RATIBA YA MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA KATIKA SEMINA YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

RATIBA YA MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA KATIKA SEMINA YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA


SEMINA YA KUANDAA MPANGO WA BIASHARA(BUSINESS PLANNING)

Kuhusu Semina
Semina ya kuandika mpango wa biashara au semina ya michanganuo ya biashara, ni masomo ya kina ya jinsi ya kuandaa na kuandika mpango wa biashara  yatakayotolewa kwa njia ya mtandao hasa kwa kupitia e-mail, blogu maalumu(Darasa la michanganuo ya biashara) pamoja na njia ya sauti(mp3). Njia zote 3 zitatumika.

Washiriki kila baada ya somo watapewa fursa ya kuuliza maswali pamoja na kupewa maswali na mwisho wa semina kila mshiriki ataandaa mpango wa biashara yake atakayochagua yeye mwenyewe huku akipewa usaidizi wa karibu na mkufunzi wa semina.

YAFUATAYO NI MASOMO YA SEMINA YATAKAYOTOLEWA

SOMO LA KWANZA
Maana ya Mchanganuo/Mpango wa biashara
ü Majina mbalimbali ya mpango wa biashara
ü Ni kina nani wanaohitaji mpango wa biashara
ü Aina za michanganuo ya biashara na tofauti zake.

SOMO LA PILI
Jinsi ya kuanza kuandika mpango/mchanganuo wa biashara
ü Mawazo utayatoa wapi?
ü Utafiti wa soko/biashara au feasibility study
ü Vipengele/sehemu za mpango wa biashara
ü Ni kipengele kipi huanza na ni kipi humalizia.

SOMO LA TATU
Kasha la nje, kichwa cha mchanganuo na Yaliyomo
ü Utajifunza ni vitu gani hukaa nje kwenye jalada na namna ya kuvipanga
ü Pia utaona ni nini huwekwa kwenye yaliyokuwemo

SOMO LA NNE
Muhtasari.
ü Ni vitu gani muhimu vinavyounda Muhtasari?
ü Mifano ya  muhtasari ya biashara mbalimbali
ü Aina za muhtasari
ü Muda muafaka wa kuandika Muhtasari
ü Mbinu za kuandika Muhtasari utakaomfanya msomaji yeyote asiweze kukwepa kusoma mpango wako mzima.

SOMO LA TANO
Maelezo kuhusu biashara au Kampuni
ü Umiliki wa biashara, kampuni, ubia au mtu binafsi
ü Historia ya kampuni.
ü Usajili wa biashara
ü Jina na eneo biashara ilipo
ü Dhamira kuu
ü Maono
ü Malengo ya biashara
ü Siri ya mafanikio.

SOMO LA SITA
Maelezo kuhusu Bidhaa
ü Bidhaa au huduma utakazouza
ü Kwanini wateja wanunue kutoka kwako?
ü Faida atakayipata mteja kutokana na bidhaa au huduma zako
ü Namna utakavyopata malighafi au bidhaa na jinsi utakavyokidhi mahitaji ya wateja
ü Teknolojia itakayotumika
ü Mabadiliko ya bidhaa au huduma katika soko kwa siku za baadae.

SOMO LA SABA
Mpango/uchanganuzi wa soko.
ü Wateja wako ni kina nani?
ü Mahitaji ya wateja na tabia zao
ü Kwanini wanunue kutoka kwako na siyo washindani?
ü Mwelekeo wa soko na jinsi wateja walivyosambaa
ü Ukubwa wa soko unalomiliki
ü Ukuaji wa soko
ü Tathmini ya sekta uliyopo
ü Washindani wako wakubwa
ü Tathmini ya Nguvu, Udhaifu, Fursa  na Vikwazo

SOMO LA NANE
Mikakati na utekelezaji.

Mkakati wa masoko
ü Bidhaa/Huduma,
ü Bei,
ü Matangazo,
ü Eneo na Usambazaji
ü Huduma kwa wateja
ü Programu ya masoko

Mkakati wa mauzo
ü Makisio ya mauzo
ü Programu za mauzo

Utekelezaji/Uendeshaji
ü Kazi za kila siku
ü Mpango wa utekelezaji vitendo na muda malumu wa utekelezaji

SOMO LA TISA
Wafanyakazi na Uongozi
ü Mchoro wa Utawala
ü Timu ya viongozi, wasifu wao na majukumu watakayohusika nayo
ü Idadi ya wafanyakazi na sifa zao
ü Pengo la wafanyakazi na mahitaji ya wafanyakazi ya siku za baadae.
ü Jedwali la mishahara.


SOMO LA KUMI
Makisio ya Taarifa za Fedha
ü Unaingiza vipi fedha?
ü Muhtasari wa mahitaji yote ya fedha, vyanzo na matumizi yake
ü Makisio ya gharama za awali(unazolipa mara moja)
ü Makisio ya mali(rasilimali) za kudumu
ü Makisio ya mauzo
ü Makisio ya gharama za mauzo
ü Gharama za kudumu za uendeshaji
ü Makisio ya kodi na riba ya mikopo
ü Makisio ya Faida na Hasara
ü Makisio ya fedha taslimu
ü Makisio ya mali na madeni(Mizania ya biashara)
ü Tathmini ya mauzo yatakayorudisha gharama zote (Break even analysisi)
ü Uwiano wa Sehemu muhimu za biashara.

SOMO LA KUMI NA MOJA
Viambatanisho Muhimi
ü Majedwali na vielelezo
ü Leseni, vibali na stakabadhi za kodi na benki
ü Taarifa za mahesabu ya nyuma
ü Kopi za barua na mikataba mbalimbali.

...................................................................................................


ADA YA KUJIUNGA NA SEMINA

v Kujiunga na semina hii, ada ni shilingi elfu 10 tu.

v Kila siku utasoma somo moja

v Njia zitakazotumika ni, E-mail, Blogu hii maalumu na Sauti(mp3)

v Unaweza kumuuliza mkufunzi maswali muda wowote

v Mwisho wa semia unaandaa mpango wa biashara na utapewa msaada wowote utakaohitaji kwa mkufunzi

v Utapewa na kitabu cha michanganuo PDF/softcopy bure

v  Wale wateja wote waliokwishanunua kitabu cha Michanganuo na Ujasiriamali watajiunga bure bila malipo.


Kwa maelezo zaidi ya semina bonyeza hapa, Shule ya Michanganuo ya Biashara, au wasiliana na mkufunzi kwa simu, 0712202244  au  0765553030,  Peter Augustino






0 Response to "RATIBA YA MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA KATIKA SEMINA YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA"

Post a Comment