Pichani juu, Mrembo akiwa katika hali ya kawaida kabla hajaanza kuyachomoa macho yake nje na kuyarudisha tena ndani mithili ya kinyonga. |
Chini ni video ya mrembo akionyesha namna anavyoyachomoa macho yake na kuyarudisha tena ndani mithili ya kinyonga au kamera ya 'kuzoom'.
Hebu nieleze ndugu yangu ikiwa ni wewe umekumbwa na mkasa kama huo na haukuwa umekutana tena na mtu wa namna ile katika maisha yako yote huko nyuma ungelichukua hatua gani?. Utafunga mlango utoke nje mbio…., utaanguka chini na kuzimia.……, au utafanya kitu gani? Hebu toa maoni yako hapo chini baada ya kumaliza kuisoma hii habari tafadhali.
Pichani chini ni mrembo katika hatua za mwazo
za kuchomoa macho yake nje na kisha kuyarudisha tena ndani.
Pichani chini ni mrembo jicho likiwa limeshamtoka pima.
Kitendo au tuseme kipaji cha kuyachomoa macho nje na kuyarudisha ndani “Eye popping” kwa kimombo siyo cha kawaida sana kwa watu wengi. Hata mtu unapofikiria kufanya hivyo, unashangaa ni vipi inawezekana lakini Dunia hii imejaa maajabu mengi, kuna watu tena wengi tu wenye uwezo wa kufanya hivyo. Tena wengine wameweza kuufikia uwezo huo ‘simply’ tu kwa kufanya mazoezi kidogokidogo na wala siyo ndumba(uchawi) kama baadhi ya watu wanavyoweza kudhania.
Kitaalamu
Madaktari kitendo hiki hukiita “Globe Luxation” Wanasema kwamba mhusika anachofanya
ni kuikaza kwa nguvu misuli na mishipa
yake ya damu iliyoko kati ya macho na
kichwa, kitendo ambacho humfanya mhusika kuhisi vibaya lakini kwa kawaida hali
hiyo haiwezi ikasababisha madhara ya kudumu.
Mbrazili
mmoja aitwaye “Claudio Paulo Pinto” ambaye hapo mwaka 2006 aliwahi kupigania
ili awekwe katika kitabu cha kumbukumbu za rekodi za Dunia “Guiness Book of
Records” aliwahi kusema kwamba, yeye alianza kufanya mchezo huo tangu alipokuwa
na umri wa miaka 9 na wala huwa hasikii maumivu anapoyachomoa na kujarudisha
ndani macho yake kama watu wanavyofikiria.
"Claudio Paulo Pinto" kabla na baada ya kuyachomoa macho yake
|
Hapa ni Pinto akizidi
kuyachomoa macho yake nje.
|
Pinto
alikuwa na uwezo wa kuyachomoa macho yake kwa urefu wa milimeta 7 sawa na inchi
0.3 na alidai kuwa kwa wakati huo
alikuwa na uwezo mara mbili ya huo. Hii inamaanisha kwamba ikiwa ni kweli
basi angeweza kumpiku “Kim Goodman” wa
Chicago ambaye kwa wakati huo ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia
katika ‘Guiness book’ kwa kuwa na uwezo
wa kuyachomoa macho yake hadi kufikia
urefu wa milimeta 11 sawa na inchi (0.43)
Macho
kutoka nje ‘dizaini’ hiyo pia kunaweza kusababishwa na magojwa fulani ya macho
ambapo miwani maalumu au lensi huhitajika ili mgonjwa aweze kuona vizuri. Yupo
jamaa mwingine huko Liverpool nchini Uingereza kwa jina “John Doyle” mwaka huu
amewashangaza watu kwa kitendo chake cha kuyachomoa macho. Ameweka hadi video
yake kwenye “You Tube” akichomoa macho huku muziki mzuri ukipigwa jambo ambalo
limewafanya maelfu ya watu kuvutiwa na video hiyo.
"John Doyle" akipimwa
urefu macho yake yalipofikia.
|
Hebu
na wewe mtazame hapo chini na kusikiliza muziki mtamu alioutumia katika video
hiyo huku akiyatoa macho yake utadhani kinyonga vile. Amesema anayo matumaini
ya kujitengenezea ajira ya uhakika
kupitia kipaji chake hicho cha kuchomoa macho ikiwa ni pamoja na kuvunja
rekodi ya dunia ili aingie katika kitabu cha kumbukumbu za ‘Guiness’.
Kama umewahi kuziona zile kamera zenye uwezo wa “kuzoom out” na “kuzoom in” basi watu hawa macho yao hayana tofauti na hizo kamera. Mwanamke ambaye video yake unaiona ple mwanzoni kabisa mwa hii stori alipoulizwa ni jinsi gani anaweza kufanya vile alijibu mbele ya umati wa watu kwamba anaweza kutokana na kufahamu namna ya ‘kuicontol’ (kuidhibiti) misuli yake ya macho na alipotakiwa kusema ni muda gani amekuwa akifanya vile alijibu ni miaka 10.
Kweli dunia imejaa maajabu, hata mimi hapo kabla sikuwa nafahamu kabisa kitu hiki mpaka hivi karibuni nilipokutana nacho mtandaoni.
ReplyDelete