Kitabu “Think & Grow Rich",(Fikiri Utajirike) au Msahafu wa Mafanikio, kilichoandikwa na Andrew Carnegie miaka 70 iliyopita, hakuna shaka yeyote kuwa ndiyo kitabu pekee duniani cha elimu ya pesa na mafanikio maarufu cha wakati wote.
Siku za nyuma tuliahidi kukitafsiri katika tovuti ya jifunzeujasiriamali.com, na tulifanya hivyo kwa Dibaji na sura ya kwanza tu na kuahidi sura zinazofuata tutaziweka katika blogu hii. Kuanzia leo tumeanza tena kuweka mfululizo wa sehemu za kitabu hicho kidogo kidogo ila safari hii hatutasitisha tena, ni kila siku fuatana nasi usikose. Ikiwa hukusoma Dibaji na sura ya 1 basi fungua hapa kusoma.
Wakati Edwin C. Barnes aliposhuka kutoka kwenye treni ya
mizigo katika mji wa Orange, NJ. Ungeweza ukamfananisha na mzururaji, lakini mawazo yake yalikuwa ni
sawa na ya mfalme!.
Akiwa anaelekea ofisini kwa Thomas A. Edison akili yake
ilikuwa kazini. Alijihisi mwenyewe kama vile tayari alikuwa mbele ya Edison.
Alisikia sauti ndani mwake ikimuomba Bwana Edison fursa ya kutekeleza jukumu
zito katika maisha yake, shauku kuu ya kuwa mbia kibiashara
na mgunduzi mkubwa.
Shauku ya Barnes haikuwa matumaini wala matamanio.
Ilikuwa ni shauku kali iliyokuwa ikimbubujika na iliyopitiliza kila kitu.
Ilikuwa dhahiri.
Shauku hiyo haikuwa mpya alipomsogelea Edison. Ilikuwa
shauku aliyokaa nayo Barnes kwa muda wa kipindi kirefu. Mwanzoni wakati shauku
ilipojitokeza kwa mara ya kwanza akilini mwake, ingeweza kuwa, na pengine
ilikuwa ni matamanio tu, lakini haikuwa tena matumaini matupu pindi alipofika
mbele ya Edison.
Miaka michache baadae, Edwin C. Barnes akaja kusimama
tena mbele ya Edison katika ofisi ileile alipokutana na huyu Mgunduzi. Safari
hii hamu yake ikiwa imeshageuka kuwa kweli. Alikuwa katika biashara na Edison.
Ndoto iliyokuwa imetawala katika maisha yake ilikuwa imegeuka kuwa kitu halisi.
Leo hii wanaomfahamu Barnes humuonea wivu kutokana na
mafanikio aliyojaliwa maishani. Wanamuona katika siku zake za furaha, bila ya
hata kujisumbua kuchunguza sababu za mafanikio yake.
Barnes alifanikiwa kwasababu alichagua lengo dhahiri, na
akaelekezea kwalo nguvu zake zote, matumaini yake yote pamoja na jitihada zake
zote katika kulitimiza lengo hilo. Alikuwa yuko radhi kuanza na kazi ya chini
kabisa, ilimradi tu kazi hiyo ingempatia japo fursa ya kupiga hatua moja
kuelekea lengo alilokuwa amelitunza.
Miaka mitano ilipita kabla hajafanikiwa kuipata nafasi
aliyokuwa akiitafuta. Kwa kipindi chote hicho hakuwa na mwanga wowote wa
matumaini, wala ahadi moja ya kufikiwa kwa shauku yake.
Kwa kila mtu, isipokuwa yeye mwenyewe, alionekana tu kama
jino
jingine la gurudumu(kitu kisichomuhimu) katika gurudumu la biashara ya
Edison. Lakini ndani ya akili yake mwenyewe alijua alikuwa mbia wa Edison kila
sekunde iliyokuwa ikipita, kuanzia siku ya kwanza kabisa alipokwenda kuanza
kazi pale.
Huu ni uthibitisho mkubwa wa nguvu ya shauku iliyokuwa
wazi. Barne’s alishinda lengo lake kwasababu alitaka kuwa mbia kibiashara na
Bwana Edison zaidi kushinda alivyotaka kitu kingine chochote kile. Alitengeneza
mpango ambao kwa kupitia huo aliweza kutimiza lengo hilo. Lakini “aliteketeza
moto madaraja yote yaliyokuwa nyuma yake” Alisimamia shauku yake mpaka ilipogeuka kuwa jambo
lenye kutawala maisha yake na mwishowe kuwa kitu halisi.
Alipokwenda katika mji wa Orange, hakujisemea mwenyewe,
“nitajaribu kumshawishi Edison anipe kazi ya aina fulani” Alisema “nitamuona
Edison na kumpa ujumbe kuwa, nimekuja kuingia naye ubia wa biashara”
Hakusema, “Nitafanya kazi pale kwa miezi michache, na
ikiwa kama sitapata motisha, nitaacha na kutafuta kazi mahali pengine” Alisema,
“Nitaanza popote, nitafanya chochote Edison atakachoniambia nifanye lakini
kabla sijakamilisha, nitakuwa nimeshakuwa mbia naye”
Hakusema, “Nitakuwa macho kwa fursa nyingine, ikitokea
nikishindwa kupata ninachotaka kwenye kampuni ya Edison”, Alisema, kuna kitu
kimoja tu katika Dunia hii ninachonuwia kuwa nacho, nacho ni ubia wa kibiashara
na Thomas A. Edison. Nitayaunguza madaraja yote yaliyoko nyuma yangu, na kuweka
rehani mustakabali wa maisha yangu yote yajayo kusudi niwe na uwezo wa kupata
kile ninachokitaka”.
Mwenyewe binafsi hakujiachia kabisa uwezekanao wa kurudi
nyuma. Ilikuwa ni lazima aidha ashinde au afe! Na hiyo ndiyo historia ya
mafanikio ya Barnes.
Hapo zamani za kale, Mpiganaji mashuhuri alipaswa kufanya
uamuzi ambao ulimhakikishia ushindi katika uwanja wa mapambano. Alikuwa
akijiandaa kupeleka jeshi kupigana na adui aliyekuwa na nguvu, na ambaye idadi
ya wanajeshi wake ilizidi ile yakwake.
Alijaza askari wake kwenye meli na kuelekea nchi ya adui,
aliwashusha askari na vifaa kisha akatoa amri ya kuchoma moto ile meli
iliyokuwa imewabeba. Akiwahutubia askari wake kabla ya pambano la kwanza
alisema, “Mnaiona meli ikiteketea kwenye
moshi, hiyo ina maana kwamba hatuwezi tukaondoka ufukwe huu tukiwa hai ikiwa
kama hatutashinda vita! Sasa hatuna chaguo- ni lazima tushinde, vinginevyo
tuangamie! Walishinda.
Kila mtu anayeshinda kwenye jambo lolote lile gumu, ni
lazima kwanza akubali kuchoma meli yake na kukata vyanzo vyote vinavyoweza
kumfanya arudi nyuma. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo mtu anapoweza kuwa na
uhakika wa kudumisha ile hali ya akili inayojulikana kama shauku kuu(hamu
kubwa) ya kushinda ambayo ni muhimu katika mafanikio.
Sura hii, Itaendelea kesho 'never miss'........!
Ukipenda kusoma mfululuzo wa sehemu zote, huu hapa chini
Kazi njema.
ReplyDelete