Jembe
lisilokuwa na mpini.
|
Kabla
haujatuambia ni nini kilichotokea baada ya kuanza kazi yako hiyo ya
kulima hekari 5 kwa jembe lisilokuwa na mpini, hebu kwanza tuoanishe
kulima shamba kwa jembe lisilokuwa na mpini na kufanya biashara bila
kuwa na mtaji au kuwa na mtaji lakini usiotosheleza mahitaji ya
biashara husika.
Watu
wengi utawasikia wakisema, siyo lazima kuwa na mtaji ndipo uanzishe
biashara, hili ni kweli kabisa asilimia mia moja na wala silipingi.
Ndio maana kichwa cha makala hii nimeanza “Kuendesha
biashara....”
na wala siyo
“Kuanzisha biashara......”
Kuendesha na kuanzisha ni vitu viwili tofauti. Unaweza ukaanzisha
biashara ukiwa na wazo peke yake lakini mtaji wa kuiendesha ukatoka
mahali pengine hata kama hauna hata senti tano. Makala nyingine inayozungumzia vyanzo 7 vya mtaji ni hii hapa unaweza ukaisoma.
Zipo
stori nyingi za watu walioanza bila mtaji, na unapozisikia unaweza
ukadhani kwamba biashara bila mtaji inawezekana tu kirahisirahisi
lakini ukweli ni kwamba siyo jambo rahisi vile. Utakuta baada ya
kuanzisha bila mtaji itafika mahali ni lazima itahitaji mtaji wa
ziada ili iweze kukua vinginevyo basi itabakia vile vile kwa muda
mrefu au hata kufa. Hapa ndipo utakuta mtu akienda benki au taasisi
za fedha kukopa, kukopa bidhaa toka kwa wanaokusambazia, kutafuta
mbia, kuomba ndugu au jamaa akukopeshe, kuomba msaada nk.
Biashara
kama haina mtaji wa kutosha ni mtihani mkubwa! Hebu fikiria, pengine
una duka, anakuja mteja anataka kitu fulani, unamwambia hakuna,
anakuja mwingine ameshika noti ya shilingi elfu kumi, anakwambia nipe
soda, “oo..sina chenji” unamjibu, kweli hauna chenji na wala
siyo kwamba unamkatalia bure, na hata ukifikiri ukaombe chenji kwa
jirani bado unahisi ni kama vile unajisumbua bure kwani ni muda si
mrefu ulienda kuomba ya shilingi elfu mbili na bado ukakosa. Kuna
changamoto nyingi unapoendesha biashara na mtaji usiotosheleza, hizo
ni chache tu.
Biashara
hiyo hiyo pengine ndiyo kila kitu unategemea hapohapo nikiwa namaana
kwamba inabidi ujilipe kiasi kikubwa cha mshahara ili kukidhi
mahitaji yako ya kila siku binafsi na hata ya familia. Biashara hiyo
hiyo inatakiwa ilipe pango la chumba unachofanyia biashara, ilipe
umeme, ushuru wa takataka, kodi ya mapato pamoja na leseni kila
mwaka.
Kuendelea na biashara kwa mtindo kama huo bila ya kuwa na mtaji wa kutosha ni hatari sana itakupotezea muda wako mwingi huku ukimtafuta mchawi anayekuloga bila ya mafanikio. Tafuta mtaji kwa kutumia njia yeyote ile halali uweze kupaa mithili ya ndege badala ya kuendelea kusota chini kama kinyonga au kobe.
Kuendelea na biashara kwa mtindo kama huo bila ya kuwa na mtaji wa kutosha ni hatari sana itakupotezea muda wako mwingi huku ukimtafuta mchawi anayekuloga bila ya mafanikio. Tafuta mtaji kwa kutumia njia yeyote ile halali uweze kupaa mithili ya ndege badala ya kuendelea kusota chini kama kinyonga au kobe.
Hauna
tofauti na yule anayelima ekari 5 kwa jembe lisilokuwa na mpini.
Atasota hapo chini wee! Mpaka msimu wa kulima unamalizika, msimu wa
kupanda nao utakuja utapita hajakamilisha hata robo heka, na hata
msimu mwingine wa kulima utamkutia tena hapo hajasogea hata heka
moja. Atahitaji chakula, gharama mbalimbali pamoja na madawa akiumwa
huku familia nayo ikimsubiri pasipokuona hata mhindi mmoja wa
kuchoma.
Mwishowe
hakuna kitakachokuwa kimefanyika. Tuseme labda angelikuwa na jembe
lenye mpini, kazi ingekwenda harakaharaka, na labda hata jembe hilo
lingekuwa ni lile la kukokotwa na ngombe au trekta basi kazi
ingelikuwa na tija kubwa zaidi.
Soma pia na hii; 'Unaogelea ndani ya maji baridi huku ungali unakufa kwa kiu'
Suala
la mtaji pia hutegemea sana aina ya biashara, kwa mfano, biashara ya
kutoa huduma ni tofauti na ile ya kuuuza au kuzalisha bidhaa. Kutoa
huduma mtu atahitaji mtaji kidogo zaidi na hata zipo biashara zingine
hutahitaji mtaji kabisa kwa maana ya fedha. Uzalishaji wa bidhaa
utahitaji mtaji mkubwa hasa wa fedha kununulia malighafi kabla bidhaa
zenyewe hazijauzwa.
Halikadhalika na uuzaji wa bidhaa ni hivyohivyo, utahitaji kuwa na fedha taslimu za kununua bidhaa husika kabla haujaziuza. Ikiwa hauna uhakika wa kupata mtaji wa kutosha kuendeshea biashara kabla ya kuanza fikiria uwezekano wa kufanya biashara ya utoaji huduma.
Halikadhalika na uuzaji wa bidhaa ni hivyohivyo, utahitaji kuwa na fedha taslimu za kununua bidhaa husika kabla haujaziuza. Ikiwa hauna uhakika wa kupata mtaji wa kutosha kuendeshea biashara kabla ya kuanza fikiria uwezekano wa kufanya biashara ya utoaji huduma.
Una maoni gani ngugu msomaji? au una jambo lolote ungependa kuuliza, basi yaweke hapo chini katika maoni. Asante.
Mnaweza kunikopesha mtaji kidogo? ninataka kuanzisha biashara ya kuuza nafaka.
ReplyDeleteSisi tunashughulika na utoaji elimu kwa wajasiriamali wadogo kupitia njia mbalimbali kama vitabu, mitangao ya kijamii, blogs nk. Hatuhusiki na utoaji mikopo, ila tunakushauri kama unahitaji mkopo basi wasiliana na taasisi mbalimbali za mikopo kama vile benki, saccos, vyama vya kuweka na kukopa au vicoba. Usiogope kwenda kuwaona na kuwaulizia masharti ya kukopa, linganisha sehemu tofauti kuona ni wapi masharti yao utaweza kuyamudu zaidi.
Delete