Duniani kote na hata hapa Tanzania kumejaa
hadidhi na masimulizi mengi kuhusiana na utajiri na mafanikio hasa hasa suala
la jinsi mtu anavyoweza akapata utajiri haraka kwa njia nyepesi zisizochosha
wala kuchukua miaka mingi. Wapo wanaoamini kwamba njia hizo za kutengeneza
utajiri na mafanikio haraka zipo na vile vile wapo watu wanaoamini utajiri wa haraka
haupo labda uupate kupitia bahati na sibu au kutoka kwa ndugu yako wa karibu
aliyekurithisha baada ya kufariki dunia.
Kiukweli mtu yeyote anaweza akawa tajiri kwa
njia halali ingawa siyo kwa haraka na rahisi kama watu wengi wavyowaza,
vinginevyo basi iwe tu ni kwa njia zilizotajwa hapo juu za bahati na sibu,
urithi, au kwa njia haramu kama vile za wizi na ufisadi. Kuna watu wengine
hufikia hata hatua za kufanya vitendo vya ajabu na vya kikatili kabisa wakisaka
utajiri wa haraka ambao mwishowe huwa hawaupati au huishia jela na kupata laana
na majuto maisha yao yote badala ya maisha mazuri na mafanikio waliyokuwa wakiyatamani.
Vitendo kama kuua watu kutokana na imani za
kishirikina, ubakaji na hata kuamini vitu vya ajabuajabu kunakohamasishwa na
waganga uchwara wa kienyeji au watu wa imani za baadhi ya madhehebu na imani
zisizokuwa na msingi wowote ule ndivyo kwa kiasi kikubwa vinavyowapotosha watu
kuamini kwamba kuna njia za haraka za kupata utajiri na mafanikio kipesa.
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote kutajirika.
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote kutajirika.
Vile vile wapo watu ambao wao kwa kutaka
kupata utajiri wa haraka pasipo kutoa jasho, huwapotosha watu wengine kupitia
vyombo mbalimbali vya habari na hususani intaneti kwa kuwahadaa kuwa wanazo
mbinu au njia za kuwatajirisha upesi, hivyo sharti lao kubwa huwa ni kulipia
mafunzo, vitabu, DVD au semina. Sisemi
hamna vitu vya namna hiyo vya ukweli hapana, ila nasema katika wote wanaojinadi
hivyo pia na wajanja wamo humohumo, ni kama ilivyo kwa kundi la mamba, kenge
nao hawakosekani.
Kwenye hii mitandao wapo watu wengi wanaotoa
mafunzo ya ukweli na yenye tija na hata ikiwa mtu unatoa pesa yako baada ya
kupata huduma au bidhaa kama ni kitabu, dvd au semina, unatamka; “Kweli pesa
yangu haijakwenda bure, imetoka kihalali”. Hali kadhalika wapo watoa mafunzo
ambao lengo lao ni kupata pesa ‘kupitia mgongo wa kukutajirisha wewe’ Hivyo,
chukua tahadhari na uwe makini vya kutosha!
Sasa basi baada ya maelezo hayo mafupi, hebu
twende moja kwa moja tukazione hizo njia 7 halali kabisa na za uhakika
unazoweza ukazitumia kutajirika.
1.
Fungua biashara.
Kufungua biashara isijekuwa ni kufungua biashara
tu hivihivi kulikozoeleka kila siku, ni lazima hapa uwe “mjasiriamali” kidogo,
nikimaanisha uweke ubunifu na jitihada za kutosha. Katika ubunifu na jitihada
hizo, hakikisha mambo yafuatayo unayazingatia kikamilifu;
· Hakikisha
unafanya kile kitu unachokipenda, biashara ikusisimue kuifanya na siyo uifanye
basi tu ilimradi kwa kuwa inabidi uifanye.
