Bila shaka yeyote ile, chakula ndilo hitaji
la msingi la binadamu lililokuwa muhimu pengine kushinda mahitaji mengine yote
duniani. Hii ina maanisha kwamba, pasipo kujali hali yeyote ile iwe ni ya
kisiasa ama ya kichumi watu ni lazima wale kusudi waendelee kuishi. Kunaweza
kukawa na vita au mdororo mkubwa sana wa kiuchumi, lakini haiwezekani watu
kuishi bila kula.
Ingawa biashara ya chakula ina ushindani
mkali sana, lakini ni biashara yenye faida nono mno endapo itafanywa kwa
usahihi unaotakiwa. Zipo hoteli nyingi na migahawa, achilia mbali mama na baba
lishe au kwa jina maarufu mama ntilie na baba ntilie, lakini bado mahitaji ya
chakula hasahasa katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na
Arusha ni makubwa kupita kiasi.
Kama mtaji wako ni kidogo, huna mtaji wa
kutosha kukodisha jengo au eneo la kufungua mgahawa wako, unaweza ukaamua
kuanzisha biashara hii ya chakula nyumbani kwako na hata ikiwa nyumbani siyo
eneo zuri wateja wanaloweza kuja na kulia pale, basi njia nyingine mbadala
unaweza ukawa unawapelekea wateja wa chakula kule wanakopatikana kwa mfano
katika maeneo yao ya kazi, majumbani au katika maeneo ya vyuo na shule.
Vyovyote vile iwe unao mtaji wa kutosha
kufanya kila kitu wakati wa kuanza ama iwe huna mtaji wa kutosha kufanya kila
kitu lakini hatua za kufuata ili kufungua biashara ya chakula au mgahawa ni
zilezile hazitofautiani.
Zifuatazo hapa chini ni hatua au dondoo
muhimu anazotakiwa kuzingatia mtu yeyote
anayeanzisha biashara ya chakula au mgahawa wa chakula;
1. Soko lako lengwa ni lipi?
Kabla
hata haujatumbukiza senti yako moja ya mtaji kwenye biashara hii ya chakula,
hakikisha unawafahamu vizuri wateja wako(soko utakalouza) Elewa tabia zao,
wanapendelea kitu gani, umri wao na hata huwa wanakula mara ngapi kwa siku.
Mambo hayo yote utayajua kupitia utafiti wa soko au kwa jina jingine upembuzi
yakinifu (Jinsi ya kufanya utafiti wa
soko ni somo lililopo ndani ya kitabu cha
“MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” na limefafanuliwa kila kitu pamoja na
mifano)
2. Ainisha ni aina gani ya vyakula
utakavyouza.
Bado
hapa utategemea sana taarifa utakazozipata kutokana na utafiti wako wa soko(market survey) Kumbuka utafiti wa soko
siyo lazima uufanye kitaalamu sana, zipo njia nyepesi na zimeainishwa vizuri tu
katika kitabu cha Michanganuo ya
biashara na Ujasiriamali. Ni lazima aina za vyakula utakavyouza ziendane na
aina za vyakula wateja wako walengwa wanavyopendelea.
3. Andika Mchanganuo/mpango wa biashara
yako ya mgahawa
Mpango
wa biashara siyo dude kuuubwa!, linalotisha, kwa kifupi tu unaweza ukaorodhesha
katika karatasi pointi zile muhimu zote zinazoihusu biashara yako kuanzia wazo
la biashara, mtaji mpaka faida unayotarajia kupata kwa makisio mepesi, wala
huhitaji kuwa sahihi kwa asilimia kubwa.
4. Tafuta mtaji.
Sasa
umeshajua makadirio ya mtaji kutokana na mchanganuo mdogo uliofanya. Mtaji
itategemea, unaweza ukatumia fedha zako mwenyewe kama unazo, au unaweza ukaenda
kukopa kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki, saccos au taasisi nyingine yeyote ile
itakayokubali kukukopesha. Unaweza pia ukauza mali yako ya thamani kama vito au
kuweka rehani vyombo nk.ili kupata mtaji wa kuanzishia biashara yako ya
chakula.
Kumbuka
haiwezekani ukaendesha biashara ya mgahawa au chakula pasipo kuwa na fedha za
kugharamia vitu kama, kodi ya jengo utakalofanyia biashara, malighafi(vyakula
vibichi, matunda na mbogamboga), mishahara ya wafanyakazi, bima(kwani kitu kama
moto unaweza ukazuka ghafla na kama huna bima ukala hasara kubwa) na gharama za
masoko au matangazo.
5. Chagua eneo zuri.
Wakati
unachagua eneo la kuweka biashara yako, zingatia sana vitu kama, wingi wa watu
eneo hilo, sheria kutoka mamlaka za serikali za mitaa, kufikika kwa urahisi na
wateja ikiwemo na parking ya magari, pango la nyumba na historia kwa ujumla ya
eneo husika. Hii hasa ni kwa wale waliokuwa na mtaji mkubwa wa kutosha lakini
kwa upande wa wale wenye mtaji kidogo kama nilivyotangulia kusema, wanaweza
biashara hii wakaifanyia nyumbani na kusambaza vyakula kwenda maeneo ya jirani
au maofisini na katika biashara za watu.
6. Tengeneza mandhari ya kuvutia ya mgahawa wako
Tenga
maeneo mbalimbali kama vile, sehemu ya jiko, sehemu ya kulia chakula “dinning”
stoo, sehemu ya kunawia mikono nk. Hakikisha madhari nzima ya biashara yako
inakuwa ni yenye kuvutia.
