Ndani ya darasa letu la WHATSAP na CHANNEL YA TELEGRAM la MICHANGANUO-ONLINE -MASTERMIND-GROUP tunajifunza kila siku masomo yenye maudhui ya pesa pamoja na Semina za mara kwa mara kuhusiana na uandishi wa Michanganuo ya Biashara za Kitanzania zilizo na fursa kubwa ya kuzalisha faida.
Kujiunga
na Darasa hili, mwanachama hulipia kiingilio cha mwaka mzima (niezi 12) shilingi elfu 10 tu na tunampatia baadhi ya vitabu na Michanganuo ya biashara kwa ajili ya rejea wakati wa kujifunza.
Darasa hili limeanzishwa mahsusi kwa lengo la kuhakikisha wale wote wanaonunua
kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lengo la kusoma
michanganuo mbalimbali ya biashara pamoja na kujifunza namna ya kuandika
michanganuo ya biashara zao wanapata fursa ya kuwa karibu zaidi na wakufunzi wa
somo hili ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali yanayowatatiza na mwisho
kuhakikisha wanaandaa mipango ya biashara wanayoitaka wao wenyewe wakipewa
usaidizi kila wanapokutana na ugumu wowote ule.
Katika maisha ya biashara na pesa
ipo siku unaweza kujikuta unauhitaji mpango wa biashara. Hata
kama hutahitajika kuandika mwenyewe lakini kuna wakati unaweza ukatakiwa labda na benki au taasisi yeyote ile ya fedha uwasilishe mpango wa biashara yako. Sasa utakapokwenda kwa mtaalamu akuandikie unatakiwa angalao uwe na uelewa wa msingi
juu ya mpango wa biashara ndipo mtaalamu aweze kukuandikia mchanganuo mzuri baada ya kukuhoji maswali kuihusu biashara yako.
Si hivyo tu kuna sehemu nyingine huwa wanahitaji upeleke mpango/mchanganuo
wa biashara yako na kuuwasilisha mwenyewe kwa mdomo wako. Hivyo ni
muhimu sana mtu yeyote uliyekuwa na ndoto za kuja kuwa mfanyabiashara na
mjasiriamali mkubwa kujifunza walao hata kwa kusoma tu jinsi ya kuandaa mpango
wa biashara na namna mipango yenyewe halisi inavyokuwa.
Lakini faida kubwa zaidi pengine kushinda zote za mtu
kufahamu michanganuo ya biashara ni ile ya kuendesha biashara yako vizuri kwa
ufanisi, unapofahamu namna ya kupanga biashara yako unazidisha uwezekano wa
mafanikio katika biashara hiyo. Faida haipo kwenye mchanganuo wenyewe kama
kurasa na maandishi hapana, bali ipo kwenye mchakato mzima wa kufikiria kwani
MPANGO WA BIASHARA ni kila kitu kinachohusiana na biashara kuanzia wazo lenyewe
la biashara mpaka unapofikia hatua ya kupata faida.
Kwa hiyo kile kitendo tu cha kukaa na kuifikiria biashara
yako, mwanzo mwisho namna utakavyoiendesha ni mchanganuo tosha wa biashara hata
pasipo kuchukua kalamu na karatasi. Ndiyo maana nasisitiza kuwa unaweza
kujifunza michanganuo ya biashara hata kama hupendi kuiandika na hilo linatosha
wewe kuendesha biashara yako vizuri kimkakati.
Ukiwa mwanachama wa Group hili unapata fursa ya kuuliza swali lolote lile kuhusiana na Michanganuo na Ujasiriamali kwa ujumla lakini pia kupewa usaidizi kwenye kuandaa mpango wa biashara utakayo.
Namba za kulipia ada sh. elfu 10 ni 0765553030 au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Na baada ya ,alipo Tuma ujumbe ukisema;
"NIUNGANISHE NA MASTERMIND-GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE"
*TUNATOA PIA HUDUMA YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA ZA AINA ZOTE KWA GHARAMA RAFIKI*
ninashukuru kwa msaada wa mawazo mazuri kwani inatufungua kuwa na maono ya mbali kutoka ki biashara
ReplyDeleteTunashukuru pia kwa mrejesho wako mzuri na tunaahidi kuendelea kuwaletea mambo mazuri zaidi siku za usoni
Deletehi
ReplyDeleteHi Hans How do you do?
DeleteInachukua Muda gani mpaka kuunganishwa
ReplyDeleteMara tu ulipiapo tunakuunganisha muda huohuo
DeleteNimependa somo kwanza nifanye mpango wa kujiunga
ReplyDeleteUnakaribishwa sana Mdau wetu, njoo tujifunze ujasiriamali na mambo ya fedha.
DeleteNi biashara ipi au aina ipi ya ujasiriamali ambayo inauwezo wa kukua na kufikia hatua ya kiwanda kikubwa,hasa katika kilimo
ReplyDelete