Unapoanzisha biashara ama kutaka kuboresha biashara ya zamani, utafiti
ni jambo la lazima endapo mtu utataka upate mafanikio, ingawaje ni jambo
linalogharimu pesa na muda mwingi, lakini gharama hizo haziwezi kamwe kuzidi
hasara ambayo mtu unaweza akaipata
endapo utapuuzia ama kukwepa jambo hili.
Neno upembuzi yakinifu "feasibility study" lina maana sawa na Utafiti isipokuwa
upembuzi yakinifu lina maana pana zaidi. Kwa mfano unaposema utafiti wa masoko
unamaanisha kipengele kimojawapo cha upembuzi yakinifu katika kipengele cha
soko pekee. Vipo vipengele vingine kama vile, bidhaa/huduma, tekinolojia, fedha,
na utawala.
Vilevile upembuzi yakinifu wapo watu wengine huuweka katika aina
za michanganuo/mipango ya biashara ijapokuwa vitu hivi viwili vina tofauti
kidogo kama tutakavyoona huko mbele.
Lengo kuu la kufanya
utafiti/upembuzi yakinifu ni kupata picha
halisi ya biashara itakavyokuwa siku za baadaye na hivyo kwa kutathmini kila hatua utakayopitia unaweza kubaini kama biashara husika italipa au la, na hivyo kukufanya uamue kuendelea nayo au kuiacha. Vile vile kwa kubaini kabla matatizo ambayo yataweza
kuja kujitokeza mbele
ya safari, unaweza ukapanga mapema
mikakati ya kukabiliana nayo.
Utafiti/upembuzi yakinifu
hukupatia taarifa za
msingi zinazohusiana na wazo lako la biashara. Yapo
mawazo mengi ya biashara, mengine yanafaa na mengine hayafai, kupata wazo
fulani la biashara haimaanishi
kwamba litaleta mafanikio/faida. Sababu kubwa ya wajasiriamali wengi
kuanguka mara waanzishapo biashara ni kuwekeza fedha zao na muda katika biashara ambazo hawajazifanyia utafiti wa kina.
Umuhimu mwingine wa kufanya
utatifi wa biashara ni katika kuandaa Mpango
ama Mchanganuo wa Biashara. Kama ilivyoelezwa
katika kitabu cha JIFUNZE MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI, msingi
mkuu wa mpango wa biashara ni yale yale
majibu unayoyapata kutoka katika utafiti wa biashara na masoko/upembuzi yakinifu ulioufanya.
Tofauti yake tu ni kwamba; kwenye utafiti/upembuzi yakinifu, unaorodhesha na kuainisha njia mbalimbali za kufanya biashara,wakati kwenye mchanganuo wa biashara unaonyesha vitendo vinavyotakiwa kufanywa
kusudi wazo la biashara lililopendekezwa liweze kugeuzwa kuwa
biashara halisi. Vilevile tofauti nyingine ni
kwamba utafiti/upembuzi ndio huanza kufanyika kwanza kabla mchanganuo
haujatengenezwa na kutekelezwa
Wakati mwingine utafiti wa
biashara hufanywa na makampuni ya ushauri wa kibiashara, chagua kampuni yenye
uzoefu na biashara unayotaka kuifanya. Pia ukumbuke kuwa, unapompa mtaalam
afanye kazi hii haimaanishi na wewe
hautashiriki, hapana, kila hatua inabidi
uhusike, fahamu kila kitu kinachofanyika na wakati mwingine uhoji
matokeo ya utafiti wenyewe.
Upembuzi yakinifu umegawanyika katika vipengele vikuu 3
vifuatavyo:-
1. Ufafiti wa soko na bidhaa/huduma unayotaka kuuza.
2. Utafiti wa
maswala ya kiufundi na Utawala.
3. Utafiti wa
maswala ya fedha.
Badala ya kutumia njia ya kitaalamu sana kufanya utafiti, mfanyabiashara ndogo ndogo,
asiyekuwa na utaalamu mkubwa wala fedha
za kutosha kuajiri kampuni ya utafiti anaweza akajibu maswali yafuatayo na akawa ametimiza lengo lake la kujua ikiwa biashara anayotaka
kuifanya au kuipanua itamlipa aendelee
nayo ama aachane nayo.
Majibu hayo atayapata kwa
kufanya utafiti usiokuwa rasmi kwa kuingia mitaani na kuuliza watu maswali
mbalimbali, wanaweza wakawa wale wanaofanya
biashara kama ya kwake, wauzaji wa jumla, wauzaji wa rejareja, wataalam
wa biashara, pamoja na kusoma machapisho mbalimbali yanayoelezea sekta
anayotaka kuifanya. Maswali hayo yamepangwa kufuatanana na mtiririko
wa vipengele vile vitano yaani maswali yanayohusu Bidhaa/Huduma, soko, teknolojia/ufundi, maswala ya kiutawala
/management na Maswala ya fedha.
SOKO.
·
Soko lako ni lipi?
·
Walengwa wako ni kina nani?
·
Fahamu tabia za wateja wako ni zipi.
·
Wapo wateja wangapi?
·
Kuna changamoto gani zinazokabili soko hilo?
·
Ni gharama kiasi gani itakayotumika kulifikia soko hilo?
·
Ni nani mshindani wako wa moja kwa moja?
·
Bidhaa zako zinafanana au
kutofautiana vipi na za washindani wako?
·
Ni nini siri yako kuu ya mauzo?
·
Je washindani wako wana
weza kukuiga kirahisi?
·
Washindani wako
wanachukuliaje ujio wako katika soko?
·
Ni nani washindani wako wasiokuwa wa moja kwa moja?
…………………..Inaendelea
sehemu ya 2……
Asante sana kwa maarifa haya ambayo si rahisi kuyapata katika mfumo wetu wa elimu.
ReplyDeletembarikiwe saana na msikate tamaa tunawafuatilia kwa ukaribu sana sana.
hakika mnafanya kazi nzuri sana.
Asante sana
ReplyDelete