Tathmini ya soko imegawanyika katika
vipengele vidogo kadhaa ambavyo vyote ili uweze kuviandika unahitaji kupata
takwimu na taarifa mbalimbali nje ya biashara yako zinazohusiana na soko au
wateja watarajiwa, sekta ya biashara uliyopo pamoja na ushindani.
Taarifa hizi na takwinu mbalimbali utaweza
kuzipata kupitia kufanya utafiti wa soko ambao unaweza kwenda moja kwa moja
kuwauliza wateja wanaonunua bidhaa/huduma kama unazotarajia kuuza au kwa njia
ya machapisho mbalimbali kutoka taasisi na vyombo vya habari kama vile
majarida, mtandao wa intaneti, maktaba, vituo vya kuwasaidia wajasiriamali,
wizara za serikali kama Wizara ya viwanda na biashara, ofisi au tovuti ya
takwimu ya Taifa nk.
Kwenye utafiti wako wa soko hakikisha
unawajua vizuri wateja wako, fahamu idadi yao na unaweza kujua idadi hiyo kwa
kuangalia katika takwimu mbalimbali kama za sensa ya watu na makazi au ofisi za
serikali za mitaa kama katika eneo lako kuna idadi ya watu wangapi, au kuna
biashara ngapi ambazo ndizo unategemea kuwa soko lako nk. Kwa mfano ikiwa wewe
biashara yako unatarajia kusambaza vifaa vya usafi mahospitalini na mashuleni,
nenda kaulize katika eneo hilo kuna jumla ya mashule na mahospitali mangapi?
Mbali na kufahamu idadi ya wateja wako pia
utatakiwa kufahamu mahitaji yao na ni kigezo kipi kinachowafanya wanunue. Ikiwa
ni mteja mmoja mmoja basi fahamu wastani wa umri wao, kipato chao, idadi ya
wanafamilia, na tabia zao za manunuzi zinazohusiana na biashara yako. Na
taarifa kama hizi unaweza kuzipata aidha kwa kuuliza watu moja kwa moja mitaani
au kwa kutumia machapisho na taarifa mbalimbali kama za sensa ya watu na
makazin nk. Utafiti wa soko umefafanuliwa vizuri kwenye kitabu cha Michanganuo
ya biashara na ujasiriamali uk. wa 20
Vipengele vidogo kwenye sehemu hii ya Soko ni
hivi vifuatavyo;
4.1 Mgawanyo wa soko
4.2 Mkakati wa soko lengwa
4.2.1 Mahitaji ya soko
4.2.2 Mwelekeo wa soko
4.2.3 Ukuaji wa soko
4.3 Tathmini ya sekta
4.3.1Washiriki katika sekta
4.3.2 Usambazaji ulivyo
4.3.3 Vigezo vya ushindani
4.3.4 Washindani wakuu
Ngugu
msomaji wa blogu hii huu ni utangulizi tu wa somo lenyewe la 7, ukitaka kusoma
somo zima na masomo mengine yote 10, jiunge na darasa hili la semina ya kuandika mpango wa biashara kwa kulipa shilingi elfu 10 kupitia namba
0712202244 au 0765 553030 jina ni “Peter
Augustino” kisha tuma na email yako ili kuunganishwa na blogu hii ya semina
hapa.
Ili
kufahamu huduma nyingine tunazotoa fungua ukurasa huu hapa.
0 Response to "SOMO LA 7: TATHMINI YA SOKO "
Post a Comment