UJUZI
MAALUMU
Uzoefu
Binafsi na Ushuhuda
(Hatua ya 4 kuelekea utajiri)
Kuna aina mbili za ujuzi(Maarifa), moja ni
ujuzi wa jumla na mwingine ni ujuzi maalumu. Ujuzi wa jumla pasipo kujali ni
mkubwa kiasi gani au ni mwingi kiasi gani, una matumizi kidogo sana katika
kujipatia pesa.
Vitengo katika vyuo vikuu vikubwa vinamiliki
kwa kiasi kikubwa karibu kila aina ya ujuzi wa jumla unaojulikana kwenye
ustaarabu. Wanabobea katika kufundisha maarifa, lakini hawabobei katika
kuyapanga au kuyatumia marifa(ujuzi)
Ujuzi
hautavuta pesa ikiwa kama hautapangiliwa na kuongozwa kwa akili kupitia mipango inayotekelezeka ya kivitendo kuelekea kwenye lengo lililokuwa dhahiri la kujichumia
pesa. Ukosefu wa ufahamu wa ukweli huu umekuwa chanzo cha mkanganyiko wa
mamilioni ya watu ambao huamini uwongo kwamba, “Ujuzi ni nguvu” Hakuna kitu
kama hicho. Ujuzi ni uwezekano tu wa nguvu ambayo bado haijadhihirika kuwa
nguvu halisi. Huwa nguvu tu pale ambapo na ikiwa itaratibiwa kwa mipango halisi
ya kivitendo kuelekea lengo lililokuwa dhahiri.
“Ukosefu wa kiungo” hiki katika mifumo yote
ya elimu inayojulikana kwenye ustaarabu leo unaweza kuonekana katika kushindwa
kwa taasisi za elimu kufundisha wanafunzi wao JINSI YA KUSIMAMIA NA KUTUMIA
UJUZI BAADA YA KUUPATA.
Watu wengi hufanya kosa la kudhani kwamba, kwasababu
Henry Ford alikuwa na “elimu ndogo”
basi yeye siyo mtu wa “elimu” Wale
wanaofanya kosa hili hawamjui Henry Ford, wala hawaelewi maana halisi ya neno
‘elimu’. Neno hilo limetoholewa kutoka Kilatini, ‘educo’ maana yake ni to “educe” “ kutoa kutoka ndani” au “kukua
kutokea ndani”
Mtu aliyeelimika siyo lazima awe ni yule
aliye na ujuzi mwingi wa jumla au maalumu. Watu walioelimika wamejenga vitivo
vya akili zao kusudi ziweze kupokea kitu chochote wanachotaka, au ni sawa na
kusema, pasipo kuingilia haki za watu wengine. Henry Ford ni mfano mzuri anafaa
zaidi kwenye maana ya huu ufafanuzi.
Wakati wa vita kuu ya kwanza ya Dunia, gazeti
moja la Chicago lilichapisha tahariri fulani ambazo miongoni mwa kauli
nyingine, Henry Ford aliitwa, “Mpinga vita mjinga” Bwana Ford alipinga kauli
hizo na kufungua kesi dhidi ya gazeti kwa kumkashifu. Wakati kesi ikizungumzwa
mahakamani,wakili wa lile gazeti alitoa ushahidi na kumuweka Bwana Ford
mwenyewe katika upande wa ushahidi kwa lengo la kuithibitishia mahakama kwamba
alikuwa mjinga. Bwana Ford aliulizwa maswali kama ifuatavyo,
“Benedict Arnold alikuwa nani?”
“Ni wanajeshi wangapi waliotumwa na Uingereza
kwenda kuzima uasi wa mwaka 1776?”
Akijibu swali la mwisho Bwana Ford alisema,
“Siijui idadi kamili ya wanajeshi Uingereza
iliyotuma, lakini nimesikia kwamba ilikuwa ni idadi kubwa kushinda idadi ya
wale waliorudi”
Mwishowe, Bwana Ford alichoka na huu msururu
wa maswali. Katika kujibu swali hilo la uchokozi, aliegama akamnyooshea kidole
wakili ambaye alikuwa amemuuliza lile swali na kusema,
“Ikiwa kama kweli ningetaka kujibu swali la kijinga ambalo umetoka kuuliza, au
maswali mengine yeyote ambayo umekuwa ukiniuliza, ngoja nikukumbushe kwamba
nina mstari wa vitufe vya umeme vya
kubonyeza juu ya dawati langu, na kwa kubofya kitufe sahihi, naweza nikaita
msaada wa watu wanaoweza wakajibu swali lolote
ninalotamani kuuliza kuhusiana na biashara ambayo naelekeza nguvu zangu nyingi.
