Maandamano ya Hong Kong kudai Demokrasia |
Ni kimbele mbele hihikihiki
kilichosababisha Iraq kutumbukia katika lindi la maafa makubwa, kwa kisingizio
cha kuleta demokrasia. Afganistan, lLibya, Misri, na sasa Syria na Ukraine.
Koote huko tangu wapandikize maafa hayo wala hakujatulia, moto bado ungali
unawaka, pasipokuwa na hata chembe ya aibu, Obama na Cameroon wanadiriki eti
kutamka, “Tupo pamoja na wanaoandamana nchini Hong Kong
kupinga sera za China Bara dhidi ya
sheria zake za kuchagua wagombea katika jimbo lake hilo“.
Cha ajabu kabisa ni
pale Mataifa haya ya Magharibi yanapojifanya kuwasaidia wale wanaojiita
wanademokrasia ‘pro-democracy’na kisha bada ya kufanikiwa kuziondoa serikali
zinazodaiwa kuwa za kidikteta, wanageuka kuwa magaidi hatari, ukitaka kuona
mifano angalia Syria, Iraq na Libya. ISIS ni mfano mzuri na makundi yanayoisumbua serikali
dhaifu ya Libya iliyojigamba kumng‘oa
Muhamar Gadafi. Magaidi na wenye uroho wa kutawala hujinufaisha sana na
vuguvugu la kudai demokrasia kwani wanajua hakuna kitu kingine Mataifa ya
Magharibi wanachopenda kama madai ya demokrasia hasa katika nchi zile
zinazoonekana kuiminya.
Wako radhi kusaidia
chochote, kwa gharama yeyote ile hata ikiwa ni kwa kulipa gharama kubwa kama
wanayoilipa sasa kule Iraq na Syria. Kwa nini hawajifunzi tu? Kwa maoni yangu binafsi sasa naona funzo
watalipata kutoka Uchina, endapo wataendelea na ujinga wao huo wa kila mara
kudai wapo pamoja na wadai demokrasia hata ikiwa wanamageuzi hao ni kikundi cha
wahuni wenye malengo yao binafsi kama ilivyokuwa syria na Libya. Sifikiri kama Xi Jinping atakubali kirahisi rahisi tu
himaya yake kuchezewa.
Hivi kwa
mfano watokee watu leo katika jimbo mojawapo la Marekani mfano jimbo la
Virginia, litake kujitenga, au kudai demokrasia na madaraka zaidi, Obama atakubali kirahisi? Wanahistoria
wanakumbuka jinsi Marekani ilivyopigana vita chungu karne ya 18 katika harakati
za kuzuia mpasuko baina ya majimbo ya Mashariki na Magharibi. Sasa iweje leo
hii wanakuwa wa kwanza kushadidia mipasuko na utengano katika nchi za wenzao?. Uingereza
kukosa kuogopa aibu sidhani kama juzi wangekubali ile kura ya maoni ya
Scotland, hata ushindi wa London dhidi ya kura hiyo kama isingelikuwa vitisho
vya Waingereza, Wascotish ni lazima wangeshinda.
Hali ni
hiyo hiyo katika nchi kama Uhispania, jimbo linalolilia kujitenga la Catalonia
limefanya hivyo kwa miongo mingi pasipo matumaini, na hata kura ya maoni
walioahidiwa itafanyika wiki hii kama wenzao Scotland, nayo katika hali ya
kutatanisha Mahakama kuu imeisitisha, wameshashitukia kura hiyo itapita. Kusema
ukweli hakuna nchi inayopenda kumegeka megeka bila sababu ya msingi, hivyo
Uchina na Hong Kong ingeachwa iamue maswala yake pasipo kuingiliwa na Mataifa
ya kigeni.
Putin kwa
hasira aliamua kuinyakua Kremia kwa nguvu, ni kwa sababu hizi hizi baada ya
nchi za Magharibi kuunga maandamano yasiyokuwa na kikomo yaliyomng’oa Viktor
Yokunovych aliyekuwa akiungwa mkono na Urusi. Namuunga mkono Rais wa Iran
Hassan Rouhan aliyesema juzi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa ”Magaidiwanatengenezwa na zile nchi zinazojidai kueneza Demokrasia Duniani“.
0 Response to "UGAIDI NI KIMBELEMBELE CHA MAREKANI NA UINGEREZA KUENEZA DEMOKRASIA DUNIANI. "
Post a Comment