5.0 MIKAKATI
NA UTEKELEZAJI.
Mikakati.
Mikakati ni malengo au vipaumbele vya
biashara yako ulivyochagua miongoni mwa vitu vingine vingi ili kuifanya
biashara hiyo iweze kuibuka kidedea kutoka washindani wengine wanaofanya
biashara kama ya kwako.
Unapoitazama biashara nzima kuna mambo/vitu
mbalimbali kama vile, bidhaa/huduma za aina mbalimbali, makundi tofauti ya
wateja, vyanzo mbalimbali vya mtaji, njia tofauti za kutangaza biashara, bei
tofauti, mauzo au kitu chochote kile kingine. Sasa hebu jiulize katika makundi
au aina ya vitu hivyo mbalimbali, ni kipi unachokipa kipaumbele zaidi kwenye biashara
yako?, na hicho ndicho kinachoweza kuwa moja kati ya mikakati yako.
Kabla hujaielezea mikakati ya biashara yako
kwanza unatakiwa ufahamu vizuri ni mahitaji gani ya wateja biashara yako
inayoyakidhi pamoja na sifa za kipekee huduma au bidhaa zako zilizokuwa nazo
ambazo bidhaa na huduma za washindani wako hazina.
Katika kipengele hiki cha mikakati, mwanzoni
kabisa kuna Sifa au nguvu za kiushindani, mkakati wa soko ambao chini yake
unabeba vitu vinne ambavyo ni bidhaa/huduma, bei, promosheni/matangazo na
usambazaji. Pia kuna mkakati wa mauzo ambao chini yake kuna makisio ya mauzo na
programu za mauzo. Mwisho kuna mkakati wa ushirikiano.
Kwa ujumla vipengele vidogo unavyoweza
kuvijumuisha katika sehemu yako hii nzima ya Mikakati na utekelezaji ni hivi
hapa chini halafu baadae tutavielezea kila kimoja. Ukumbuke pia kwamba siyo
sheria kwamba ni lazima mpango wako wa biashara ubebe kila kipengele kidogo
kilichoorodheshwa hapa, itategemea aina na malengo ya mchanganuo wako.
5.1 Sifa au Nguvu za kiushindani
5.2
Mkakati wa masoko
5.3.1 Kaulimbiu ya kujipanga katika soko
5.3.2 Mkakati wa bei.
5.3.3 Mkakati wa matangazo
5.3.4 Mkakati wa usambazaji
5.3.5 Programu za masoko
5.4 Mkakati
wa mauzo
5.4.1 Makisio ya mauzo
5.4.2 Programu za mauzo
5.5 Mkakati wa ushirikiano
5.7 Vitendo na Utekelezaji.
Anza kama kawaida na aya ya muhtasari wa sura
yako nzima ambayo huandikwa mwishoni baada ya kumaliza sura nzima, hii ina maana
kwamba unaacha wazi sehemu hiyo kwanza.
…………………………………………………………………
Somo
hili huu ni utangulizi tu, somo lenyewe zima pamoja na masomo mengine 10
unaweza kuyapata kiukamilifu baada ya kulipa ada ya Semina ambayo ni shilingi elfu
10, na kutuma email yako kwenye namba za simu
0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo.
Utapewa
pia bure kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali na cheti cha
kuhitimu semina ni wewe kuweza kuandika mwenyewe mpango wa biashara utakayoamua
huku ukipewa usaidizi wowote utakaohitaji na wakufunzi wa semina, mwisho wa
semina ni wewe kuelewa.
Kufahamu
zaidi juu ya huduma zinazotolewa na Self Help Books Tanzania tembelea ukurasa
huu wa HUDUMA ZETU
Kwa
ratiba nzima ya masomo ya semina hii bonyeza hapa palipoandikwa, ratiba yamasomo ya semina ya michanganuo
0 Response to "SOMO LA 8 SEMINA YA MICHANGANUO: MIKAKATI NA UTEKELEZAJI"
Post a Comment