Sasa tafadhali unaweza kutuambia kwanini
nihangaike kuichanganya akili yangu kwa maarifa ya jumla, kwa lengo la kuweza
kujibu maswali, wakati ninao watu wanaonizunguka wanaoweza kunipa ujuzi wowote
ninaouhitaji?
Hapo bila shaka kulikuwa na mantiki kwa jibu
hilo.
Jibu lile lilimshinda wakili, kila mtu kwenye
chumba cha mahakama alitambua lilikuwa ni jibu siyo la mtu mjinga, bali la mtu
mwenye elimu(msomi). Mtu yeyote aliyeelimika ni yule anayefahamu pa kupata
maarifa anapoyahitaji, na jinsi ya kuyapangilia hayo maarifa katika mipango
dhahiri ya kivitendo kupitia msaada wa “Kundi lake la kushauriana”(Mastermind Group). Henry Ford alikuwa
ana mamlaka na ujuzi maalumu wote aliouhitaji kumfanya kuweza kuwa mmoja kati
ya watu matajiri zaidi Marekani. Haikuwa muhimu kwamba alikuwa na maarifa hayo
katika akili yake mwenyewe. Ukweli hamna mtu mwenye mwelekeo wa kutosha na
akili kusoma kitabu cha aina hii anaweza kutoona umuhimu wa mfano huu.
Kabla hujaweza kuwa na uhakika wa uwezo wako
wa kubadilisha shauku kuwa katika
kiwango chake cha fedha kinacholingana nayo, utahitaji ujuzi maalumu wa huduma, bidhaa au utaalamu unaokusudia kuutoa kwa
ajili ya kupata utajiri. Pengine
unaweza ukahitaji ujuzi maalumu zaidi kuliko vile ulivyokuwa na uwezo au mwelekeo wa kuupata,
na kama hili litakuwa kweli, unaweza ukauziba udhaifu wako kupitia msaada wa
kundi lako la kushauriana(Mastermind group)
Andrew Carnegie alisema kwamba, yeye mwenyewe
hakuwa anajua kitu kuhusiana na maswala ya kiufundi ya biashara ya chuma cha
pua, zaidi ya hapo hakujisumbua kabisa kujua kitu chochote kuhusiana nayo.
Ujuzi maalumu aliouhitaji kwa ajili ya kuzalisha na kuuza chuma cha pua
aliupata kutoka kwa mtu mmoja mmoja katika kundi lake la kushauriana(Master
mind group)
Ulimbikizaji wa utajiri mkubwa huhitaji nguvu na nguvu hupatikana kupitia ujuzi
maalumu uliopangiliwa vizuri na kuongozwa kwa akili, lakini ujuzi huo siyo
lazima uwe ni mali ya yule mwenye kulimbikiza huo utajiri.
Aya iliyotangulia inapaswa kutoa matumaini na
ari kwa mtu mwenye nia ya kupata utajiri ambaye hakuweza kupata “elimu” ya
kutosha ya kutoa huo ujuzi maalumu kama unavyohitajika. Watu wakati mwingine huumia
maishani kutokana na “hali ya kutokujiamini” kwasababu hawakupata elimu rasmi.
Mtu mwenye uwezo wa kuunganisha na kuongoza
“kundi la watu wenye kushauriana”(Mastermind group) wenye ujuzi unaoweza
ukatumika katika kulimbikiza utajiri(pesa), mtu huyo anahesabika kuwa na elimu
sawa tu na mtu mwingine yeyote yule katika kundi hilo. Kumbuka hili kama
unakabiliwa na hisia za kutokujiamini kutokana na kutokupata elimu ya kutosha.
