Mara nyingi watu hukaa na kutafakari ni
biashara zipi wanazoweza wakaanzisha ambazo zina fursa kubwa wakati ujao ukizingatia
mabadiliko makubwa na ya haraka yanayotokea kila siku duniani. Biashara
unayoweza kuiona leo kuwa inayo fursa nzuri ya kutengeneza faida, miaka miwili
au mitatu ijayo siyo tena itakayokuwa biashara yenye kulipa vizuri.
Kama mjasiriamali makini ni lazima ujiulize
hivi, “ni wazo gani la biashara linaloweza kuja kuwa na fursa kubwa baada ya
miaka tuseme miwili, mitatu au hata kumi ijayo?”. Karne ya leo si kama
karne zilizopita, wakati Waingereza walipoanzisha Mapinduzi ya viwanda karne ya
19, wazo la biashara au fursa kubwa iliyoonekana wakati huo kushika chati ya
juu kabisa ilikuwa ni biashara ya kuunda na kuuza mitambo mbalimbali kwa ajili
ya kuzalisha viwandani.
Wamarekani nao katika karne ya 20 wakiwa
katika kilele cha ukuu wao, wakatawala duniani kwa wazo lao kuu la biashara ya
uzalishaji na utoaji huduma mbalimbali. Leo hii karne ya 21 iliyopewa jina kuwa
ni karne ya mawasiliano, tumeshuhudia wakiibuka miamba mingine kama Uchina na
hata India wakiwapa ushindani mkali kwelikweli miamba wengine waliokuwa wametawala
uchumi wa Dunia hii kwa kipindi kirefu.
Kinachowapa nguvu kubwa sana miamba hao
wapya ni teknolojia ya mawasiliano. Leo hii Wamarekani hawaishi kulialia
mitandao yao kudukuliwa na kuibiwa siri kibao kuanzia za kibiashara na hata
zile nyeti kama za uchaguzi mkuu pasipo hata kuwa na nguvu kubwa ya kujitetea.
Ingawa hatuwezi kufahamu kwa uhakika mia kwa
mia kuwa ni biashara gani au mawazo gani ya biashara zitakazoshika nafasi ya
juu miaka michache ijayo, lakini watu tunaweza kutabiri ni biashara gani
zitakazoweza kuja kushika chati katika miaka ijayo kwa kutumia vigezo
mbalimbali.
Kidunia sekta zinazotabiriwa kuja kuwa tishio
kwa mujibu wa taasisi iitwayo, “World Economic Forum”(WEF) ni hizi hapa chini;
Biashara
ya simu za mkononi na teknolojia ya kuhifadhi data mtandaoni(Cloud technology)
Kompyuta
zenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu.
Vyanzo
vipya vya nishati na teknolojia
Biashara
ya kwenye mtandao(Intaneti)
Biashara
ya vifaa vinavyojiendesha vyenyewe kama vile maroboti, vyombo vya usafiri kama
ndege na magari yasiyokuwa na dereva nk.
Teknolojia
za viumbehai(Biotechnology)
Tukirudi katika mawazo ya biashara zinazotabiriwa na watu
wengi hapa Tanzania kama biashara zinazotabiriwa kuwa na fursa kubwa miaka
ijayo kuanzia mwaka 2018 na kuendelea mpaka 2020 na zaidi, tunaweza kuzitaja
fursa au mawazo ya biashara hizo kuwa ni hizi hapa;
1. Biashara ya ujenzi.
Ujenzi
hasa wa nyumba za makazi, maofisi na miundombinu mbalimbali kama barabara na
madaraja. Ongezeko kubwa la watu hasa mijini linaifanya fursa hii kuwa ya
kipekee kabisa na itakayoshika chati kwa kipindi kirefu kijacho. Vilevile nchi
kama Tanzania bado ni nchi inayoendelea hivyo ujenzi unahitajika mno. Kwa hiyo
wazo la kuanzisha biashara kama ya vifaa vya ujenzi(hardware), ujenzi wa majumba(Real
estate) na hata udalali wa majumba na viwanja ni mawazo muafaka ya biashara
kabisa kuanzia mwaka huu, ujao na kuendelea.
Kuna
mtu mmoja, mwanamke, hivi karibuni aliniacha hoi, alisema kuwa yeye sasa
ameshachoka na biashara nyingine zote,
anatafuta mtaji japo kidogo tu akafungue hardware yake maeneo ya nje kidogo ya
mji wanakoanza kujenga, akasema hata kama ataanza na sementi mfuko mmoja ya
kupima kwa kilo, hilo halimpi wasiwasi kwani biashara ya vitu vya ujenzi ina
uhakika wa wateja na bidhaa zake haziharibiki upesi. Hata usipouza mwaka huu
utauza mwakani.
2. Wazo la biashara ya kilimo cha mazao ya
chakula.
Fursa
ya kilimo cha mazao ya vyakula nayo inatabiriwa kuwa itakuwa na uhitaji mkubwa
miaka ijayo kutokana na ongezeko kubwa la watu mijini na vijijini. Ongezeko
hilo la watu linaenda sambamba na ongezeko la watu wasiopenda kazi ya kilimo,
wao manapenda kuishi mijini na kufanya kazi za uchuuzi tu. Ukiwa mjanza
ukakamata fursa hii utachuma senti zao kidogo wanazopata kutokana na uchuuzi
kwani hakuna binadamu mwenye ujanja wa kuishi bila kula hata ikiwa anaishi London,
New York au Paris.
……………………………………………………………………....
Ndugu
msomaji, ungana nasi katika kampeni yetu ya “jirudishie tena ukuu wako”(Make
yourself Great again) kwa kusoma makala hapa katika blogu hii kila siku.
Jitahidi pia kupata kitabu cha “Kanuni ya kujifunza ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO” tunachotoa bila malipo kwa muda mfupi
na kisha kitaanza kuuzwa pindi idadi ya watu waliokusudiwa itakapotimia.
Jipatie
pia moja kati ya vitabu vingine vifuatavyo au vyote ukiweza lakini napendekeza
zaidi usikikose kitabu cha, MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” kuona vitabu hivyo vyote fungua blogu hii hapa,
SMART BOOKS TANZANIA
Ili
tuweze kwenda sambamba zaidi, jiunge na Darasa la semina ya kujifunza jinsi ya
kuandaa na kuandika mpango wa biashara yako au biashara yeyote ile utakayotaka.
Kujiunga na darasa hilo fungua hapa, DARASA
LA SEMINA YA MCHANGANUO WA BIASHARA.
Nahitaji kitabu cha ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, je Nitaipata wapi?
ReplyDelete