· Weka Mipango:
Usidanganyike kuwa eti, kufanya mpango au mchanganuo wa biashara ni kupoteza
muda bure. Hakuna jambo lolote duniani hufanywa pasipo kuwepo mpango, tazama
harusi(vikao kila wiki), ujenzi wa majengo(ramani kwanza kabla ya jengo
lenyewe), uendeshaji wa serikali(kila mwaka wabunge hukaa Dodoma kupanga) na
hata pale nyumbani kwako kila siku mnapoamka asubuhi, baba na mama hukaa na kupanga
siku hiyo itaendaje huku mama akiorodhesha kwenye karatasi vitu anavyopanga
kwenda kununua sokoni mchana. Huo ndio mpango wenyewe! Na biashara ni
hivyohivyo.
Tatizo watu wengi tunakuwa wavivu, huwa tunapanga vichwani basi na
kuishia hapohapo. Unapoandika katika karatasi hata kama ikiwa ni kurasa1 au 2,
ni bora zaidi kuliko kuuacha mpango wako kichwani, wewe ni binadamu unaweza
ukasahau badhi ya vitu vya msingi mbele ya safari.
· Juhudi
zako zote ni lazima zilenge kwenye mahitaji ya wateja wako.
· Jitangaze
wewe na biashara yako, usione aibu kuwaambia wateja; “Jamani siku hizi natengeneza sabuni laini nzuri za unga, maji na za
miche, njooni mnunue” au “Nimeanzisha
darasa la tuisheni la chekechea pale nyumbani, waleteni wanenu jioni”
· Ichukulie
biashara yako kwa umakini na weledi wa hali ya juu na siyo kuidharau,
ukiidharau na wateja watafanya hivyohivyo.
· Wape
wateja huduma za kipekee, kila mmoja
ajisikie unamjali tofauti na mwingine.
· Tumia
fursa ya teknolojia za kisasa kama
mitandao ya kijamii kujitangaza na biashara yako zaidi kwa wateja.
· La mwisho
lakini lenye umuhimu pengine kushinda mengine yote niliyoyataja hapa ni; “USISAHAU KUWA NA NIDHAMU YA PESA”.
Pesa itoke tu pale penye ulazima. Acha wakuite, “wewe ni bahili”, “Hutoi
shilingi yako”, “Sijui wewe ni ‘mchagga’ pesa ikidondoka ukiwa ‘theater’ mahututi
unazinduka” lakini wewe kaza uzi tu, ipo siku utakuja kuwapa msaada mkubwa hata
zaidi ya huo wanaoutaka sasa kutoka kwako.
2.
Wekeza katika biashara ya majengo na ardhi(Real Estate)
Niliwahi kuandika kuhusiana na biashara hii
kwenye kitabu nilichoandika cha, “MIFEREJI
7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA”, nikaelezea vizuri sana
jinsi biashara hii ilivyokuwa na uwezo wa ajabu wa kumtajirisha mtu katika
kipindi kifupi. Kwa mfano, badala ya kukopa fedha benki au kokote kule na
kuanza kuumiza kichwa jinsi ya kupata pesa(faida) au utazizalishazalisha vipi,
unaweza ukaziingiza pesa hizo kwenye biashara hii na ukapunguza kwa kiasi
kikubwa hatari na “stress” zitokanazo na biashara za kawaida.
SOMA: Usilaumu tena mikopo ya benki na taasisi za fedha.
SOMA: Usilaumu tena mikopo ya benki na taasisi za fedha.
Tuseme pengine mkononi unazo shilingi milioni
zako mbili 2, (huu ni mfano lakini) Unakwenda benki unakopa shilingi milioni
saba 7, jumla zinakuwa milioni 9. Unanunua kiwanja nje kidogo ya mji na kisha
baada ya miaka labda tuseme miwili au hata mwaka huo huo ulionunua unamtafuta
mtu mwingine anayekihitaji unamuuzia kwa shilingi milioni 12. Hapo tayari
utakuwa umeweka kibindoni milioni tatu 3 za chapchap pasipo hata kuumiza kichwa
chako wala kugombana na wateja.
Shughuli hiyo unaweza hata ukaifanya kuwa
ndiyo kazi yako ya kudumu huku pengine ‘wife’ kama unaye akiendelea kuuza genge
lenu au biashara nyingine yeyote ndogondogo mliyonayo kwa ajili ya kuingiza
senti kidogo za kununulia vitafunio asubuhi.