Inalipa
Kufahamu Jinsi ya Kununua Ujuzi
Kwanza kabisa, amua juu ya aina ya ujuzi
maalumu unaouhitaji na lengo la kuhitaji ujuzi huo. Kwa kiasi kikubwa lengo
lako kuu maishani, lengo unalofanya kazi kulifikia, itasaidia kutambua ni ujuzi
gani unaohitaji. Swali hili likiwa limeshapata majibu, kazi yako nyingine
inahitaji kwamba una taarifa sahihi kulingana na vyanzo vya kuaminika vya
maarifa. Vyanzo muhimu zaidi kati ya hivyo ni;
a) Uzoefu
na elimu ya mtu mwenyewe
b) Uzoefu
na elimu vinavyopatikana kupitia ushirikiano na wengine
c) Vyuo
na vyuo vikuu
d) Maktaba
za umma(kupitia vitabu na majarida ambamo unaweza ukapatikana ujuzi wote
uliokusanywa na ustaarabu
e) Kozi
maalumu za mafunzo(kupitia madarasa ya jioni na zaidi mafunzo kwa njia ya
posta.
Kadiri ujuzi unavyopatikana, ni lazima
upangiliwe na kutumiwa kwa ajili ya lengo lililokuwa wazi kupitia mipango
inayotekelezeka. Ujuzi hauna thamani isipokuwa ule unaoweza kupatikana kutokana
na matumizi yake katika jambo lenye manufaa. Hii ni sababu moja kwanini shahada
za vyuo vikuu haziwezi kuwa hakikisho la ajira zenye mafanikio.
Kama utafikiria kuchukua masomo ya ziada,
kwanza tambua lengo linalokufanya utake ujuzi unaoutafuta, halafu jifunze ni
wapi aina hiyo ya ujuzi(maarifa) inapoweza kupatikana kutoka vyanzo vinavyoaminika.
Watu wenye mafanikio, katika nyanja zote kamwe hawaachi kujifunza ujuzi maalumu
unaohusiana na lengo lao kuu, biashara au taaluma. Wale wasiokuwa na mafanikio,
kwa kawaida hufanya kosa la kuamini kwamba kipindi cha kujiongezea maarifa
huishia wanapomaliza shule. Ukweli ni kwamba shule haifanyi chochote zaidi ya
kumuelekeza mtu jinsi ya kupata maarifa ya kivitendo.
Nidhamu
binafsi mtu anayopata kutokana na programu dhahiri ya mafunzo maalumu huwa
kiasi hicho kutokana na fursa iliyopotezwa wakati ujuzi ulipokuwa ukipatikana
bila gharama. Njia ya mafunzo ya nyumbani ya kufundisha sanasana hufaa kwa
mahitaji ya watu walioajiriwa ambao hukuta baada ya kumaliza shule ni lazima
wapate ujuzi maalumu wa ziada, lakini hawawezi wakapata muda wa kurudi tena
shuleni. Mabadiliko endelevu ya hali ya kiuchumi katika jamii yetu
yamesababisha maelfu ya watu kutafuta kipato cha ziada au vyanzo vipya vya
kipato. Kwa waliokuwa wengi suluhisho la matatizo yao huweza kupatikana kwa
njia ya kujipatia ujuzi maalumu.
Wengi watalazimika kubadilisha shughuli zao
kabisa. Mfanyabiashara atakapokuta kwamba aina fulani ya bidhaa haiuziki, kwa
kawaida ataibadilisha na bidhaa nyingine inayohitajika zaidi.Watu ambao
biashara zao ni zile za kutafuta soko la huduma zao ni lazima pia wawe wafanyabiashara
hodari. Kama huduma zao hazileti mapato ya kutosha katika shughuli moja, ni
lazima wahamie kwa nyingine ambapo fursa pana zaidi zinapatikana.
Watu wanaoacha kujifunza kwasababu tu
wamemaliza shule, daima wataangamia kwenye umasikini bila ya matumaini
pasipokujali wanafanya kazi gani. Nija ya mafanikio ni njia ya kutafuta maarifa
bila kukoma. Hebu tuangalie tukio la kipekee…
.................................................................................................
Ndugu msomaji mfululizo wa sehemu za kitabu hiki sasa tutakuwa tukikuletea kila siku ya Jumatatu na Alhamisi, tafadhali usikose mpaka mwisho wa kitabu.
.................................................................................................
Ndugu msomaji mfululizo wa sehemu za kitabu hiki sasa tutakuwa tukikuletea kila siku ya Jumatatu na Alhamisi, tafadhali usikose mpaka mwisho wa kitabu.
0 Response to "WASOMI NA WATU WENYE MAFANIKIO HAWAACHI KUJIFUNZA MAARIFA MAPYA-HENRY FORD"
Post a Comment