Mwandshi wa kitabu hiki, Rich Dad Poor Dad bwana Robert Kiyosaki, anaamua
kuivalia njuga elimu ya fedha, elimu ambayo kwa miaka mingi sasa duniani kote
nahata katika zile nchi zilizoendelea kama Marekani Uingereza na China, imekuwa
kamwe haifundishwi mashuleni wala katika vyuo vya kawaida vya jadi
vilivyozoeleka. Hiki ni kitabu cha 3 katika mfululizo wetu wa viatu 300 vya pesa na mafanikio maarufu na vilivyosomwa zaidi duniani.
Kiyosaki anasimulia jinsi alivyokuwa na
mababa wawili, baba yake halisi aliyempa
jina la “Baba masikini au Poor Dad” ambaye maisha yake yote alikuwa kutwa kucha
katika miezi yote 12 ya mwaka yeye ni kukimbizana na ajira ya mshahara tu
iliyomwacha kila wakati akihangaika kulipa madeni yasiyokauka.
Kwa upande mwingine baba yake wa pili, huyu
hakuwa baba yake halisi bali alikuwa ni baba wa hiyari na alimpa jina la “Baba
tajiri au Rich Dd” Baba huyu sifa yake kubwa alikuwa ni mtu tajiri sana(Milionea)
aliyeacha shule(drop out) na kuamua kuwekeza katika vitegauchumi mbalimbali huku
akizingatia zaidi elimu ya pesa isiyofundishwa rasmi katika mashule na vyuo vya
kawaida.
·
Ni kwa kupitia kwa baba huyu tajiri, Kiyosaki
ndipo alipoweza kujifunza na kuiga maarifa adimu sana ya pesa, kama vile;
·
Tofauti
iliyopo baina ya rasilimali na madeni(asset & liability)
·
Kile
matajiri wanachowafundisha watoto wao kuhusiana na pesa.
·
Ukweli
kwamba hata nyumba ya kuishi unayomiliki kumbe siyo rasilimali kwako bali ni deni!, na
·
Umuhimu
wa kufahamu namna ya kuwekeza na elimu ya ujasiriamali kwa ujumla katika
kujipatia uhuru kifedha kwenye dunia hii ya utandawazi uliojaa ushindani kila
kona.
Maudhui makuu yaliyomo kwenye kitabu hiki
kilichojipatia umaarufu mkubwa sana duniani ni kwamba, siri kuu iliyojifichanyuma ya matajiri wote duniani si nyingine bali siku zote matajiri ndio
wanaotumikiwa au kufanyiwa kazi na fedha zao wakati masikini wao ndiyo
huzitumikia fedha au kuzifanyia fedha kazi.
Ndugu msomaji, hebu kitafute kitabu hiki
ukisome ili uweze kuijua elimu hii ya fedha isiyofundishwa mashuleni wala
vyuoni, uweze kufahamu jinsi unavyoweza kuzifanya fedha zikutumikie badala ya wewe
kuzitumikia.
So fortunes to keep running over your mind boggling on the web diary. Your online diary presents to me a great deal of fun.. Favorable circumstances with the site.
ReplyDeleteBookzhub
Thank you John!
DeleteHow can I download this book??
ReplyDelete