Mnamo mwaka 1915, Einstain katika Kanuni yake maarufu
ijulikanayo kama “General Relativity” inayoelezea uhusiano wa vitu vyote
vilivyokuwepo ndani ya Ulimwengu, aligundua pia kuwepo kwa nguvu fulani
ya mawimbi, ‘gravitational waves’ ambayo huweza kuzalishwa na kitu
chochote kile kilichokuwa kwenye mwendo wa kasi
tukiwamo na hata sisi binadamu, nyota, jua, na maumbo mengine yote
yaliyokuwepo angani.
Nguvu hizi huwa kubwa kadiri kitu kinachohusika
kinavyokuwa kikubwa zaidi na kwa kasi kubwa. Mawimbi hayo husambaa mithili ya
mawimbi yanayotokea unapotupa jiwe katika maji. Lakini jambo la ajabu pamoja na
Einstain kutabiri mawimbi hayo yasiyoonekana kiurahisi miaka 100 iliyopita,
hakuna mtu yeyote aliyeweza kuthibitisha
uwepo wake wala ni kwa nini nguvu hizo zipo.
Wanasayansi mbalimbali katika vipindi tofauti walijaribu
kuunda vyombo vya kuyanasa mawimbi hayo
lakini haikuwezekana mpaka hivi leo ambapo kwa mara ya kwanza kabisa
jaribio lililopewa jina la “Advanced Laser Interferometer Gravitational Wave
Observation(VIGO)” limeweza kuyanasa na kuyapima mawimbi hayo na mpaka sasa
ninapoandika, Wanasayansi hao wanaendelea na kazi ya kuchanganua ‘data’.
Mwanasayansi
katika uchunguzi huo.
|
Majaribio hayo yamefanyika katika maeneo tofauti Duniani
yakiwamo Marekani, Italia na Ujerumani na katika kila moja watalinganisha
matokeo yake kuona ikiwa taarifa(data) zinafanana na hivyo kuthibitisha kwa
uhakika kabisa pasipo shaka kuwa alichotabiri mwanasayansi Albert Einstai katika
kanuni yake mashuhuri “General Relativity” miaka 100 iliyopita kilikuwa sahihi
kwa asilimia 100%.
Mawimbi hayo"gravitational waves".
|
Kufanikiwa kuthibitisha uwepo wa mawimbi hayo kuna
umuhimu mkubwa katika uchunguzi wa anga za juu pamoja na kufahamu namna
Ulimwengu ulivyotokea, kitendawili ambacho kimekuwa kigumu kuteguliwa na
wanasayansi kwa muda mrefu sasa.
Ugunduzi huu pia utasaidia katika uchunguzi wa
maeneo mengine ya ulimwengu katika anga za mbali kabisa ambazo vyombo vya
kawaida “telescope” haviwezi kuona na pengine kugundua mifumo mingine ya Sayari inayofanana na huu wa jua letu ambao labda kuna sayari zilizokuwa na uhai kama
ilivyokuwa Dunia yetu. Kwani mpaka sasa hivi katika mfumo wetu huu wa sayari
hakuna mahali popote palipogundulika kuishi viumbe hai.
0 Response to "MAWIMBI YASIYOONE ALIYOTABIRI MWANASAYANSI ALBERT EINSTAIN YANASWA, NI BAADA YA MIAKA 100"
Post a Comment