Wanasayansi
wa Kiingereza wamegundua programu ya kompyuta ambayo wanadai inao uwezo wa
kupima hisia za wananchi katika Taifa kwa kutumia mtandao wa kijamii wa
Twitter. Programu hiyo waliyoiita “EMOTIVE” inafanya kazi kwa kutathmini mawazo
ya mihemko yanayotumwa katika mtandao huo wa kijamii.
Wamesema
ina uwezo wa ‘ku-scann’ (kupitia) mpaka ‘tweets’(mawazo) 2,000 kwa sekunde moja
na kuyatolea majibu ikiwa wananchi hao wapo katika hali ya hasira, chuki,
huzuni ama furaha. Wanadai ‘Emotions’ itasaidia katika kukabiliana na vurugu za
kiraia na kutabiri mapema tishio la usalama wa umma.
Zaidi
ya watu million 500 duniani kote wanatumia Twitter, na zaidi ya ‘tweets’(jumbe)
340 milioni hutumwa kila siku. Profesa John Jackson , aliyeongoza utafiti huo alisema, jamii kutumia mitandao ya kijamii
kuelezea mawazo yao huonyesha kwa usahihi na kwa wakati kile watu
wanachofikiria.
Naye
Dr.Ann O Brien mshiriki mwingine alisema, “Kwa tukio lolote lile tunaweza kuona
jinsi mwitikio unavyoongezeka na kupungua kwa muda fulani”
Mfumo
huu kwa sasa unatumika kupima tweets(jumbe) nchini Uingereza peke yake, lakini
watafiti hao wamesema, baadaye wataweza kuuboresha zaidi kupima tweets Duniani
kote.
Na,
BBC
0 Response to "PROGRAMU YA KOMPYUTA INAYOTUMIA TWITTER KUPIMA HISIA ZA WATU YAGUNDULIWA."
Post a Comment