Biashara ya kuuza vocha za simu za mkononi, kwa jumla na hata kwa rejareja kama ilivyokuwa biashara nyingine yeyote ile ina changamotozake mbalimbali moja wapo ikiwa ni mahesabu ya mara kwa mara hasa wakati unapokwenda kununua kutoka kwa yule anayekuuzia kwa jumla, iwe ni mtu binafsi ama kampuni.
Inampasa mtu kuwa makini sana na hesabu kuhakikisha
kwamba ni sahihi na haupunjwi hata senti
tano ukizingatia kuwa biashara hii ya uuzaji wa vocha, iwe ni kwa jumla au rejareja, faida yake ni asilimia ndogo sana na inakubidi uuze vocha kwa kiasi
kikubwa sana ndipo uweze kuona faida kubwa. Uzuri wake tu ni kwamba hazikai,
hutoka chap chap.
Kutokana na uzoefu wangu binafsi, biashara ya vocha za simu za mkononi, inahitaji ujue hesabu hasa kuzidisha idadi ya vocha mara bei yakununulia/kuuza vocha mojamoja na kisha kujumlisha kiasi cha thamani ya kila
aina ya vocha kwa mfano tuseme unauza
vocha za jumla na mteja anakuja na karatasi yake ameorodhesha vocha zote
anazohitaji kama ifuatavyo,
(A)
Karatasi za Orodha ya manunuzi ya vocha duka la jumla.(aina 2) |
Kuepukana na kupiga hesabu ndeefu...! Kama hii iliyoonyeshwa
hapa chini ukizidisha voda za 5,000 mara 4,750/- na kuendelea mpaka Zantel ya 500
mara 475/- na kisha uje ujumlishe zoote...!, ipo njia rahisi ambayo muuzaji wa vocha za
jumla anaweza akaitumia na kuokoa muda ambao wateja wake wangesubiri kwa foleni
wakati akikokotoa kila aina ya vocha, hivyo kuwapunguzia kero.
(B)
|
Unachopaswa kujua ni kwamba, makampuni karibu yote ya
simu za mkononi, vocha zao zote wameweka asilimia ya faida inayofanana katika mauzo. Mathalani katika kila vocha,
haijalishi ni ya shilingi elfu kumi, elfu mbili ama ya mia tano, zote asilimia
ya faida katika mauzo ni 5%. Hii ina maana
kwamba ukiuza vocha tuseme labda ya shilingi 10,000/- faida yake ni sh( 5%*10,000/)
ambapo ni sawa na na shilingi, 500/- Halikadhalika vocha ya shilingi 500, ni (5%*500 ) sawa na shilingi. 25/-
Badala ya kuzidisha bei ya kununulia kila vocha na idadi
ya vocha moja moja na kisha uje kujumlisha tena zote kupata jumla ya fedha zinazotakiwa
kununua vocha zote kama inavyoonyesha hapo
juu katika kielelezo (B);
Zidisha kila idadi ya vocha mara bei ya kuuzia ambayo huwa rahisi hata kwa
kichwa pasipokuhitaji ‘calculator’ wala kufikiri sana kwani
tarakimu zake mara nyingi huishia na ‘000’ mwishoni, kwa mfano unajua vocha ya sh. 5,000 zikiwa mbili jibu lake ni elfu,10,000 nk. badala kama ingelikuwa katika bei ya manunuzi tuseme labda sh. 4,750 ambayo tarakimu zake inakulazimu kutumia mashine ya hesabu(Calculator). Halafu jumlisha thamani ya aina zote za vocha kama kielelezo C kinavyoonyesha hapa chini;
(C)
Dhamani katika bei ya kuuzia vocha
tarakimu zake ni rahisi kukokotoa.
|
na ukishapata jumla yake sasa jibu hilo zidisha
mara asilimia 5% ili kupata faida kwa jumla ya vocha zote.(220,000 * 5/100 = 11,000/-) Baada ya hapo, ili
kupata kiasi cha fedha za manunuzi, toa faida hiyo kwenye kiasi cha fedha katika bei ya kuuzia ulichopata hapo juu katika (C); (220,000 - 11,000 = 209,000/-
Njia hii ni rahisi na ya haraka, na ili mteja kuwa na
kumbu kumbu unamwandikia chini ya
karatasi kiasi cha pesa alicholipa tu, hata ikiwa umekosea, na yeye akienda
kurudia hesabu akirudi ni rahisi
kurekebisha, kwani unajua kiasi alicholipa na ni wewe uliyeandika kwa mkono
wako.
