Kwenye kipengele hiki cha Ongea na mshauri wa biashara, leo kuna msomaji mmja ambaye kama nilivyoahidi siwezi kutaja jina lake lakini huwa swali na majibu nayaweka hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali kusudi na wajasiriamali wengine nao waweze kunufaika na majibu ya swali hilo.
Msomaji wetu huyo aliuliza hivi;
"Ni jinsi gani nitaweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?"
Majibu.
Ngugu( ….), mradi wowote ule wa kiuchumi unaotengeneza faida ni biashara, na biashara zote duniani ni lazima zipitie mchakato utakaohusisha vipengele mbalimbali kama vile hatua ya wazo, utafiti kujua ikiwa wazo linalipa au la, mtaji na vyanzo vyake, kuanza biashara yenyewe, soko, ushindani, timu itakayofanya kazi na uongozi, maswala ya fedha nk.

Hatua zote hizo kwa
kifupi mtu unaweza ukazielezea kwenye kitu kinachoitwa mchanganuo au mpango wa
biashara, lakini pia kabla ya mpango wenyewe wa biashara ni lazima ufanye
utafiti wa soko lako na maswala yote yanayohusika na biashara hiyo ili
kuifahamu vizuri kabla haujaianza.
Na katika hatua hiyo ya mwanzo kabisa kabla hata haujaandika mpango wa biashara, unaweza kufanya tathmini nyepesi iitwayo, Mauzo yanayorudisha gharama zote(Brea even Analysis) inayokuwezesha kujua ikiwa mradi unaweza kukurudishia gharama utakazoweka na katika muda gani.

Kufanya utafiti wa
soko lako na kuandika mpango wa biashara kutakusaidia kupunguza hatari ya kuja
kufeli kwa biashara kwani utagundua makosa mengi kabla hata hujaanza ikiwa ni
pamoja na kujua ikiwa biashara itaweza kuleta faida ama la.
Kwa hiyo ndugu yangu (….),
mimi siwezi nikakutabiria ikiwa utapata faida au hutapata kwani sijafanya
utafiti wa biashara hiyo, ila ninaloweza kukuambia ni kwamba sekta ya kilimo na
hususani ukamuaji wa mafuta ya alizeti kama ulivyosema ni sekta ambayo ina
fursa kubwa bado na bila shaka ni biashara yenye faida. Mwelekeo wa
jamii(trend) kiujumla ni watu kupenda mafuta au vyakula visivyokuwa na lehemu
au mafuta ya mgando, wanahitaji mno mafuta ya mimea kama alizeti. Cha msingi
hapo ni wewe kuingia kwenye utafiti na hatimaye uandike mchanganuo hata ikiwa
siyo mchanganuo rasmi sana.
Na mchanganuo wenyewe
siyo lazima uuandike kwenye makaratasi au kompyuta, unaweza tu kuuhifadhi
katika kichwa chako, au pia kuna ‘option’ zingine kama vile kuandika kitu kinachoitwa,
MPANGO WA BIASHARA WA DAKIKA 15, au kwa jina jingine UKURASA MMOJA WA
MCHANGANUO.
Ikiwa utapenda
kufahamu zaidi namna ya kufanya utafiti wa biashara na jinsi ya kuandika
mchanganuo wa biashara iwe ni mchanganuo sanifu uliokamilika kila kitu au hata
ni ule 'simple' tu, kurasa moja au mbili kwa ajili ya kuthibitisha wazo la
biashara yako kama ni zuri au halifai, basi nakushauri kupata angalao moja kati
ya huduma zetu zifuatazo;
1. KUJIUNGA NA SEMINA
YA MICHANGANUO SH. 10,000/= AMBAPO UTAPEWA NA KITABU CHA BURE(SOFTCOPY) CHA
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI NA VITU VINGINE VINGI KAMA TEMPLATES
UTAKAZODOWNLOAD KUTOKA KWENYE BLOGU HII YA MICHANGANUO(itafunguka baada tu ya kulipia na kuunganishwa).
2. KUNUNUA KITABU CHA
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI CHA KARATASI HARDCOPY SH. 20,000/= AMBAPO
UTALETEWA KITABU MPAKA ULIPO MOJA KWA MOJA KAMA UPO DAR ES SALAAM NA KAMA UPO
MIKOANI TUTAKUTUMIA KWA BASI
3. KUNUNUA KITABU CHA
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI KATIKA MFUMO WA E-MAIL(PDF) SH.
10,000/= NA TUNAKUTUMIA HARAKA KWA EMAIL BAADA YA KUTUMA PESA NA ANUANI YAKO YA
EMAIL KATIKA NAMBA, 0712202244 AU 0765553030 ,JINA PETER AUGUSTINO
Ndugu yangu(…..)nadhani
mpaka hapo nitakuwa nimejitahidi kukupa majibu ya swali lako na ikiwa utakuwa
bado na maswali mengine unaweza kutuma kwa email, jifunzeujasiriamali@gmail.com
ASANTE
Peter A. Tarimo
0 Response to "JINSI GANI NAWEZA KUTENGENEZA PESA KWENYE MRADI WA MASHINE YA KUKAMUA MAFUTA YA ALIZETI?"
Post a Comment