Ufuatao ni muhtasari wa mpango wa biashara ya ufugaji wa
kuku wa mayai, mchanganuo mzima wa mradi huu unapatikana katika blogu maalumu
ya Darasa la michanganuo ya biashara" lililoanzishawa rasmi kwa ajili ya wale
wote wenye nia ya kujua jinsi ya kuandika michanganuo kwa ufasaha. Ili kuweza
kuingia katika blogu hiyo na kuwa mwanadarasa wa darasa hilo unatatakiwa kuwa
na kiingilio/tiketi au ada. Tikiti hiyo ni kununua tu kitabu cha Michanganuo ya
Biashara na Ujasiriamali ambacho bei yake ni shilingi elfu 10.
Ndani ya Darasa utapata fursa nyingi zikiwemo, kuuliza
kitu chochote ulichoshindwa kukielewa katika kitabu cha michanganuo ya biashara
na ujasiriamali, kutoa michango mbalimbali ya mawazo na hata ushauri kwa
wanadarasa wengine, kushirikishana na wadau wengine katika kutafuta njia za
kupata mafanikio zaidi kimaisha na kiuchumi kwa ujumla. Darasa hili ni kwa
upande mwingine ni kama “MASTERMIND GROUP”, kikundi cha kupeana ushauri wa ni
vipi mnaweza kusogea zaidi ya pale mlipo.
………………………………………………………...................
MCHANGANUO WA BIASHARA
MRADI WA MAYAI BORA PROJECT
(KUKU 1000)
P.0.
BOX 01010
KIMARA
SUKA
DAR
ES SALAAM
TANZANIA
Simu:
255765 553030
Email:
info@mayaibora.co.tz
2/11/2016
Umeandaliwa na Barikiel Sanga
Simu: +255712 202244
MUHTASARI
TENDAJI.
Waanzilishi wa mradi wa Mayai Bora Project(MBP),
Bwana Barikiel Sanga na Mkewe Bibi Marieth Mdegella wana dhamira ya kuzalisha
mayai bora na makubwa kwa ajili ya kuboresha afya za watu lakini wakati huohuo
wakijiingizia faida itakayowasaidia katika maisha yao baada ya kustaafu
utumishi wa Umma.
Malengo ya mradi huu ni kuzalisha trei
zipatazo 27 kwa siku ifikapo wiki ya 18 kutoka mradi unaanza na kuendelea hadi
kuku watakapofikisha wiki 90, Kutoa ajira ya kudumu kwa watu wawili, pamoja na
wamiliki kujihakikishia kipato endelevu pindi watakapostaafu miaka mine kutoka
sasa.
Mradi utaanza rasmi hapo Januari 2017 kwenye
eneo linalomilikiwa na waanzilishi wa mradi lililopo Kimara Suka jijini Dar es
salaam kandokando kabisa ya Barabara iendayo Morogoro.
Moja ya siri za mafanikio ya mradi huu
itakuwa ni kuhakikisha chakula bora na cha kutosha, maji safi, vitamini, madini
na chanjo kwa kuku katika muda wote mradi utakapokuwa ukiendelea. Upunguzaji
gharama kwa njia za kiteknolojia kama vile, kukuza majani mabichi ya
kuku(hydroponic fodders) na uthibiti wa hali ya juu kabisa wa magojwa
kibaiolojia(Biosecurity measures) ni vitu pia vitakavyopewa kipaumbele cha
kwanza.
Mahitaji yote ya mradi ili uweze kuanza
vizuri yamekadiriwa kuwa ni shilingi za Kitanzania milioni 25, fedha hizi ndizo
zitakazotumika kujenga banda, chumba cha kulala mfanyakazi, ofisi/duka la mradi
pamoja na gharama nyingine zote zitakazohitajika tangu mradi unaanza siku ya 1
mpaka wiki ya 18 kuku watakapoanza kutaga mayai.
Gharama za uendeshaji mradi zinazojirudia
kama vile, chakula cha kulishia kuku, maji na mishaha ya wafanyakazi peke yake
ni wastani wa shilingi milioni 89 katika kipindi chote cha wiki 90(miezi 2 na
nusu)
Bidhaa zitakazouzwa na kampuni ni, chakula
cha kuku, mayai, kuku pindi muda wao wa kutaga utakapokuwa umefikia ukomo,
mbolea na mifuko mitupu iliyokwisha chakula cha kuku.
Soko la mayai wameligawa katika makundi 2,
wauzaji wa jumla wa mayai na wateja wa kawaida lakini soko watakalolipa
kipaumbele zaidi ni hili la wauzaji mayai kwa jumla kutokana na ukubwa na
uhakika wake. Uhitaji wa mayai Tanzania na hususani jiji la Dar bado ni mkubwa
sana kama takwimu za hivi karibuni zinavyoonyesha kwamba, kwa wastani Mtanzania
hula chini ya mayai 100 kwa mwaka ili-hali angepaswa ale mayai zaidi ya 250 kwa
mwaka.