Tena ili kufanya mambo yawe rahisi zaidi na muda uzidi kuwa mdogo, wala hauna haja ya kuweka dhamani kila mbele ya vocha, wewe unaweza hata kujumlisha kwa kichwa na ukatumia mashine wakati wa kuzidisha na ile asilimia 5% tu, na jibu ndilo utakaloandika pale chini ambalo ndiyo kiasi atakacholipa mteja unayemuuzia kama kielelezo kifuatacho kinavyoonyesha hapa chini;
(D)
Kukokotoa
hesabu ni rahisi, huchukua muda mfupi na karatasi haichafuki.
|
Jibu utakalopata (209,000/-) ni sawa sawa na ambavyo ungepata kama ungelitumia njia ndefu na ngumu inayochukua muda mrefu(kielelezo B), labda tu, itokee kuna vocha faida yake imepigwa kwa viwango tofauti, na mara nyingi huwa ni zile za Sh. 500, badala ya 475 wengi huuza 480, hata hivyo ni mara chache sana hutokea na hata ikitokea basi tofauti huwa ni kidogo sana, utakuta hesabu inazidi au kupungua siyo zaidi ya shilingi mia mbili mpaka mia nne.
Kwa muuzaji vocha wa rejareja wakati unapotaka kununua vocha kwa ajili ya kuja kuuza, ukisha tengeneza orodha yako, fanya hesabu hiyo ili kujua kabla, iwapo vocha zako zitagharimu kiasi gani cha pesa. Hasa kwa wale wanaowatuma watu wengine wakawanunulie inakuwa vizuri zaidi kwani unampa kiasi kamili kinachohitajika.
Kwa muuzaji vocha wa rejareja wakati unapotaka kununua vocha kwa ajili ya kuja kuuza, ukisha tengeneza orodha yako, fanya hesabu hiyo ili kujua kabla, iwapo vocha zako zitagharimu kiasi gani cha pesa. Hasa kwa wale wanaowatuma watu wengine wakawanunulie inakuwa vizuri zaidi kwani unampa kiasi kamili kinachohitajika.
Ndugu msomaji wa blogu hii, una maoni gani juu ya uendeshaji wa biashara ya uuzaji wa vocha za simu za mkononi? Je, kuna mbinu yeyote ile unayoitumia katika kuifanya biashara hii kuwa rahisi zaidi kwako? Au makala hii unaionaje, kuna chochote cha manufaa ulichojifunza? Hebu tushirikishane kupitia njia ya maoni hapa chini. Asante.
Niliwahi kununua vocha za jumla duka moja, nikastaajabu kasi ya ajabu muuzaji aliyokuwa nayo, kisha alinirudishia karatasi ikiwa imeandikwa pale chini jumla ya kiasi cha pesa nilizotakiwa kulipa. Makala hii leo ndiyo imenitegulia hicho kitendawili, nimefurahi, ni makala nzuri inayoelimisha.
ReplyDeletenimeipenda mkuu kuna jambo ningeomba unisaidie. naweza nikapata contact zako. za kwangu 0755761778/0713945970
ReplyDeleteasante sana
Mkuu wasiliana nami kwa namba 0712202244 au 0765553030 au baruapepe: peter@jifunzeujasiriamali.com
DeleteNapenda kujua kuhusu supplier mkubwa wa vocha kilimanjaro na arusha nitampataje
ReplyDeleteTatizo mimi sijuwi wapi zinauzwa vocha kwa bei ya jumla kwaajili ya wauzaji wa jumla,maana mimi nataka niuze vocha kwa bei ya jumla.Niko Kiluvya Pwani.
ReplyDelete