Dar es Salaam. Wanawake wafanyabiashara kwenye sekta isiyo rasmi wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kuteua mtu mmoja kutoka miongoni mwao ili kuwawakilisha kwenye Bunge Maalumu la Katiba.Wafanyabiashara hao wanatoa ombi hilo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa Bunge Maalumu la Katiba, ambalo linatarajia kufanyika baada ya kupatikana rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
Mbali na kutaka kupewa nafasi ya kutoa mwakilishi kwenye Bunge hilo, wajasiriamali hao wametaka kuendelea kupewa elimu kuhusu Katiba, kwani wengi wao hawafahamu ni kitu gani na hawakushiriki kwenye hatua za mwanzo za kuiandika.
Sababu ambazo wanadai zilisababisha kutoshiriki kwa wingi kwenye hatua za mwanzo za mchakato huo, ni pamoja na kutingwa na shughuli nyingi za kutafuta kipato, jambo ambalo wanaamini kama watapata mwakilishi kwenye Bunge Maalumu la Katiba itasaidia kuwasilisha maoni yao kwa kina.
Mapendekezo yao
Wakitoa mapendekezo yao, wajasiriamali hao wanasema kwa kuwa Rais Kikwete ana mamlaka ya kuchagua wajumbe 166 kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba, hivyo kwa nafasi yake wanamwomba achague mwakilishi mmoja kutoka kwao.
Mwakilishi kutoka soko la Mchikichini, Manispaa ya Ilala, Beth Mtewele anasema, “Kwa kweli mchakato huu wa Katiba Mpya umetusahau wafanyabiashara ndogondogo, kwani hatukushirikishwa kikamilifu.
Anaongeza; “Idadi kubwa ya wanawake walio masokoni hawakushirikishwa kwenye mchakato wa Katiba, jambo linalosikitisha kwani huenda haki zetu za msingi zikapotea.”
Anafafanua kwamba tatizo ni kutopewa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye mchakato huo na Katiba kwa ujumla.
Mfanyabiashara mwingine kutoka Manispaa ya Ilala, Consolata Kiiza anasema, “Tunaomba Katiba Mpya itukumbuke wafanyabishara ndogondogo, kwani rasimu ya kwanza imetusahau, na wengine hata sura ya Katiba ya zamani hatuijui.”
Anaongeza; “Mwanamke ni nguvu ya taifa, hivyo ni vyema tukapewa kipaumbele kwenye Katiba Mpya kwa kuwa njia hiyo ndiyo fursa pekee inayoweza kumlinda mwanamke kupata haki zake ma hivyo kujenga.SOMA HABARI HII KWA UNDANI ZAIDI KATIKA TOVUTI YA MWANANCHI HAPA
0 Response to "WAJASIRIAMALI WATAKA MWAKILISHI BUNGE LA KATIBA"
Post a Comment