Niliposoma habari ya mwanadada
huyu katika blogu ya Irenemwamfupe kwa kweli nilikumbuka mbali sana, enzi zileee……….,
tukiwa ‘O level’ tukisoma vitabu vya Literature
form one na two. Kulikuwa na kitabu kimoja kilichotungwa na mwandishi mashuhuri
Richard S. Mabala, ‘HAWA THE BUS DRIVER’, Hawa alielezewa na Mabala kama
mwanamke aliyekuwa jasiri, shupavu kiasi ambacho hata wanaume akiwemo na mumewe
mwenyewe walimuogopa na kumheshimu. Hawa mbali na kuwa jasiri pia alikuwa dereva
wa basi, nadhani wakati huo labda ilikuwa ni UDA, akifanya safari zake kwenda
mjini.
Nilikisoma kitabu hicho
karne iliyopita ya 20 lakini leo hii ninapokikumbuka maudhui yake na mafundisho
utafikiri ndiyo kwanza kimeandikwa leo, vitabu vya Mabala vilinivutia sana
nadhani hata na watu wengi viliwavutia pia.
Dereva Nusura Maguluko akiwa 'mzigoni' |
Dereva Nusura Maguluko kwa
mujibu wa Irene blogu ni dereva wa kike katika basi la Ndenjela Coach
linalofanya safari zake, Mbeya na Dar es sala.
Picha ya kitabu ni kutoka blogu ya Susan Abraham.
0 Response to "NUSURA MAGULUKO THE BUS DRIVER, 'HAWA THE BUS DRIVER' WA KARNE YA 21"
Post a Comment