Veronica Kibuga (katikati)
akiwa na wanawe
Hali hii ndiyo iliyomkuta Veronica Kibuga (85) mkazi wa
Kitongoji cha Kahangala wilayani Magu, Mwanza ambaye kwa miezi kadhaa amekuwa
akiishi kwa hofu kwani anasubiri utekelezaji wa ‘adhabu ya kifo’ kukatwa kwa
mapanga kutokana na tuhuma kuwa yeye ni mchawi.
Ujumbe uliotumwa kwake uliandikwa kwa
lugha ya Kisukuma na ulikutwa kisimani ambako
waliupeleka walipokwenda kuteka maji na unasema: “Bamayo yashikaga izamu igawo
ya kukatwa mapanga”, ukimaanisha: ‘Imefika zamu yako ya kukatwa mapanga’.
Majirani wamejaa nje ya nyumba ya Kibuga kwani wanafahamu fika
kwamba mwandishi wa ujumbe ule hatanii, kwani wote waliowahi kupata ujumbe kama
wake waliuawa. Huyu ni mmoja, lakini ukweli ni kwamba wanawake wengi, hasa
wazee wanaishi na makovu na wengine wamepoteza maisha baada ya kupokea taarifa
kama hizi.
Wakati dunia nzima ikisherekea Siku ya Mwanamke Duniani leo hii,
wanawake wa aina ya Kibuga wako ndani wamejifungia wakihofu usalama wao
kutokana na kuishi katika jamii ambayo inamwona kama mkosi na chanzo cha
matatizo yote.
Wanawake wanasherehekea leo na kutukuzwa kwa mchango wao mkubwa
katika masuala mbalimbali, lakini wapo wanaohitaji ukombozi ili watoke kwenye
madhila ambayo yamewafanya kuishi kwa wasiwasi mkubwa.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWasamaria wema serikali pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserekali tungefanya jitihada za kuwawezesha hawa kinamama kupata nyumba imara ya kuwakinga na hao ‘majangili’ au hata kuhakikisha wanahama kabisa eneo hilo na kwenda kuishi sehemu nyingine iliyokuwa salama zaidi. Pia wananchi tuache unafiki, sisi wenyewe ndiyo tunaendekeza imani hizi za kishirkina, lakini ujue kama leo hii ni kwa Veronika Kibuga na mabinti zake, inawezekana kabisa siku nyingine ikawa ni wewe, bibi yako, mama yako, shangazi, mjomba, mama mdogo au yeyote yule anayekuhusu.
ReplyDeleteHakuna asiyezeeka, hata mtoto mdogo anayezaliwa leo ipo siku atazeeka kama Mungu atamjalia uhai. Tuachane na fikra hizi za kale, Dunia sasa hivi inakumbwa zaidi na matatizo hasa ya umasikini na wala siyo uchawi, vifo, magonjwa na mikosi mbalimbali asilimia kubwa kama siyo 100% vinatokana na umasikini tuliokuwa nao.Tutafute njia na mikakati ya kisayansi ya kuondokana na umasikini na siyo kuanza kutuhumiana uchawi usiokuwa na msingi wowote ule.