Anza na Lengo.
Kwanini uko kwenye mitandao ya kijamii? ana nadi
Kuna majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana
kwa bidhaa zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa
usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi zaidi,watakaonunua
mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali hili.
Wapuuze wapinzani wako-
Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza
kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra
na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia nafasi
ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu wanafanya
kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.
Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao
wa kijamii unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua
zile utazipa kipao mbele.
Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika
mitandao ya kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama
hauna fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda
mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam
inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.
Weka lengo rahisi-
Kwa mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia
bloga mmoja kwa siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda
wako kwa sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya
kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato kutoka
kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya
rasilmali zako chache na kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini
utaona kuwa uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya
kijamii yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia
kimkakati.
Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta'' ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio
wanaochosha.Jinsi unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa
wasikilizaji wako na faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana
kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.
Kuwa na sauti.
Watu hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka
kuungana na wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni
yako ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati
ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika mazungumzo''.Ni njia
mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia
watu,kujenga imani yao na kuwawezesha kushiriki zaidi.
Tamba sana kupia Facebook na Twitter.
Mitandao ya kijamii na mauzo kwenye mtandao inaanza na DNA
yako,bidhaa ama huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu
yako kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa
kampuni yako.
CHANZO: BBC
Niko mbioni kufungua biashara ya duka la bidhaa za nyumbani maarufu kama duka la mangi, najitahidi sana kusoma makala zako na hata za waandishi wengine kujifunza ni namna gani nitaifanya biashara yangu inipe mafanikio makubwa
ReplyDelete