Rais wa Marekani Barack Obama ameisifu Afrika kwa maendeleo yake ya kiuchumi, akiita, “Moja kati ya maeneo Duniani yanayoku a kwa kasi” Aliyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Ujasiriamali wa Dunia pamoja na mwenyekiti mwenzake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jijini Nairobi.
Katika mkutano wake wa kwanza rasmi tangu alipowasili
jijini Nairobi jana amesema kwamba;
“Afrika inasonga mbele” “Watu wanaondokana na umasikini, vipato vinapanda,
daraja la kati linakua, na vijana kama ninyi wanaitumia teknolojia kwa manufaa
kubadilisha mtindo ambao Afrika inafanya
biashara.” Aliuambia mkutano.
Akichangia jukwaa na Obama, Kenyatta pia alionyesha
matumaini kuelekea mustakabali mwema wa Bara hilo.
“Simulizi za kuvunja moyo kuhusu Afrika ni za uwongo, na
kwa kweli hazijawahi kuwa kweli” Kenyatta alisema. “Waache wajue kwamba, Afrika
ipo wazi na tayari kwa biashara.”
Angalia na kusikiliza hotuba hiyo ya Obama hapa (full speech)
Kongamano hilo linalenga kuchochea biashara itakayowainua Waafrika wengi zaidi kutoka kwenye umasikini na kusaidia kuzikinga jamii dhidi ya wenye misimamo mikali.
Kongamano hilo linalenga kuchochea biashara itakayowainua Waafrika wengi zaidi kutoka kwenye umasikini na kusaidia kuzikinga jamii dhidi ya wenye misimamo mikali.
Obama mara tu alipotua Kenya nyumbani alikozaliwa baba
yake mzazi, umati mkubwa wa watu ulikuwa umejipanga mtsari kusindikiza msafara wa magari na pikipiki,
wakishangilia kwa vifijo na kupunga mikono huku helikopta ikizunguka angani.
Ripota mmoja wa Aljazeera akiwa mjini Nairobi alisema; “Ni furaha isiyo kifani” Obama alipowasili,
akaongeza kuwa Rais wa Marekani ndiyo kiongozi wa kisiasa “mashuhuri zaidi”
nchini Kenya.
Siku ya Ijumaa jioni, Obama aliungana na ndugu zake wote
upande wa baba. Amewahi kusema kuwa hamkumbuki vizuri baba yake aliyemuona angali bado mdogo sana.
Baba yake alizaliwa Magharibi kabisa mwa Kenya katika
kijiji kiitwacho Kogelo, pwani ya ziwa Victoria. Alikuwa mchumi na aliondoka
Marekani Obama akiwa na miaka 2. Aliishi Kenya akifanya kazi serikalini mpaka
mwaka 1982 alipokufa kwa ajali ya gari alilokuwa akiendesha mwenyewe akiwa umri
wa miaka 46.
Mwaka 2006 Kabla hajawa Rais, Obama alifanya ziara
binafsi kijijini Kogelo wanakoishi ndugu zake wengi upande wa baba.
Chanzo: Aljazeera
Chanzo: Aljazeera
0 Response to "HOTUBA YA RAIS BARACK OBAMA KENYA AKIFUNGUA KONGAMANO LA DUNIA LA UJASIRIAMALI"
Post a Comment