Mchanganuo wabiashara au mpango wa biashara unahitajika na watu mbalimbali ukiwemo wewe
mwenyewe mmiliki wa biashara na umuhimu wake kwako wewe mwenyewe biashara
tofauti na inavyodhaniwa na watu wengi, ni mkubwa zaidi hata kushinda wadau
wengine kama benki taasisi za fedha na wabia. Hebu tutazame sasa ni watu gani
wanaohitaji mpango wa biashara,
1) Wale wanaotaka kuanzisha biashara mpya ni
lazima wawe na mipango ya biashara ili kufahamu kwa uhakika ikiwa biashara zao
zitalipa pamoja na kusaidia kuwaonyesha njia ni kitu gani wanapaswa kufanya ili
wafanikiwe. Kama unafanya biashara pasipo
kuwa na mpango wa biashara ni sawa na mtu anayetembea njiani angali amefumba
macho.
2) Wenye biashara zilizokwisha anzishwa
siku nyingi nao wahahitaji mipango ya biashara ili kuzipanua
na kuziboresha zaidi pamoja na kuitumia katika kuomba mikopo kutoka taasisi
mbalimbali za fedha.Utakuwezesha kufahamu pale ulipo, ulikotoka na unakotaka
kwenda.
3) Wawekezaji, mameneja wa mabenki na wabia
huhitaji kuona michanganuo ya biashara inayogusa maeneo yote yanayoihusu
biashara ili wajiridhishe kuwa ni kweli mjasiriamali amejizatiti na yuko makini
na kitu anachotaka kukifanya.
4) Ikiwa wewe ni mfanyakazi katika taasisi
fulani ni lazima bosi ama mabosi wako wahitaji mchanganuo
kamili wa biashara kwa miradi itakayoanzishwa na taasisi kwa ajili ya
utekelezaji.
5) Wanafunzi katika taasisi mbalimbali za
elimu kama vyuo vikuu na vituo vya kuendeleza biashara
ndogondogo pamoja na wahadhiri wao au wakufunzi huhitaji michanganuo ya
biashara katika kujifunza ujasiriamali na namna ya kuiandika michanganuo
yenyewe.
0 Response to "NI AKINA NANI WANAOHITAJI MPANGO/MCHANGANUO WA BIASHARA?"
Post a Comment