Ni misemo iliyozoeleka
katika maisha ya kila siku mitaani, utawasikia watu wakisema; “biashara
ya duka bwana, kichaa kabisa hailipi”, “duka unalinda mtaji wako tu usipotee
lakini hamna unachopata”, “duka ukila hapo hata pipi umekula faida yenyewe”,
“duka labda ukae wewe na mkeo, wengine watalifilisi mara moja”.
Kauli za
kukatisha tamaa kuhusiana na biashara hii hasa yale maduka ya rejareja ni nyingi mno kiasi kwamba ukizifuata unaweza
uione biashara hii haifai kabisa kufanya.
Lakini cha kustaajabisha ni pale utakapokuta katika mitaa
yetu kila kukicha maduka yanafunguliwa, kweli kama zilivyokuwa biashara nyingine
zote duniani, siyo maduka yote yanayofunguliwa hufanikiwa hata kudumu miezi
yake sita ya mwazo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa kuna walioanzisha maduka
tena ya rejareja tu wakatajirika na kufikia hatua za juu kabisa kama kumiliki
nyumba nzuri, magari na hata kufungua biashara nyingine kubwa zaidi.
Kiukweli hakuna biashara yeyote ile isiyokuwa na faida,
bali faida au mafanikio ya biashara yeyote ile yanatokana na jinsi biashara
yenyewe itakavyoendeshwa pamoja na mazingira ya biashara hiyo. Mbali na uzushi wote
huo katika mitaa yetu kila kukicha utashuhudia maduka yakimea kama uyoga, mbona
hawayafungi kama hayana faida?.
Wakati wewe ukidanganywa kuwa duka ni biashara kichaa, wapo wenzako wanaosomeshea watoto wao shule za ‘international’ na wakati huo huo wakiwa na uwezo wa kubadilisha mboga majumbani mwao watakavyo. Kitu kingine cha kutia matumaini zaidi ni kwamba duka ni rahisi mno kuanzisha na halihitaji mtaji mkubwa sana wa kuanzia ilimradi tu una vifaa muhimu na chumba kilichokuwa eneo watu wanakopita.
Wakati wewe ukidanganywa kuwa duka ni biashara kichaa, wapo wenzako wanaosomeshea watoto wao shule za ‘international’ na wakati huo huo wakiwa na uwezo wa kubadilisha mboga majumbani mwao watakavyo. Kitu kingine cha kutia matumaini zaidi ni kwamba duka ni rahisi mno kuanzisha na halihitaji mtaji mkubwa sana wa kuanzia ilimradi tu una vifaa muhimu na chumba kilichokuwa eneo watu wanakopita.
Asilimia kubwa ya watu kwa mfano katika miji mikubwa kama
Dar es salaam, Mwanza na Arusha wanapowaza akilini mwao juu ya biashara ya kufanya,
wazo la kwanza linalowajia akilini huwa ni biashara ya duka na hasa maduka yale ya
rejareja kutokana na soko lake kuwa la chapchap mno, unajua hakuna binadamu
asiyekuwa na mahitaji hasa yale ya kila siku kama, chumvi, majani ya chai,
sukari, unga, mchele, sabuni, mafuta, dawa za maumivu kama panadol, nk. Kwa
hiyo unapoanzisha duka ni lazima uuze tu.
Katika kitabu nilichoandika, SIRI YA MAFANIKIO YA
BIASHARA: DUKA LA REJA REJA, nimetumia uzoefu wangu binafsi wa miaka zaidi ya
12 katika biashara hii, tangu nikiwa Msimbazi Kariakoo kwenye vibanda, Sinza,
Buguruni na hata Ubungo. Kitabu hiki ni kazi ambayo najivunia kwani nimeiandika
kutoka moyoni mwangu asilimia mia moja.
Kuna anayeweza kuhoji, “Peter kama umefanya biashara hiyo kwa miaka 12 tuonyeshe mafanikio
uliyoyapata” Na mimi nakujibu hivi; “hebu ‘imagine’ miaka zaidi ya 10 mtu
ukiendesha maisha na familia, bila ya kukutajia mafanikio mengine niliyoyapata,
nadhani wewe mwenyewe unaweza kuona ni kwa kiasi gani biashara hii inaweza
kumuweka mtu mjini”.
Hata hivyo ninachokushauri kama wewe una mpango wa
kuifanya biashara hii au hata tayari unayo na ungependa ikupe kile
unachokitaka, basi nitafute upate kitabu hiki, ninaamini kabisa ikiwa kama
utashindwa hata kujifunza mafanikio niliyoyapata kutokana na biashara hii ya
duka, basi angalao utajifunza changamoto nilizokutana nazo kwa miaka 12 ili na wewe usije
ukazirudia.
