Kutokana na shida kubwa
ya usafiri katika majiji makubwa kama vile Dar es salaam, kuna wakati mtu
unakaa ndani ya daladala na kutamani kama kungelikuwa na usafiri wako
binafsi wa angani ambao hakuna foleni
ambayo ingekuzuia".
Teknolojia ya usafiri
wa chombo ambacho nusu ni gari na nusu ni ndege, haipo mbali tena, Professa
katika taasisi ya teknolojia ya anga ya Massachusset anasema hivi, “Tunakoelekea
kutakuwa na usafiri binafsi wa anga ambao nusu ni gari na nusu ni ndege, ni
mchanganyiko wa ndege zisizokuwa na rubani zinazoendeshwa kwa kompyuta ‘Drones’
na magari ya roboti, hivyo ndege yako pia itakuwa ndiyo gari lako”
“Ijapokuwa ndege za
drones zinapigiwa sana kelele na vyombo vya habari, lakini ukweli ni kwamba mtu
unaposafiri kwa ndege ya kawaida ni sawa
sawa na unasafiri ukiwa katika Drone.
Usafiri siku za baadae angani na nchi
kavu utakuwa salama zaidi na ikiwa matumizi ya kompyuta yatatumika kwa kiasi
kikubwa. Hamna kikwazo kikubwa kiteknolojia katika kufikia ndoto hizo, zaidi ya
vikwazo vya kisaikolojia na kitamaduni katika watu kuachana na usafiri wa
magari ya kawaida.
Chanzo BBC
Bora uje tu maana shida tunayopata hasa sisi tunaokaa mbali kama huku mbezi inatisha
ReplyDelete