Ndoto za kuanzisha biashara ya rejareja hususani duka zinaweza kuwa kweli haraka
na kwa urahisi zaidi endapo mtu atafuata taratibu hizi pamoja na kufanya
maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kamili (mchanganuo) wa biashara yake iwe ni katika karatasi
ama kichwani mwake.
1. Chagua mfumo wa bishara kisheria
Kuchagua mfumo wa biashara yako kisheria ni uamuzi wa
msingi kabisa kabla ya kuanza bishara, kwani kuja kubadili baadaye ni jambo la
ghrama na usumbufu mkubwa.
Mifumo ya biashara kisheria
ipo ya aina tatu;
(a)
Biashara ya mtu bianafsi.
(b)
Biashara ya ubia.
(c)
Biashara ya kampuni yenye dhima ya ukomo
(Limited company)
Biashara nyingi za rejareja hasa zile
ndogo ndogo wanatumia sana mfumo huu wa
biashara ya mtu mmoja au binafsi. Faida na harasa za mifumo yote 3 imefafanuliwa kwa undani sana katika
vitabu mbalimbali kikiwemo kitabu kikubwa “Jifunze
Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”
2. Chagua jina la biashara yako.
Unaweza ukawa na
mpango mzuri sana wa biashara yako ya rejareja lakini ukaipa jina lisilofaa
ukawa umeharibu kila kitu. Kuipa biashara jina ni hatua muhimu sana ingawa
unaweza kuona ni kazi nyepesi tu kufanya hivyo. Ni kazi inayohitaji ufikirie
kwa umakini mkubwa, unapotaka kuipa biashara yako ya rejareja jina
linalofaa zingatia vipengele hivi hapa
chini;
·
Orodhesha kwenye karatasi bidhaa ama huduma unazotoa, maneno yote
yanayohusiana na biashara unayotarajia kuifanya pamoja na mazingira na eneo
itakapokuwa.
·
Fanya
utafiti kwa kuangalia majina ya biashara kama ya kwako zilizokuzunguka,
unanweza pia ukatazama kwenye mtandao wa intanet n.k mpaka utakapopata jina
utakaliona unaridhika nalo.
Jina
linapaswa liwe;
ü Rahisi
kueleweka kimatamshi na kimaandishi.
ü Usichague
jina lenye mlengo hasi mfano mmoja ni
café moja jamaa alitumia jina linalokashifu timu fulani ya mpira.
ü Usichague
jina litakalopotosha watu wala lenye maana zaidi ya moja.
ü Zingatia
herufi jina la biashara yako litakapoanguakia kwenye orodha kama za yellow page
n.k.
ü Chagua
jina litakalowakilisha kile kitu hasa utakachofanya na siyo litakalominya
baadhi ya shughuli zako.
ü Chagua
jina utakalojivunia na siyo litakalokufanya uone aibu hata kuliwakilisha mbela
za watu.
ü Usitumie
majina ya jumla yanayowakilisha vitu jumla mfano; Nafuuu store, Bei rahisi duka
n.k. majina kama hayo ni vigumu kuyasajili kama alama yako ya biashara.
Baada
ya kupata jina la biashara yako, jaribu
kuuliza watu wa karibu ikiwa nao kama
watalipenda. Wakiona linafaa basi lipitishe, ukiona wengi wamelitilia mashaka
unaweza ukarudi tena kwenye orodha yako
upya.
3. Ipe
biashara yako namba ya Utambulisho wa mlipa kodi TIN
Ni vizuri ukaenda
kuisajili biashara yako mamlaka ya mapato “TRA” tawi lililopo karibuni na wewe
wakupe namba ya mlipa kodi (TIN).
Hatua hii hulipi gharama yeyote, ni bure. Baada ya kujaza fomu zao wanakupa
hati na kukufungulia faili ambalo baadae
ndilo huja kulitumia utakapokwenda kulipa kodi ya mapato. Ikiwa biashara yako
ni ndogo sana unaweza ukaianza hivyo hivyo tu bila TIN lakini baadae ukaja kujisajili.
4. Uchaguzi wa ni bidhaa gani utakazouza.
Kwa biashara ya duka la rejareja la mtaani hakuna ukomo
wa bidhaa unazotakiwa kuuza. Cha kuzingatia hapa ni kuangalia katika utafiti
wako uliofanya ni bidhaa zipi unaona wakazi wa eneo husika wanapendelea zaidi
kununua.
Vigezo vingine ni pamoja na faida, angalia ni bidhaa zipi
zenye faida kubwa kwa mfano aina fulani ya maji yanaweza kuwa yananunuliwa kwa
wingi sana lakini faida yake ni kidogo mno. Hivyo ni juu yako kuamua upate
faida kidogo uuze sana au faida kubwa lakini mauzo kidogo.
Angalia pia bidha zinazoendana na wakati uliopo,
ushindani: ukichagua bidhaa za kipekee unaweza ukashindana hata na biashara
kubwa kubwa.
Katika vitu muhimu sana unavyopaswa kufanya kabla
haujaanzisha duka lako ni kuandaa mpango kamili wa biashara, mpango unaweza
kuwa upo kichwani mwako tayari lakini ni vizuri zaidi ukauandika katika
karatasi hata kama hautafuata taratibu
rasmi za kuandika, unaweza tu ukaorodhesha mambo yako yote muhimu unayotarajia
kuyafanya ili kukamilisha malengo ya biashara yako pamoja na gharama
utakazotumia, pia faida au mauzo unayotarajia kwa siku, mwezi au mwaka, na
tayari huo unatosha kuitwa mpango wa baishara yako.
Mwanamke
akiuza duka la rejareja.
|
Ni kama vile unapotoka nyumbani kwenda sokoni kununua
vitu vya nyumbani, unaorodhesha vitu vyote unavyotarajia kwenda kununua kwenye
karatasi pamoja na bajeti ya fedha utakazotumia. Michanganuo ya biashara kwa
undani zaidi pamoja na mifano yake hai imefafanuliwa katika kitabu “Jifunze
Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”
6. Fahamu sheria na taratibu
za mamlaka husika.
Watu
wengi baaba ya kufungua maduka yao miezi miwli, mitatu hushangaa kuona afisa
biashara anakuja na kudai vitu kama
leseni, au watu wa mamlaka ya mapato TRA wakidai TIN namba, wakati mwingine
huja watu wa Halmashauri au serikali za mitaa na kudai leseni za kuuza vileo
ama uwaonyesha sehemu ya wateja kujisaidia (choo) ikiwa biashara ni
grosari au mkahawa. Na wakati mwingine
huja hata matapeli wajanja tu wa mjini kukutisha wakijua kabisa hukufuata
taratibu za vibali ili uwape hongo ya pesa.
Usihatarishe biashara yako uliyoilipia pango
fedha nyingi na kupoteza muda wako wa thamani, hakikisha unafuata taratibu zote
hasa kupata vibali kama TIN namba,
leseni kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wako au manispaa na vibali vinginevyo
ikiwa ni biashara kwa mfano kama ya
kuuza madawa ya binadamu itabidi uende mamlaka ya chakula na dawa TFDA.
Duka la rejareja la vyakula. |
Fungua hapa kujua hatua 10 za kuanzisha biashara ya rejareja (DUKA) sehemu ya ii
biashara ya duka inasheria ya kupima afya kwa muzaji
ReplyDeletenakala nzuri kabisa
ReplyDelete