Wanasayansi wa Marekani wamegundua aina mpya ya mamalia
anayeishi misitu minene huko Colombia, na Equado anayeitwa Olinguito na ni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35
iliyopita ugunduzi kama huo kufanyika katika eneo la Marekani ya kusini. Yupo katika kundi la
mamalia wanaokula nyama (Carnivore) na jina lake kisayansi anaitwa Bassaricyon neblina.
Mnyama Olinguito aliyegunduliwa. |
Ugunduzi huo uliochukua zaidi ya muongo mmoja umehusisha
taasisi ya Smithsonia ambapo mtaalamu Kristofer Helgen alipokuwa akipanga vitu kwenye jumba la
makumbusho la Chicago aligundua ngozi na mifupa iliyokuwa imehifahiwa. “Ilinibidi
nisimame kwanza” aliieleza BBC. “Ngozi ilikuwa na rangi nyekundu iliyokolea na
nilipotazama fuvu lake, sikuweza kubaini kama ni la mnyama wa aina gani.
Lilikuwa tofauti kabisa na wanyama jamii
yake. Mara nikafikiri angeweza kuwa spishi(aina) mpya katika sayansi”
Oliguito ni jamii ya
Carnivora(mamalia wanaokula nyama) kundi moja na Paka, Mbwa na Dubu.
Naye Chris Norris, kutoka
Makumbusho ya Yale Peabody Museum of Natural History Connecticut na raisi wa
taasisi ya (Preservation of Natural History Collections) anasema kwamba mnyama
huyu katika miaka ya 70 alidhaniwa kimakosa kwamba yupo katika kundi moja na
wanyama wale wanaofanana naye kumbe siyo. “Wataalamu walishangaa ni kwa nini
alipochanganywa nao hawakuweza kuzaana na walijaribu kumchanganya katika zoo
mbalimbali lakini alikufa kabla hawajamgundua. Pengine ilikuwa ni kutokana na
kutokuwepo wakati huo utaalamu wa kisasa kama wa kuchuja DNA.
Mpaka sasa hivi
Wanasayansi Duniani kote wameweza kugundua na kuhifadhi sehemu ndogo sana ya viumbehai
wa Sayari hii. Spishi mpya za wadudu, minyoo, bacteria na virusi bado
wanagunduliwa lakini kwa mamalia imekuwa ni kwa nadra sana.
Mgunduzi Dr. Helgen akiwa na spishi ya mamalia aliyogundua. |
“Hii
inatukumbusha kwamba Dunia bado kabisa haijatafitiwa vya kutosha na zama za
ugunduzi bado kabisa zingali zipo katika hatua za mwanzo” Anasema Dr.Helgen. MnyamaOliguito anatufanya tufikiri ni vitu
gani zaidi ambavyo bado havijagunduliwa.
0 Response to "WANASAYANSI WAGUNDUA MNYAMA WA AJABU"
Post a Comment