MBP wamezungukwa na washindani wakubwa 3
lakini siyo tishio kwake sana kwani washindani hao wote wanayalenga masoko
tofauti kabisa na la kwao.
Sifa za kipekee za Mayai Bora Project ni
kuzalisha mayai bora na makubwa, bei nzuri kwa wateja ukilinganisha na bei ya
soko pamoja na eneo zuri linalofikika na kuonekana kwa urahisi na wateja.
Ili kuhakikisha mradi unafanikiwa watatumia
mbinu mbalimbali za kimasoko zisizokuwa za gharama sana lakini zenye tija kubwa
kama vile, kuweka bango, kugawa vipeperushi, mitandao ya kijamii na huduma
nzuri kwa wateja ambao watatoa taarifa kwa watu wengine chini ya kaulimbiu yao,
“Kuku ni Utajiri”. Vile vile watatunza taarifa muhimu za wateja wao(customer
database).
Mauzo yahusianayo na kuku na mayai pekeyake
yanakisiwa kufikia milioni 99 na yale yahusianayo na uuzaji wa vyakula vya kuku
ni milioni 92 kwa msimu wote mmoja.
Viongozi wakuu wa mradi watakuwa ni Barikiel
na mkewe Marieth ambapo watawaajiri wafanyakazi 2. Wote wawili Barikiel na
mkewe wana elimu ya biashara kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika.
Mpaka kufikia wiki ya 90 ya mradi, faida
halisi ya mradi kwa ujumla inakadiriwa itakuwa shilingi milioni 21 na faida ya
mayai peke yake katika kipindi cha utagaji ni wastani wa shilingi milioni 12.
Baada ya awamu hii wanatarajia kuanza tena msimu mwingine wa pili kwa idadi
hiyohiyo ya kuku 1,000.
Faida
na hasara kwa ufupi ya mayai kwa wiki 72 za utagaji.
Unaweza kuusoma mchanganuo huu wa ufugaji kuku wa mayai
wote kuanzia mwazo hadi mwisho pamoja na michanganuo mingine na mawazo ya
biashara zaidi ya 50 ya biashara unazoweza kuanzisha hapa Tanzania kwa kununua
kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali, ambapo pia unapata fursa ya
kuwa mwanachama wa kudumu wa blogu ya MICHANGANUOYA BIASHARA yenye Darasa maalumu ambamo Mipango ya biashara hufundishwa kwa
kina.
Unapomaliza darasa hili hakuna tena kitu
kitakachokutatiza kinachohusiana na Mpango wa Biashara na Unakuwa umepata uwezo
mkubwa wa kuanzisha na kusimamia biashara yeyote ile kwa ufanisi wa hali ya
juu.
Kujiunga na Shule hiyo ya Michanganuo, unatakiwa kwanza,
kutuma anuani yako ya E-mail(ni lazima iwe ya GMAIL) mfano, wewe@gmail.com. Kitu cha pili muhimu, lipia
kitabu cha “MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI”
chenye kurasa 410 kwa shilingi 10,000/=.
Nami nitakutumia kitabu hicho kupitia hiyo email mara moja na Tayari sasa utakuwa umekwisha kuwa mwanachama rasmi wa darasa hili la aina yake kuwahi kuanzishwa hapa Tanzania. Hakuna gharama za ziada utajifunza kwa miezi 3-6 Ordinary Level halafu tena miezi mingine 3 Advanced Level ambapo utakuwa umewiva kwelikweli.
Ukitaka kulipia kitabu, tumia Tigo pesa au Mpesa na namba ni hizi hapa, 0712 202244 au 0765 553030 jina litatokea, Peter Augustino Tarimo.
Nami nitakutumia kitabu hicho kupitia hiyo email mara moja na Tayari sasa utakuwa umekwisha kuwa mwanachama rasmi wa darasa hili la aina yake kuwahi kuanzishwa hapa Tanzania. Hakuna gharama za ziada utajifunza kwa miezi 3-6 Ordinary Level halafu tena miezi mingine 3 Advanced Level ambapo utakuwa umewiva kwelikweli.
Ukitaka kulipia kitabu, tumia Tigo pesa au Mpesa na namba ni hizi hapa, 0712 202244 au 0765 553030 jina litatokea, Peter Augustino Tarimo.
0 Response to "UFUGAJI BORA WA KUKU WA MAYAI: MCHANGANUO WA BIASHARA, KUKU 1000"
Post a Comment