Kuna wakati niliwahi kuandika makala isemayo, “HAKUNA UTAJIRI WA MIUJIZA KWENYE MITANDAO:FANYA KAZI”, makala hiyo, sikuwa na maana kuwa haiwezekani mtu akatengeneza
pesa kupitia mtandao wa intaneti au katika blogu na tovuti, bali maana yangu
ilikuwa kwamba. “unaweza ukapata utajiri wa pesa au mali kwa njia ya kupitia
mtandao wa intaneti, lakini siyo kimiujiza kama watu wengi walivyokuwa
wakifikiria hapo kabla.
Miaka tuseme kama mitatu
mpaka mitano iliyopita, dhana hii ya kujiingizia kipato kupitia mtandao wa
intaneti ilikuwa bado ni changa sana hapa Tanzania, na kwa kweli watu wengi
walikuwa na fikra nyingi hasi ama zisizokuwa sahihi juu ya utajiri wa kwenye
mitandao, tovuti na blogu. Nayasema haya siyo kwa kubuni bali ni kwa ushahidi
niliokuwa nao tena ambao nilishuhudia mwenyewe binafsi baada ya kufanya utafiti
wa kina.
Mwaka 2011 nilimaliza
kutunga kitabu changu ambacho siogopi kusema kilikuwa ni kitabu kilicholeta mapinduzi
makubwa mno katika tasnia nzima ya elimu ya pesa na mafanikio nchini
kupitia mitandao na hata kupitia sekta nyinginezo za kiuchumi. Kitabu cha “MIFEREJI YA PESA NA SIRI MATAJIRIWASIYOPENDA KUITOA” “kilikuwa ni kitabu cha
maajabu” (magic book)
kwani kila aliyebahatika kukisoma kitabu kile, alipata mwamko wa ajabu kuhusiana
na maisha na kutafuta pesa kwa ujumla.
NI ATHARI GANI MIFEREJI YA PESA ILIACHA AKILINI
MWA WALE WALIOKISOMA?
Kuchapishwa kwa kitabu
Mifereji ya Pesa kuliambatana na miradi mingine mitatu ambayo ilikuwa ni
Tovuti(website) iliyojulikana kama “KUELEKEAUTAJIRI”, blogu ambayo nayo tuliipa
jina hilohilo pamoja na kitabu kingine kikubwa tulichokibatiza jina hilohilo. Mara
tu baada ya vitu hivyo kukamilika na matangazo kuanza tulishuhudia misururu ya
simu za watu, barua-pepe pamoja na ujumbe mfupi wa maneno, wakitaka kujua zaidi
kuhusiana na kampuni yetu.
Athari zilikuwa ni za aina
mbili, chanya na hasi, kwa upande wa athari chanya, watu
wengi waliokisoma kitabu hiki walihamasika sana, vijana wengi wakaanzisha blogs
mbalimbali kwa ajili ya kujiingizia pesa, makampuni pamoja na kujitambua upya
kwamba wanapaswa kuwa na malengo fulani katika maisha ndipo waweze kufanikiwa kiuchumi,
kimasomo au katika nyanja nyingine yeyote ile.
Niligundua dhamira yetu kuu
ya kuona wafanyibiashara wadogo wengi kadiri iwezekanavyo wanapiga hatua
kuelekea mafanikio, ilikuwa ikifanikiwa na kufanya kazi baada ya kuona 'bloggers'(wanablogu) wengi wapya
wakianzisha blogu na hata wengine wakikopi makala kutoka katika tovuti na blogu yetu.
Kwa kifupi ni kwamba mtu
unapokisoma kitabu hicho kinaamsha ndani yako hamu kubwa ya kumiliki biashara
yako mwenyewe, hamu ya kuanzisha blogu au tovuti ya kutengeneza pesa, hamu ya
kutajirika kupitia mtandao wa intaneti, shauku kubwa ya kuanzisha kampuni yako
hata kama huna maelfu ya shilingi, hamu ya ku tengeneza fedha kupitia blogu au
tovuti yako, kujua mbinu mbalimbali za kutengeneza pesa ukiwa nyumbani. nk.
Kitabu cha “Mifereji ya Pesa na siri matajiri
wasiyopenda kuitoa”
|
Athari nyingine chanya
ilikuwa ni; kuongezeka kwa mwamko wa watu mbalimbali waliofanikiwa kimaisha
hususani kiuchumi, kuweka wazi siri zao mbalimbali walizopitia katika kufanikiwa.
Kama wewe ni mdadisi, hebu jaribu kufanya kautafiti hata kasikokuwa rasmi tu,
tangu mwaka 2011 kuona ni kiasi gani matajiri na watu mbalimbali waliofanikiwa
kiuchumi walivyoweka wazi njia
mbalimbali za jinsi mtu anavyoweza akaondokana na umasikini kwa kupitia njia
mbalimbali halali, kitu ambacho hapo kabla ya hiyo kampeni yetu kuanza kilikuwa
siyo kitu cha kawaida watu kuweka wazi siri zao za utajiri au siri za
mafanikio.
Mwamko mkubwa zaidi wa watu
kutaka kufahamu ni nani mtu tajiri zaidi Tanzania au watu matajiri zaidi Afrika
Mashariki, mtu tajiri kuliko wote Duniani, Tajiri mwenye umri mdogo kuliko
wote, Mwanamke tajiri kushinda wote
Afrika na Dunia kwa ujumla.nk.