Au njia nyingine unaweza ukafanya hivi; Ikiwa
unamiliki nyumba yenye vyumba vya kutosha, pangisha wapangaji na hata ikibidi
kama nyumba ipo eneo zuri la bashara, hama wewe na familia yako mkapange nyumba
eneo nafuu huko nje kidogo ya mji. Wapangaji watawaingizia kipato cha uhakika.
Kumbuka kipato cha namna hii wewe mwenyewe hauhitaji uwe pale muda wote
ukisimamia ndipo kipato kiingie hapana, siyo kama ilivyokuwa kwa ajira na
biashara nyingine za kawaida.
6.
Fungua biashara kwenye mtandao wa Intaneti
Kuna njia nyingi unazoweza ukazitumia
kuingiza pesa mtandaoni, nimezizungumzia na kuziainisha pia katika kitabu changu
hicho cha; ‘Mifereji 7 ya Pesa’.
Mfano mmoja, unaweza ukatengeneza video na ukairusha You tube. Kila
wanapoitazama watu 1000, unalipwa dola $2.
SOMA: Hatua 7 za kuanzisha biahsra yako ndogo ukiwa kwenye ajira.
SOMA: Hatua 7 za kuanzisha biahsra yako ndogo ukiwa kwenye ajira.
Sasa tuseme video yako ni ya kipekee kiasi
kwamba baada ya kuiweka tu pale, video imesambaa haraka kama moto wa nyika, kwa
maana nyingine huita; “Viral video”.
Unaweza ukatengeneza mamilioni kwa muda mfupi sana mtandaoni achilia mbali njia
nyinginezo kama vile, matangazo ya ‘google(Adsense)’, kuuza bidhaa na huduma
mbalimbali kwenye mtandao nk.
7. Tunga
kitabu, muziki au filamu.(Kutumia mawazo yako mwenyewe kuanzisha mradi wa
kiuchumi)
Kama ni hadithi, basi hadithi yako uitunge
kwa namna ambayo utamfanya msomaji abakie na shauku/hamu kubwa muda wote ya
kutaka kufahamu tukio linalofuata litakuwaje. Muziki nao ni hivyo hivyo,
muangalie kwa mfano mwanamuziki nguli Diamond Platnumz(Naseeb Abdul), tangu
atoe kibao cha ‘Mbagala’, watu kila kukicha hasahasa wale mashabiki zake
wanakuwa na shauku ya kutaka kujua Diamond kibao kitakachofuata kitakuwa vipi.
Na kwa mtindo kama huo mtu unaweza ukatajirika hata chini ya miaka mitatu 3
Wakati natunga kitabu; Mifereji 7 ya pesa,
ndani ya akili yangu njia hii kati ya zote nilizoorodhesha hapa ya kuanzisha mradi wa kiuchumi ukitumia mawazo
yako mwenyewe, ndiyo njia iliyokuwa imetawala zaidi akilini mwangu hata
kikawa ndicho kipengele nilichoanza nacho Sura ya Kwanza ya kitabu.
HITIMISHO.
Kutajirika kunahitaji mtu ujitume na siyo
kazi ya siku moja. Ukikutana na mtu yeyote yule anayekuahidi atakupatia njia rahisi zitakazo kuwezesha
kupata utajiri haraka kwa siku moja, mwezi au hata miezi kadhaa tu, mtu huyo
mtilie mashaka. Huenda wewe ukawa ndiye unayekwenda kumtajirisha yeye. Badala
ya kuhangaika usiku na mchana ukisaka njia nyepesi za kupata utajiri, muda huo
utumie kikamilifu kujiongezea maarifa zaidi ya biashara(kunoa ubongo wako) na huku
ukiendelea kufanya kazi au biashara yako kwa nguvu zako zote na maarifa,
utajiri utaupata tu.
