Sasa wale wanachama walio na ufunguo wa
kuingia katika Darasa la Michanganuo ya Biashara(Tanzanaia Online
School Of BusinessPlanning) wanaweza kudownload
bure mfano wa mchanganuo wa biashara(Business plan Template) ya kiswahili
ambayo mtu unapotaka kuandika mpango wa biashara yeyote ile, unajaza tu taarifa
zako kuhusiana na biashara hiyo pasipo kuumiza kichwa sana kufikiria ni nini
cha kuandika.
Template(kielezo) hicho kina sehemu zote zinazotakiwa
kujazwa ili mchanganuo wa biashara ukamilike, pamoja na maelekezo muhimu
yanayokuambia ni kipi cha kuandika katika sehemu husika. Ni rahisi sana
kuandika mchanganuo wa biashara na katika muda mfupi kwa kutumia njia hii hasa
ikiwa wewe haujawa mzoefu vya kutosha katika utayarishaji wa mipango ya
biashara.
Template(mfano) upo katika fomati ya “word template” na una
sehemu nane ambazo kila moja imegawanyika vijisehemu vidogovidogo ndani huku
kukiwa na maelezo kwa lugha ya kiswahili. Wewe utajaza maelezo yanayofanana na
kuendana na biashara unayotaka kuiandikia mpango wa biashara na ukishamaliza
kuandika kila kitu unasave, basi umemaliza.
Darasa linaendelea na wanachama/wanafunzi katika ngazi ya
“Ordinary
Level” wanaongezeka. Kama ulikuwa hujajiunga ni wakati wako sasa
kufanya hivyo ikiwa upo ‘serious’ kweli na kupanga biashara yako. Mpango wa
biashara utakusaidia mambo mengi ikiwemo kuijua biashara kwa kina hata kama
hupendi kwenda kuombea mkopo.
Unapoelewa mtiririko mzima wa biashara unayoifanya
kuanzia mtaji mpaka faida utakayopata, akilini unakuwa umeshajijengea picha ni
kitu gani unachotaka kukifanya hivyo hautakurupuka tena na kufanya vitu kwa
mtindo wa zima moto.
Ni kweli kabisa siyo kila utakachopanga kitaenda vilevile
ulivyopanga hapana, ndiyo maana unatakiwa mpango wa biashara yako uufanyie
marekebisho mara kwa mara kulingana na hali halisi inavyokuja kujitokeza. Hata
kama yatatokea matukio usiyokuwa umeyatarajia utakabiliana nayo vizuri zaidi
pasipo kukuchanganya akili.
Dhana ya mipango, asijekukudanganya mtu yeyote kuwa
haipo, sijui ni kupoteza muda, mara mipango siyo matumizi, ni uwongo mtupu,
hakuna binadamu asiyepanga ila kinachotokea hapa ni watu kuchukia dhana ya
kupanga kwa sababu ni kweli matokeo mara nyingi hayawezi kuwa sawasawa na kile
ulichopanga kwa asilimia 100%. Lakini ukweli utabaki palepale kwamba kupanga
kuna faida zake na ni nyingi kushinda kutokupanga kabisa.
Hebu fikiria vitu hivi vifuatavyo kama kusingelikuwa na
mipango ni nini kingelitokea?,
Vita:
mpaka unaona majeshi yakilipua mizinga siyo uamuzi wa siku moja kama mtu
anazima moto, ni maandalizi na mikakati ya siku, miezi na hata miaka kadhaa
inayohusisha bajeti, rasilimali watu na kila kitu mfano wa vile uonavyo mtu
akianzisha biashara.
Harusi: Ni
moja ya vitu tunavyovipenda mno, na ukitaka kujua watu ni mahodari wa
kutengeneza michanganuo(plans), basi hudhuria vikao vya harusi, unaweza ukasoma
makala hii hapa, Ni nini kilichokuwa nyuma ya harusi nzuri ya kupendeza?
Chakula: Hivi ni kwanini nchi au hata mtu mmoja mmoja huamua kujenga maghala kwa ajili ya kuhifadhi chakula cha ziada asisubiri mpaka njaa itakapopiga hodi ndipo aanze kukimbiakimbia kutafuta chakula? Je, kujiandaa kwa njaa kwa kujenga ghala hiyo siyo mipango?
Kuna mifano mingi, ila ninachotaka kukueleza hapa tu ni
kwamba, kama unadhani kupanga ni kupoteza muda, basi jaribu kufanya mambo yako
kwa mitindo ya zima moto uone matokeo yake. Tena watu wengi wanaoponda suala la
mipango utakuta wao mambo yao yanakwenda vizuri kutokana na mipangilio mizuri
ya shughuli zao, huku wakihubiri kupanga ni kupoteza muda.
………………………………………………………………….....…
Kujiunga na Darasala Michanganuo gharama yake ni shilingi elfu 10 tu, ambapo baada ya kulipa
pesa kupitia namba 0712 202244 au 0765
553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, unatuma na meseji yenye anuani yako ya Gmail ambayo ndiyo tutakayotumia
kukuunganisha na blogu hiyo ya darasa. Tunakupa pia na kitabu cha Michanganuoya Biashara na Ujasiriamali (softcopy) “free of charge”
Sehemu iliyopita. Ifuatayo.
Sehemu iliyopita. Ifuatayo.
0 Response to "MFANO WA MCHANGANUO WA BIASHARA(TEMPLATE) UNAPOTAKA KUANDIKA MPANGO WAKO"
Post a Comment