Kitabu kina majibu ya maswali mengi yanayowahangaisha wamiliki wachanga wa biashara za rejareja na hata wale waliokwishafikia hatua za kati lakini kikubwa zaidi ni mbinu za usimamizi wa duka au biashara ya rejareja uweze kuona faida yako 'live bila chenga'.
Mbinu za kudhibiti udokozi wa wasaidizi kwa asilimia zaidi ya 98% pamoja na mifumo ya kuleta ufanisi mkubwa. Katika toleo hili jipya la mwaka 2024 tumeongeza Sura mpya kabisa yenye kurasa 8 kuhusu teknolojia mpya ya Akili bandia (AI) inayoleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya biashara za rejareja kote duniani na Tanzania ikiwemo.
Kitabu hiki katika nakala-tete unaweza kukipata kwa njia ya E-mail kwenye kompyuta au simu (smartphone) yako na bei yake ni Tsh. elfu 6 (6,000/=) tu. Unatuma pesa shilingi elfu 6 kwenye namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, kisha nakutumia kitabu muda huohuo unadownload na kusoma au unakisave katika flash/disc yako.
Ikiwa utahitaji kupata kitabu hiki nakala-ngumu na upo jijini Dar es
salaam, wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia namba hizi, 0712 202244 au
0765 553030 na utaletewa kitabu
hicho mpaka pale ulipo. Bei yake ni shilingi elfu 16 tu nauli ya kukuletea ni
juu yangu mwenyewe.
Na kama upo Mikoa mingine kitabu hiki unaweza kukipata kwa
kutuma fedha sh. 16,000/= pamoja na gharama ya kukisafirisha ambayo ni sh. 10,000/= jumla sh. 26,000/= , kwa namba 0712 202244 au 0765 553030, Jina ni Peter Augustino Tarimo. Tupe na maelezo ya mahali/mkoa ulipo kisha tutakutumia kitabu kwa njia ya basi
linalofika hapo ulipo.
Au unaweza pia kukipata katika application ya GETVALUE kwa kujisajili kwenye website hiyo, ukishalipa kwa njia ya mtandao wa simu una-download App yao kwa simu janja kisha unapakua kitabu chako. Anuani ya kujisajili ni hii hapa, bofya haya maandishi, GETVALUE KITABU CHA DUKA LA REJAREJA
Kwa maelezo ya vitabu vingine zaidi vya maendeleo binafsi,
ujasiriamali na biashara tembelea ukurasa huu hapa; SMARTBOOKSTZ.
Mwisho usisahau kuendelea kuwa nasi katika kampeni yetu
ya #jirudishietenaukuuwako au
#makeyourselfgreatagain Narudia tena, hii siyo kampeni, “nguvu ya soda” bali ni
kampeni itakayodumu kwa muda mrefu na kwa wale ambao Ukuu wao
utarudi kipindi kampeni haijamalizika tutawaomba watoe shuhuda zao hapahapa.
Kwa wale pia walio katika Ukuu wao nao nawaomba waendelee
kutufuatilia kuhakikisha wanapata mbinu sahihi zaidi za kuendelea kuushikilia ukuu
huo usijewaponyoka. Ninaposema UKUU ninamaanisha
hali bora kimaisha katika nyanja yeyote ile, inaweza kuwa, kiuchumi, kielimu, kiafya, kiuhusiano, kiibada nk.
Makala hii imeandikwa na:
Peter ugustino Tarimo
Mwabdishi vitabu na Mtaalamu wa michanganuo ya biashara
simu/watsap: 0712202244 / 0765553030
Mtaji wa sh 2.5mil.unatosha kuanzisha duka?
ReplyDeleteUbatosha itategemea wewe unataka kuanza na bidhaa zipi na vifaa vya aina gani, mchanganuo wako ndio utakaokujulisha ni mtaji kiasi gani unahitaji kulingana na vile vitu utakavyohitaji. Mwingine hata hiyo milioni 2.5 kwake ni kubwa sana na mwingine kwake ni kidogo sana. Tuchukulie mfano labda unataka kuanzisha duka aina ya supermarket, milioni 2.5 haiwezi kutosha lakini mfano unataka kuanzisha tu duka dogo lenye mzani, friji, shelfu na bidhaa muhimu tu watu wanazohitaji kwa wingi, milioni 2.5 ni zaidi ya mtaji unaohitaji.
Delete