ANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO KWA KISWAHILI, KUNA FAIDA NYINGI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO KWA KISWAHILI, KUNA FAIDA NYINGI.







Na Mary James (Guest writer)

Watu wengi hasa hapa Tanzania tumezoea tunapohitajika kuandaa michanganuo/mipango ya biashara zetu, tunafanya hivyo kwa kutumia lugha ya kiingereza. Jambo hili linatokana na sababu kubwa kwamba watu hawaelewi madhumuni yote ya kuandika mchanganuo wa biashara. Hudhani tu kwamba michanganuo ni kwa ajili ya kuombea mikopo, Basi !

Na kwa bahati mbaya biashara nyingi mipango yake inabakia tu vichwani bila ya kuandikwa mahali popote jambo ambalo linamfanya mjasiriamali ashindwe kudumu sawasawa kwenye malendo yake aliyojiwekea. Mbali na kuombea mikopo Mpango wa biashara una kazi nyingine nyingi kama ilivyoorodheshwa hapa chini;



1)     Kuanzisha na kuendeleza biashara mpya; ni dira itakayokuongoza katika safari ya kufanikisha biashara yako.

2)     Kuweka na kufafanua malengo pamoja na mikakati ya kufanikisha biashara yako.

3)     Kuombea mikopo kutoka taasisi za fedha.

4)     Kupima utekelezaji wa malengo mara kwa mara pamoja na kufanya marekebisho pale ulipokosea.

5)     Kuainisha mikataba baina ya wabia.

6)     Kutathmini bidhaa mpya, kuzitangaza au kupanua bidhaa za zamani.

7)     Kuweka viwango  katika biashara/kampuni kwa ajili ya kuiuza au kwa ajili ya maswala mengine ya kisheria.


8)   Ni kipimo cha uwezo wako kibiashara.

Nimewahi kusoma vitabu vingi juu ya Michanganuo ya biashara lakini karibia vyote vilikuwa vimeandikwa kwa lugha za kigeni, nilikuja kushangaa pale nilipokutana na kitabu hiki “Jifunze michanganuo ya Biashara...” Sikuamini kabisa kama kurasa 400 zote zimeandikwa kwa Kiswahili. Ile dhana (myth) kwamba Kiswahili hakina ubavu kuelezea maswala ya kiufundi au kama haya yanayohusiana na biashara na ujasiriamali  ilitoweka kabisa kichwani mwangu.

Nilikuwa nachukia michanganuo ya biashara, siyo kwamba ilikuwa migumu kuelewa bali kutokana na kuandikwa kwa lugha ya kiingereza. Baada ya kukisoma kitabu hicho nikagundua, hata Mjasiriamali aliyeishia darasa la saba tu anaweza akaandaa mpango wake mwenyewe wa biashara ilimradi tu anajua kusoma na kuandika na akazifaidi faida zilizotajwa hapo juu sawasawa na Mfanyabiashara mwenye CPA.

Wengine huwa wanaogopa wanapofika kipengele cha maswala ya fedha lakini kipengele cha fedha ni sehemu tu katika mchanganuo mzima, wala siyo sehemu muhimu zaidi kushinda nyinginezo, isitoshe nilichogundua ni kwamba hesabu katika mpango wa biashara ni kufahamu tu  makisio ya  kiasi cha mauzo yako ya kila siku, gharama mbalimbali zinazohitajika, kiasi cha kodi utakayolipa na kinachobakia hapo ni wewe tu kufahamu hesabu za “MAGAZIJUTO”  (Mabano, gawanya, zidisha, jumlisha, toa = jibu) ambazo ulijifunza darasa la tatu.

Kilichonifanya niifurahie Michanganuo yao ni mazingira ya Kitanzania ambayo biashara husika ziltumiwa katika michanganuo hiyo. Kama kwa mfano unasoma mchanganuo wa biashara ya saluni na ulishawahi kuifanya basi,  Wwwaoo..!  unajisikia kama vile ni wewe, ukiwa umeshika 'Steamer' ukiligeuza geuza huku mteja akiwa pembeni akisubiri kufanyiwa steaming.

0 Response to "ANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO KWA KISWAHILI, KUNA FAIDA NYINGI."

Post a Comment