Utangulizi.
Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala katika
blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali, ninayezungumza hapa ni Bwana Peter
Augustino, Mhamasishaji mkuu na mwandishi katika blogu yako hii.
Ninayofuraha kubwa kukujulisha kwamba ile
semina yetu ya kujifunza jinsi ya kuandika mpango wa biashara sasa imeanza
rasmi katika blogu maalumu ya DARASA LA SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA. Pia hapa
nitakuelezea mambo machache kuhusiana na Semina hiyo, tafadhali nakuomba tuwe
pamoja.
Madhumuni
ya Semina
Madhumuni makubwa ya kuanzisha semina hii ya
kuandaa mpango wa biashara ni kuhakikisha wasomaji wote wanaonunua au
waliokwishanunua kitabu chetu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
wanatimiza lengo lao la kujifunza na kufahamu kwa uhakika kabisa namna ya
kuandaa au kuandika mpango wa biashara.
Namna
Semina Itakavyoendeshwa.
Masomo ya semina hii ambayo jumla yake ni 11
yatatolewa kwa kupitia mtandao wa intaneti kwa njia tatu, ya kwanza ni kupitia
e-mail ambapo masomo yatatumwa moja kwa moja kwenye email ya mshiriki. Njia ya
pili ni kwa njia ya sauti(MP3) ambapo masomo yatapatikana katika blogu ya
Darasa la semina ya michanganuo ya biashara na mshiriki atapakua masomo hayo. Njia
ya tatu masomo yatatolewa katika mtindo wa PDF kwenye blogu hiyo maalum na
washiriki pia watapakua ama kudownload masomo wakiwa ndani ya blogu hiyo.
Kwanini
tunasema semia hii ni ya kipekee na haijawahi kutokea?
Ndugu msomaji, gharama za semina hii
ukilinganisha na faida mshiriki atakazozipata ni ndogo sana kiasi kwamba
haijawahi kutokea semina nyingine hapa nchini ya namna hiyo. Hebu fikiria,
shilingi elfu 10 tu, unajifunza michanganuo ya biashara kwa kina kabisa
sambamba na kupewa bure softcopy ya kitabu cha Michanganuo ya biashara na
ujasiriamali. Na ikiwa basi hupendi softcopy unapenda kitabu halisi cha karatasi
unaongeza hapo shilingi elfu 10 tu kwa ajili ya uchapaji.
Tunatambua hali ngumu ya kiuchumi iliyokuwepo
sasa hivi nchini, lakini nikutoe tu wasiwasi kwa kukuhakikishia kwamba, kamwe
hautaweza kuja kujutia fedha yako unayotoa kwa ajili ya semina hii.
Muda wa kutosha wa kuwa karibu na mkufunzi wa
semina hii huku ukipewa msaada wowote ule utakaohitaji mpaka umeelewa na
kuandika mpango wako mwenyewe wa biashara. Waandaaji tumejitolea kwa hali zote
katika kipindi chote cha semina kuhakikisha hakuna mshiriki atakayeachwa nyuma
au kushindwa kutimiza lengo lake la kuandika mpango wa biashara. Na zaidi ya
yote tutahakikisha mshiriki anapata huduma zitakazopita matazamio yake na
gharama aliyotoa.
Muda
wa semina
Ndugu Msomaji, tunatambua kujifunza
Mchanganuo wa biashara siyo zoezi unaloweza ukalifanya siku moja ndiyo maana
hatukuweka ukomo maalumu wa muda tutakaokuhudumia. Mwisho wa idadi ya masomo ni
11, lakini mwisho wa darasa ni pale mshiriki atakapohitimu kwa kuandika mpango
wa biashara anayopenda mwenyewe ambao ndiyo cheti cha kuhitimu semina.
Ndugu msomaji wangu, kushiriki semina hii ni
rahisi sana, lipia semina kupitia namba ya simu 0712 202244 jina ni Peter
Augustino Tarimo, au namba zetu nyingine zilizomo kwenye blogu hii. Kisha tuma
kwa meseji anuani yako ya baruapepe ya Gmail ili niweze kukuunganisha na Blogu
ya semina ya michanganuo uanze mara moja kujifunza na kuuliza maswali sambamba
na kupokea masomo hayo kupitia hiyo email.
Hii siyo semina ya kukosa hata kidogo ikiwa
wewe una dhamira ya dhati ya kujifunza michanganuo ya biashara, hii ni fursa
pekee na adimu kabisa ambayo unaweza usijekuipata tena, sisemi kwamba
hazitatokea tena semina nyingine kama hii hapana, bali hata kama zitatokea basi
inawezekana kabisa isije tena kutokea semina
ya namna hii kwa gharama ya chini kiasi hiki ambayo unahakikishiwa
kupata kile unachokihitaji katika muda ambao ni uelewa wako utakaoamua.
Wahi wakati huu, wiki mbili mpaka 4 ambazo
wakufunzi wako tumeamua kuacha kila kitu ili tukuhudumie wewe kikamilifu.
Kipindi hiki kikimalizika japo semina inaweza kuwa bado ipo lakini tutakuwa
hatuna tena muda mwingi wa kutosha kama sasa.
Mwisho nakushukuru sana kwa muda wako
ulionisikiliza hapa, naamini pia umekuwa ukifuatilia makala zetu katika blogu
hii kwa muda mrefu lakini sasa nakusihi, njoo tukuthibitishie kwa vitendo kile
tunachokifanya. Mwaka huu hakikisha unarudisha ama kudumisha ukuu wako, #Makeyourselfgreatagain,
#jirudishieukuuwakotena
Sikiliza makala hii katika SAUTI(MP3) Kwanini tunasema semia hii ni ya kipekee na haijawahi kutokea?
ASANTE SANA NA MUNGU AKUBARIKI
0 Response to "UTAMBULISHO RASMI WA SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA"
Post a Comment