Kulikuwa na athari hasi
kitabu cha mifereji ya pesa kilichoacha kwa wasomaji wetu na miongoni mwazo ni
hii ya watu kudhani ya kwamba kampuni yetu pamoja na kampeni tuliyokuwa
tukiiendesha iliyoitwa “Kuelekeautajiri” ilikuwa na malengo ya kuwasajili au
kuwavutia watu ili wajiunge na taasisi za siri zinazohusika na kuwatajirisha
watu kimiujiza, na hili lilitokana na jina letu kuwa na “ukakasi”. Hali hii ilitulazimu kufanya marekebisho makubwa “rebranding” ya majina ya vitabu pamoja
na mitandao yetu yaani blogu, ‘website’, na mitandao ya kijamii kama makala hii
ya, “hakuna utajiri wa miujiza kwenye mitandao, fanya kazi kwa bidii”,
inavyoeleza.
Tukio lililonishtua ni siku
moja, aliponipigia simu mtu mmoja aliyejitambulisha ni mkazi wa Kinondoni na yakuwa
baada ya kutusoma kwenye tovuti yetu na blogu, alikuwa na shauku ya kuonana na
sisi kwani alikuwa na mipango ya kuanzisha mradi wa kutengeneza filamu
inayohusiana na maswala ya utajiri. Mwanzoni nilitaka ‘kumpotezea’ na kumjulisha kuwa sisi tunashughulika na vitabu tu na
wala hatufadhili miradi ya aina yeyote ile, lakini alinishawishi sana nikutane
naye hata ikibidi tuingie ubia kutokana na yeye kuwa tayari anao wafadhili wa
uhakika wa kutoa fedha za mradi.
Nilimkubalia tukapanga
kukutana Rozana stendi ya mabasi
katika mkahawa mmoja jirani. Katika mazungumzo yetu nilibaini hakuwa na lolote
kuhusiana na filamu bali lengo lake lilikuwa ni kunihoji ikiwa kampuni yetu
ilikuwa na uhusiano na vyama tata vinavyohusishwa na maswala ya utajiri wa
miujiza. Niligundua japo hakupenda kunijulisha kuwa alikuwa mwandishi wa habari
kutoka chombo fulani cha habari tena kinachoheshimika na bila shaka alikuwa
amepewa “assignment” na mkuu wake wa
kazi. Akiwa amekificha kinasa sauti chake nisikione, alijaribu kuelekeza mazungumzo
yetu kwenye mada zinazohusiana na vyama hivyo akitaka ahakikishe ikiwa kweli
tulikuwa tunahusiana nao ama la.
Tuliongea kirafiki sana nikamuelezea
kwa ufasaha malengo ya kampuni yetu, na kile tulichokuwa tumekusudia
kuwaelimisha watu hususani wafanyabiashara wadogo wanaoanzisha biashara zao
pasipokuwa na elimu ya ujasiriamali ya kutosha. Kwa kweli baada ya ‘interview’ hiyo, siku ileile nilichukuauamuzi wa kwenda kubadilisha kabisa muonekano mzima wa blogu, tovuti na vitabu vyetu
ikiwa ni pamoja na kubadilisha kabisa jina lililokuwa likiwapa watu tashwishi.
Vile vile ilitubidi kufanya
kazi ya ziada kuandaa makala mbalimbali kama hii hapa zilizotoa elimu na ujumbe kuwa mitandaoya kijamii na mtandao wa Intaneti kwa ujumla haikulengwa kwa ajili ya shughuliza kuleta uharibifu kwa wanadamu au hata kuwasaidia “wajanjawajanja” wanaopenda kula pasipo hata kutoa jasho kidogo au
kutumia akili zao katika vitu vyenye mitazamo chanya na hivyo kwa mtu yeyote
eti kuanza kusaka mitandaoni njia za kimiujiza za kutajirika haikuwa sahihi
bali upotofu ulioenezwa na wajanja wachache kwa sababu zao binafsi.
Matokeo ya kubadilisha
majina ya mitandao yetu ghafla kwenye google
na “search
enginse” nyingine yalikuwa na athari mbaya sana kwa idadi ya watu
waliokuwa wakitutembelea kwani, idadi ilishuka ghafla kutoka watu 200-300 kwa
siku mpaka kufikia watu 20-50 kwa siku.
Tukajifunza somo kubwa sana kuhusiana na hii mitandao kumbe unapobadilisha vitu
kama majina, anuani(url) basi kama usipokuwa makini ukatumia kanuni
zinazotakiwa utajutia kubadilisha.
Njia za kuingiza pesa(kipato cha ziada) nje ya
kazi zako za kawaida.
Uchawi wa kitabu hiki, kama
nilivyotangulia kusema kwamba ni kitabu cha maajabu au ‘magic book’, upo katika eneo hili, namna ya kujitengenezea ukwasi
wa ziada na huku ukiendelea na ratiba zako za kawaida, iwe ni kazi, masomo au
hata biashara yako ya msingi uliyoizoea.
Mwanamke mjasiriamali akitengeneza pesa kupitia
mtandao/blogu yake.
|
Pamoja na njia nyinginezo 6 za ukweli
za kujiingizia pesa hata ukiwa umelala, au ukiwa umelazwa hospitalini pengine
kwa bahati mbaya umeugua, au ukiwa umesafiri kwenda kuwajulia hali ndugu na
jamaa zako waliokuwa mbali, kuna hii njia yenye nguvu sana ya kujitiririshia
noti kirahisi kabisa kupitia mtandao wa intaneti, tovuti au blogu yako
unayoweza kuanza biashara hata na mtaji wa shilingi elfu kumi 10,000/= pekee.
0 Response to "NJIA ZA KUINGIZA KIPATO CHA ZIADA NJE YA KAZI YAKO"
Post a Comment