7. Hakikisha unazingatia usalama kwa
kuweka vifaa vya usalama kama vile vya kuzuia moto pamoja na
bima. Kuwa pia na mwanasheria kwa ajili ya maswala yahusuyo sheria.
8. Kuwa na wasambazaji maalumu wa vifaa
kama vyakula na matunda na mbogamboga, utakaowekeana nao
mikataba ya kukusambazia vitu hivyo na uhakikishe bei watakazokuuzia ni za
chini kwa kadiri inavyowezekana kusudi usipate hasara.
9. Nunua vyombo muhimu kama vile
mafriji,viti, meza, majiko, oven, vifaa vya chipsi,
sahani, bakuli, vijiko, sufuria nk.
10. Ajiri na kuwapa mafunzo wafanyakazi.
Ajiri
meneja na wafanyakazi, wape mafunzo pamoja na kuwapangia kila mmoja jukumu lake
sambamba na kupatana nao malipo kabla hawajaanza kazi.
11. Tangaza mgahawa wako.
Usipowajulisha
watu, hamna mtu atakayefika kuja kula mgahawani kwako. Kuna njia nyingi
unazoweza ukazitumia kutangaza kama vile, kusambaza vipeperushi kwa majirani,
lakini ni vyema pia ukatengeneza mpango mkakati wa biashara au masoko
utakaotumika wakati wa kutangaza biashara yako(Kitabu cha MICHANGANUO NA UJASIRIAMALI
kimefafanua vizuri jinsi ya kuandika mpango mkakati wa biashara pamoja na mfano
wa mpango mkakati wenyewe halisi)
Unaweza
pia ukawatangazia majirani kwamba siku rasmi ya ufunguzi kutakuwa na chakula
bure bila malipo, ukawagawia kila mmoja kuponi atakayokuja nayo kula. Wakisha
kula watakwenda kuitangaza biashara yako vizuri sana kwa watu wengine.
12. Tanua biashara yako.
Wakati
ukifika sasa wateja wameshakuwa wengi, hakikisha unakuwa na leseni na vibali
vyote vinavyohitajika kwa ajili ya biashara ya mkahawa kwani sasa serikali
itakuwa imeshaanza kutambua uwepo wako. Kama ulikuwa unafanyia nyumbani, ni
wakati sasa wa kwenda kukodi jengo eneo kubwa au hata ikiwezekana unaweza
ukabadilisha mgahawa wako kuwa hoteli.
………………………………………………………………….
Ndugu
msomaji, kama wewe ni mpenzi wa biashara hii ya chakula, hususani mgahawa au
hoteli, basi nakushauri usikose kujipatia kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NAUJASIRIAMALI ili usome kwa kina mchanganuo wa biashara ya mgahawa uitwao, JANE FAST FOOD. Agiza kitabu hicho
kutoka kwangu kupitia namba za simu, 0712
202244 au 0765 553030 jina ni Peter Augustino Tarimo,
na utaletewa kitabu cha karatasi mpaka pale ulipo kama unaishi Dar es salaam.
Kama
upo Mkoani, mkoa wowote ule, tuma pesa shilingi 20,000/= pamoja na gharama za
usafirishaji kupitia namba hizo hapo juu na nitakutumia kitabu kupitia basi
linalofika kule ulipo.
Pia
kitabu hiki kipo katika mfumo wa softcopy
na naweza nikakutumia kwa njia ya E-mail.
Chakufanya tuma pesa shilingi 10,000/=
kwenye namba za simu zilizotajwa pale juu pamoja na anuani yako ya e-mail kwa meseji, kisha na mimi nitakurushia kitabu
hiki kupitia email yako kama PDF. Kwa vitabu vingine zaidi na Michanganuo ya Biashara tembelea duka letu mtandaoni liitwalo SMART BOOKS TZ
BUSINESS PLANS / MICHANGANUO YA BIASHARA
Karibu, Tunaandika mpango wa biashara yeyote ile kwa ajili ya kuombea mkopo, kuwasilisha kwa wabia, wawekezaji na hata kwa ajili ya uendeshaji wenye tija wa biashara. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakamilisha kazi kwa muda muafaka.
Ikiwa pia unapenda uandike mwenyewe na huna materials za kukusaidia tunavyo vitabu vizuri cha kiswahili na kiingereza, Templates/vielezo, Seminars na Samples au Michanganuo kamili iliyokuwa tayari unayoweza kufuatisha baadhi ya vitu wakati ukiandika wa kwako. Gharama ya package nzima ni rahisi sana na tunatuma kwa njia ya email kama softcopy
Kupata moja kati ya huduma hizo 2 za Michanganuo wasiliana nasi kwa namba, Whatsapp/call: 0765553030 au Simu/sms: 0712202244
Ikiwa pia unapenda uandike mwenyewe na huna materials za kukusaidia tunavyo vitabu vizuri cha kiswahili na kiingereza, Templates/vielezo, Seminars na Samples au Michanganuo kamili iliyokuwa tayari unayoweza kufuatisha baadhi ya vitu wakati ukiandika wa kwako. Gharama ya package nzima ni rahisi sana na tunatuma kwa njia ya email kama softcopy
Kupata moja kati ya huduma hizo 2 za Michanganuo wasiliana nasi kwa namba, Whatsapp/call: 0765553030 au Simu/sms: 0712202244
Nice
ReplyDeleteThan you and be blessed!
DeleteAsante kwa ufafanuzi mzuri.
ReplyDeleteNashukuru sana nilikuwa natafuta muongozo mzur
ReplyDeleteasanteni sana
ReplyDeleteAsante Kwa SoMo nzuri
ReplyDelete