HUSSEIN VIPO WAPI?"
Post a Comment