HATUA 5 ZA KUPITIA ILI KUMILIKI WEBSITE YA BIASHARA YAKO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATUA 5 ZA KUPITIA ILI KUMILIKI WEBSITE YA BIASHARA YAKO

Kama wewe ni mfanyabiashara wa kati au juu, basi kuwa na Website ni moja ya vitu vya lazima kwa dunia ya sasa. Takwimu zinaonesha, kuna Watanzania milioni tano wapo online kila siku. Hapa hawajajumlishwa wale walio nje ya nchi.

Kuwa na Website ya kampuni kunafungua milango zaidi kwa biashara yako, kila kona ya dunia inayofikika kwa intaneti, basi website yako inaweza kufika. Kwa kutumia mitambo ya utafutaji (searh engines) kama Google, Yahoo, Bing nk, watu ni
rahisi sana kutafuta wanachokitaka online. Hivyo usipoteze nafasi hii ya kipekee kabisa.
Katika makala za awali, tumeandika sana umuhimu wa website, mambo ya kuzingatia nk, leo hii tutaangalia hatua muhimu za kupitia hadi kumiliki website. Hivyo twende kazi...

1.Andaa bajeti

Bajeti ni kitu cha awali kama unataka kabisa kwenye kuendea kuwa na website. Siku hizi teknolojia imerahisishwa, unaweza kuwa na website inayoendana na bajeti yako. Siyo lazima uwe na mamilioni ili uwe na website, hakikisha unajieleza ipasavyo pindi unapowasiliana na watengeneza website ili kuwafahamisha ukomo wa bajeti yako na wao wataweza kukupa website iliyo ndani ya kikomo chako.
Kwa mfano, kuhost website ya kawaida haizidi elfu 60 za Kitanzania kwa mwaka,na kutengeneza website ya kawaida pia huanzia laki tatu za Kitanzania kwa kampuni ya kawaida,ingawa wapo wanaochaji chini au zaidi ya hapo. Kwa wamiliki wa makampuni makubwa kama Facebook au Google yanatumia mabilioni kuhakikisha website zao zinakuwa hewani bila tatizo. soma zaidi makala hii blogu ya Mjengwa

0 Response to "HATUA 5 ZA KUPITIA ILI KUMILIKI WEBSITE YA BIASHARA YAKO"

Post a Comment