Mchanganuo wa biashara ni mchanganyiko wa
maelezo na namba zinazowakilisha hesabu na taarifa mbalimbali. Tangu sehemu
zilizopita huko nyuma tulikwishaanza kuona baadhi ya hesabu kwa mfano katika
maelezo ya kampuni tuliona jedwali la vyanzo vya mahitaji kwa biashara mpya
pamoja na jedwali la hesabu za kipindi cha nyuma kwa biashara ya zamani.
Tuliona pia hesabu ya makisio ya mauzo, gharama za mauzo, gharama za uendeshaji
na jedwali la mishahara kwenye kipengele cha uongozi na wafanyakazi.
Katika kipengele hiki cha makisio ya fedha
ndipo unapotakiwa kuunganisha hesabu hizo nyingine ndogondogo zote na
kutengeneza makisio ya taarifa tatu muhimu ambazo ni, Faida na Hasara, Fedha
taslimu na Mizania ya biashara.
Kimsingi hesabu za mpango wa biashara ni
tofauti na hesabu halisi za kawaida za biashara kwani ni makisio, zinafanana tu
kimuundo. Kwa hiyo mtu hauhitaji kuwa mhasibu au mtaalamu wa biashara
aliyebobea ndipo uweze kukisia taarifa hizo ingawa pia mtu atahitajika kuwa na
uelewa wa msingi wa hesabu za biashara. Ikiwa unaandikampango wa biashara na
sehemu hii inakutatiza unaweza ukamtafuta mtaalamu akakusaidia eneo hili.
Tofauti nyingine ni kwamba, hakuna mtu
atakayeweza kukuwajibisha kisheria kwa kukisia mahesabu ya mpango wa biashara
yanayotofautiana na hesabu halisi lakini katika uhasibu unaweza hata kufungwa
jela kwa kuandika ripoti za hesabu zisizokuwa sahihi.
Makisio ya mpango wa biashara mara nyingi
huwa tofauti na hesabu halisi wakati wa kutekeleza mpango na unatakiwa uwe
unafanya mapitio kujua mpango wako wa biashara na hali halisi vimepishana kwa
kiasi gani na hivyo ufanye kitu gani zaidi kurekebisha.
Vipengele vidogo katika sehemu hii ni hivi
vifuatavyo,
7.1 Makisio muhimu
7.2 Mauzo yatakayorudisha gharama zote
7.3 Makisio ya Faida na Hasara
7.4 Makisio ya Fedha taslimu
7.5 Makisio ya Mali na madeni(Mizania ya
biashara)
7.6 Uwiano waSehemu muhimu za biashara
………………………………………………………………
Ndugu
msomaji, somo la kumi katika mfululizo wa masomo 11 linapatikana likiwa zima
katika blogu ya Masomo ya Semina ya Michanganuo ya biashara ambayo kiingilio
chake ni shilingi elfu 10 tu na unapewa kitabu cha michanganuo ya biashara na
ujasiriamali bure. Lipia kupitia namba za simu 0712202244 au
0765 553030 kisha tuma kwa meseji anuani yako ya e-mail(GMAIL) kwa ajili
ya kukuunganisha na blogu hiyo.
Unajifunza
masomo 11 ya jinsi ya kuandika Mchanganuo kamili wa biashara na ili kujua kama
umeelewa vizuri unaandika mpango mmoja wa biashara ambapo utakuwa ukipewa
usaidizi wowote ule utakaouhitaji kutoka kwa mkufunzi wa semina. Hakuna ukomo
wa semina ukishalipia, ni mpaka pale utakapoelewa.
· Ikiwa
unafanya biashara ya rejareja usikose kusoma kitabu hiki cha MAFANIKIO
YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA.
0 Response to "SOMO LA 10: MAKISIO YA FEDHA KWENYE MPANGO WA BIASHARA"
Post a Comment