Biashara mpya au iliyokwishaanzishwa, zote
zinahitaji mitaji ili ziweze kukua. Mtaji unaweza ukawa ni fedha, au rasilimali
nyingine yeyote inayowekezwa katika biashara. Upatikanaji wa mtaji ni moja ya
mambo yanayokwamisha biashara nyingi na ni changamoto kubwa kwa wale wanaotaka
kuingia katika biashra mpya.
Kabla haujaamua ni wapi utapata mtaji,
kwanza fanya tathmini ya mahitaji yote
ya fedha
na rasilimali zitakazohitajika katika
kuanzisha au kuendesha biashara husika. Zoezi hili mara nyingi hufanywa
wakati unapotengeneza Mchanganuo wa biashara.
Vyanzo vya mtaji.
Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kuzitumia kupata mtaji kwa ajili ya biashara, zifuatazo
ni baadhi ya zile ambazo hutumiwa mara kwa mara;
1. Akiba yako mwenyewe; na hii unaweza ukaipata bada ya kufanya kazi ya ajira, kuuza mali zako
unazomiliki mfano nyumba gari, shamba, ngombe au mazao ya shambani, kupewa
zawadi au ruzuku n.k. Pia unaweza
ukatumia faida inayotokana na biashara unayoifanya.
2. Kuingia ubia na
watu/mtu mwingine ambaye atachangia
kiasi fulani cha mtaji, lakini ukumbuke umiliki wa biashra utapungua kwani
huwezi tena kumiliki kwa aslimia mia moja.
3. Mkopo kutoka kwa
ndugu jamaa na marafiki. Mkopo wa aina hii
chukua kwa tahadhari, ingawa ni njia nzuri mara nyingi huweza
kusababisha ndugu au jamaa mkagombana hata kuuana. Hakikisha unawekeana mkataba
wa maandishi kuepuka utata baadaye.
Njia hii inatumika na watu kwenye jamii katika sura mbalimbali mojawapo
na maarufu sana ni upatu au Michezo. Michezo uzuri wake haina
riba, lakini ubaya wake ni kule kutokuwa na uhakika na kuaminika, mtu anaweza
akachukua wa kwanza na itakapofika zamu ya kuwachangia wenzake akaanza kupiga
chenga. Na kwa kuwa hakuweka dhamana yeyote inakuwa vigumu kumlazimisha alipe.
4. Mkopo wa
benki/taasisi za kifedha; Hii ndiyo njia
inayotumiwa na watu wengi zaidi ukiacha ile ya akiba binafsi kutokana na taratibu zake kuwa wazi na zisizoleta lawama.
Ipo mikopo ya muda mrefu na mfupi na
yote mkopaji hukatwa riba asilimia fulani.Tatizo
kubwa kwenye mikopo ya aina hii ni wajasiriamali wengi hasa wale wadogo kukosa
sifa za kukopa hasa katika suala la
dhamana.
5. Karadha; Badala ya kukopa fedha, unakopa zana za kufanyia kazi au vifaa mfano, mashine,
gari, friji nk. umiliki wa vifaa hivi hubakia kuwa ni mali ya mkopeshaji, na
wewe unayekopa humlipa gharama za kukodi, faida yake ni kwamba fedha ambazo
ungenunulia vifaa hivyo unaweza
ukafanyia mambo mengine katika biashara na hivyo kufanya mtiririko wako
wa fedha kuwa mzuri zaidi.
6. Kuuza madeni kama unadai wateja; unakubaliana na mtu au kampuni nyingine kudai madeni badala yako.
7. Kukopa kutoka
kwa wanao kuuzia malighafi au bidhaa, unaweza ukapokea bidhaa au malighafi baada ya kuuza ndipo ukawalipa
fedha zao na hii huweza kuchukua muda wa mwezi mmoja miwili au muda wowote
mtakaokuwa mmekubaliana.
Kazi yenu nakubali sana
ReplyDelete