Ili uweze kufanikiwa maishani ni lazima ujiwekee malengo, na hiyo ni kanuni ya msingi ya kimaumbile ambayo huwezi ukaipinga hata utoe sababu kubwa kiasi gani. Malengo husaidia kuongeza umakini na kuelekeza nguvu katika jukumu husika huku yakimfanya mtu kuwa mbali na mambo yote yanayochangia kutokutimia kwa jukumu hilo barabara.
Kuna wataalamu kama ‘Edwin A. Locke’ aliyewahi
kufanya utafiti kuhusiana na jinsi binadamu anavyoweza akatimiza majukumu yake
vizuri na kwa ufanisi zaidi pindi anapojiwekea malengo kuliko vile anavyoamua
kujifanyia mambo kiholela tu kama wanyama wafanyavyo. Edwin aliyeanza utafiti
huo miaka ya 60 na kuuhitimisha baada ya miaka 30 alitumia falsafa ya zamani
zaidi ya mwanafalsafa mwingine maarufu aitwaye Aristotle kwamba “Lengo
lina uwezo wa kusababisha kitendo”
na hivyo akaanza kutafiti athari za malengo katika shughuli za kila siku za
mwanadamu.
Mwisho ilibainika kwamba kuweka malengo
kunasababisha athari zifuatazo,
1. kufanya
uchaguzi wa kipi cha kufanya kwanza au kujiwekea vipaumbele.
2. Kuzidisha
juhudi zaidi kwa kile kinachofanyika mfano ikiwa mtu amezoea kulima eka moja
kwa siku, atakapojiwekea lengo la kumaliza eka 2 basi atafanya kila
linalowezekana kumaliza hizo heka 2.
3. Uvumilivu:
Mtu akishajiwekea malengo, atahakikisha anatimiza alichoahidi licha ya vikwazo
vitakavyojitokeza njiani.
4. Utambuzi:
Malengo humfanya mtu kujitambua na hata kubadilisha tabia kutoka tabia
alizokuwa nazo zamani na kuwa na tabia mpya zinazoendana au kusaidia kutimiza
malengoa aliyojiwekea.
Binadamu wa rangi zote kutoka mabara yote yanayounda
Dunia imedhibitika kwa dhati kabisa kwamba ufanisi wa kile wanachokifanya iwe
ni kazi, michezo au hata jambo lolote lile linalohusisha akili basi hutegemea
zaidi kujitoa katika kufanikisha lengo husika.
Na kwa kupitia uelewa huo wa kujiwekea malengo, taasisi
zote duniani zikiwemo serikali mbalimbali, makampuni na mashirika hutumia njia
ya kujiwekea malengo katika kufanikisha shughuli zao kwa ufanisi.
Hata tunaporudi kwenye biashara zetu, mameneja na
wajasiriamali wote hawawezi kukwepa suala la kuweka malengo ya kiuchumi katika
biashara zao. Utakuwa unafanya kitu cha namna gani ikiwa utajidanganya eti
unaendesha mambo pasipokuweka malengo akilini?. Matumizi mazuri ya muda na kujiwekea
malengo ni kama mapacha wawili vile, vitu hivyo viwili huwezi ukavitenganisha.
Hata hivyo kuna wakati malengo huwa yanakumbwa na vikwazo(changamoto)
kwa mfano, kuingiliana kwa malengo baina ya mtu mmoja na taasisi kama vile
malengo ya meneja yaanaweza yakakinzana nay ale yaliyowekwa na taasisi tuseme
labda kampuni lakini kinachotakiwa kufanywa ni kuhakikisha malengo ya mtu
binafsi yanaendana na yale ya mtu mmojammoja kwenye taasisi.