Ndugu msomaji wa makala hii, ukipenda kuwasiliana na nasi kwa ajili ya jambo lolote lile, iwe ni ushauri juu ya biashara, au ungehitaji vitabu vyetu, basi namba za simu ni hizi hapa chini;
Simu: 07122 202244 au 0765 553030 au 0689303098
E-mail: jifunzeujasiriamali@gmail.com
Telegram: @petertarimo
Usisahau pia kudownload hapa kile kitabu cha kanuni ya kujifunza elimu ya pesa na mafanikio kwani muda wake wa kutolewa bure karibu utamalizika na kitakuwa kikiuzwa kwa Sh. 5,000/=. Vitabu vingine vilivyopo katika duka letu la mtandaoni, SMARTBOOKSTZ navyo vyote sasa unaweza kuvipata kupitia simu yako ya Smartphone au kompyuta ya kawaida kupitia e-mail na telegramu.
Ndugu msomaji wa makala hii, ukipenda kuwasiliana na nasi kwa ajili ya jambo lolote lile, iwe ni ushauri juu ya biashara, au ungehitaji vitabu vyetu, basi namba za simu ni hizi hapa chini;
Simu: 07122 202244 au 0765 553030 au 0689303098
E-mail: jifunzeujasiriamali@gmail.com
Telegram: @petertarimo
Usisahau pia kudownload hapa kile kitabu cha kanuni ya kujifunza elimu ya pesa na mafanikio kwani muda wake wa kutolewa bure karibu utamalizika na kitakuwa kikiuzwa kwa Sh. 5,000/=. Vitabu vingine vilivyopo katika duka letu la mtandaoni, SMARTBOOKSTZ navyo vyote sasa unaweza kuvipata kupitia simu yako ya Smartphone au kompyuta ya kawaida kupitia e-mail na telegramu.
Naam Nimefurai kupata maelezo yenu ya njia bora za kibiashara itakayo wezesha mtu kujikimu kimaisha nakuweza kutoka katika hali flani ya maisha na kwa nyingine na huu ndo uhalisi wa mambo, ila swali langu ni,..wasiokua ata na uwezo wa pesa taslim zakujifungulia biashara awa nao watatumia njia gani ?
ReplyDeleteAsante sana Mr. Abu Muhammad kwa kusoma hapa, ni kweli kabisa shida kubwa inayowakabili watu wengi wanaotaka kujikwamua katika hali ngumu ya maisha ni ukosefu wa kianzio kwa maana ya mtaji hasa wa pesa.
DeleteKiuhalisia hakuna biashara isiyohitaji mtaji japo kinadharia husemekana kwamba unaweza kuanza na mawazo yako tu. Ndiyo kuna walio na bahati ya kuanza na mawazo kisha wakapata sapport mahali pengine na wakainuka lakini kwa waliokuwa wengi utakubaliana nami kwamba wanazeeka na mawazo yao kichwani.
Lakini hata hivyo suluhisho lake lipo japo siyo njia ya mkato, kwa mfano huna pesa kabisa lakini una nguvu zako na afya uliyojaliwa na Mungu basi tafuta angalao kibarua au kazi ya ajira, utafanya kwa muda fulani huku ukijiwekea akiba kwa ajili ya kupata kianzio cha biashara unayoipenda au ikiwa una mali(asset) yeyote ile hata kwa mfano simu yako ya mkononi unaweza ukaiweka rehani mahali au kuiuza pesa zile ukaanzishia mradi wa biashara ndogo.
Katika hatua za awali tukubaliane utapata hali ngumu sana lakini ukiwa na malengo na uvumilivu itafika tu mahali utakuwa na mtaji wa kutosha na hatimaye sasa utaweza kujitanua zaidi kwa kwenda taasisi za fedha wakuongezee mtaji wako.
ninafurahishwa sana na makala haya ya ujasiriamali yananitia nguvu na mwamko
ReplyDeleteAsante sana Frank
Deletemakala haya yananipa kiburi cha kukomaa ktk ujasilamali
ReplyDeleteVizuri Veronica umesema kweli kwani ujasiriamali unahitaji mtu kuwa king'ang'anizi mpaka unafikia malengo yako. Waliofanikiwa wote wamefanya hivyo na wala hakuna njia ya mkato.
DeleteThanks never give up
ReplyDelete