Tukiwa leo hii
tarehe 12 june tukiadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ya kupinga kutumikishwa
watoto wadogo na ajira mbaya, yafaa kila mpenda utu Duniani kujiuliza ni kwa
namna gani popote pale ulipo iwe ni nyumbani kwako, barabarani, kazini na hata
safarini jinsi unavyoweza kushiriki katika kuzuia mateso kwa watoto wadogo.
Masikini kundi hili
la watu haliwezi kujitetea lenyewe. Hata ikiwa mtoto atapata mateso makalikiasi gani, mfano ni yule mtoto wa boksi, ni vigumu sana kujitetea, huumia
kimya kimya mpaka anakufa, labda tu atokee msamaria atakayebaini hali hiyo na
kumuokoa.
Sasa kila mtu
angehakikisha katika mazingira anamoishi ama kufanya kazi anakuwa mlinzi wa
mtoto, maharamia wanaowadhulumu wasingelipata nafasi kwani wangeripotiwa mapema
kwenye jamii husika na vyombo vya usalama kabla hali haijawa mbaya zaidi kwa
mtoto husika.
Ikumbukwe kuwa mtoto
siyo lazima awe anaonekana na umbile dogo kama wa miaka 2 au 3, watoto wengine
hasa wale wa kike utakuta wana maumbile makubwa jambo linalosababisha ‘mijibaba’
hasa ile miroho na isiyokuwa na chembe ya huruma kudhania ni wakubwa wenzao na
kuanza kuwahadaa ili kuwaingiza katika mambo mbalimbali ya kikubwa iwe ni
mapenzi, kazi ama hata kuwatamkia maneno yasiyostahili katika umri wao.
Tuache ile tabia ya
kudai eti “Mtoto wa mwenzio siyo wa kwako bali ni mkubwa mwenzio” Kabla haujamtumikisha mtoto wa mwenzio katika
mazingira magumu au kumtendea unyama wa kutisha, hebu kwanza jiulize kama
angelikuwa ni wa kwako je, ungeliridhika Tu afanyiwe hivyo?
0 Response to "UNAWALINDAJE WATOTO WADOGO POPOTE PALE ULIPO NA MABAYA?"
Post a Comment