Kikwazo kingine katika kutimiza malengo ni pale unapokuta
lengo linahitaji mtu kujifunza maarifa mapya, mtu anapokuwa amejiwekea lengo la
kufanikisha jambo fulani anaweza kujisahau au kutokuona umuhimu wa kujiongezea
maarifa au taarifa mpya kuhusiana jambo
hilo. Suluhisho lake ni kwa mtu huyo kujiwekea lengo jingine la kujifunza katika
tasnia husika ili kutimiza lengo la msingi alilojiwekea.
Kuna watu wanaoweza wakakudanganya kuwa eti unaweza
ukafanikiwa bila ya kujiwekea malengo lakini ukweli ni kwamba wao wanajaribu
kutazama zaidi yale mapungufu yanayoweza kutokana na mtu kujiwekea malengo. Changamoto
kubwa kwenye kuweka malengo watu hao hudai kuwa wakati mwingine huwa hayawezi
kutimia kama unavyoyapanga, lakini ukweli ni kuwa kuweka malengo hakuna mbadala
zaidi ya mtu kuchunguza mahali ulipokosea katika malengo yako yaliyoshindwa
ukajipanga upya na kuweka malengo mengine sahihi zaidi(soma sifa za malengo
mazuri ndani ya kitabu, MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA
KUITOA).
Changamoto nyingine hutokea pale malengo unayotekeleza
unapokuwa umewekewa na mtu mwingine. Inatakiwa hata kama malengo yamewekwa
labda na taasisi au mtu mwingine basi mhusika uridhie kwa moyo wako na kukubali
kuyatekeleza huku ukifahamu fika faida utakazopata baada ya kutekeleza malengo
yenyewe.
Katika kitabu, MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIYOPENDA KUITOA, mada hii ya kujiwekea malengo hasa ya kiuchumi imeelezewa
kwa undani kabisa, kwanza malengo ni kitu gani, mifano ya malengo, tofaui ya
malengo na vitu vingine kama Dira, Maono, Ndoto na Dhamira. Pia kimeelezea kwa
ufasaha kabisa jinsi au namna mtu/taasisi anavyoweza akajiwekea malengo nk.
Kitabu hiki ni kizuri sana hasa kwa mtu anayetaka kuuanza
mwaka huu wa 2017 akiwa na mtazamo mpya kifikra na kiuchumi. Kama unafanya
biashara, umeajiriwa au upo katika harakati za kuingia katika biashara au ajira
basi kisome kitabu hiki utapata manufaa makubwa.
Kwa yule pia anayefuatilia kwa karibu kampeni yetu msimu
huu ya KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO ULIOPOTEZA(MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) sina
shaka yeyote kwamba umeshapata kitabu hiki kwani ni muhimu mno katika kukufanya
tuweze kuwa sambamba katika kampeni hii.
Unaweza kukipata kitabu hiki kikiwa katika mfumo wa
kitabu cha kawaida cha karatasi au mfumo pepe(softcopy) katika email yako.
Bei ya kitabu cha karatasi ni Sh. 4,000/= na Softcopy ni
Sh. 3,000/=. Kwa mawasiliano piga au tuma sms kupitia namba hizi hapa,
0712202244 au 0765553030. Kama unahitaji softcopy usisahau
kutuma email yako na pesa shilingi elfu tatu kupitia moja ya namba hizo popote
pale ulipo tunakutumia baada ya muda mfupi. Kwa maelezo zaidi na taarifa za
vitabu vingine unaweza ukatembelea ukurasa huu hapa, SMART BOOKS TANZANIA.
Usikubali mwaka huu mpya wa 2017 kuendelea kubaki nyuma,
amka usingizini na ujirudishie tena mambo yako yote mazuri uliyokuwa nayo
zamani. Inawezekana na wengi wameweza. Jiwekee malengo yako mwenyewe achana na malengo ya kuwekewa, hata wahenga hawakukosea waliposema "akili ya mwenzio changanya na ya kwako"
Mwandishi na Mhamasishaji wako,
Peter A. Tarimo
0 Response to "TAYARI MALENGO YAKO KIUCHUMI YA MWAKA 2017 UMESHAYAANDIKA MAHALI?"
Post a Comment