Ikiwa wewe ni mmoja wa wale
wanaoamini kwamba utajiri unaweza kupatikana tu kwa kitendo cha watu
wanaojikusanya wenyewe katika makundi na kudai malipo zaidi kwa huduma
kidogo, ikiwa wewe ni mmoja wa wale wanaodai msaada wa Serikali bila adha
za asubuhi na mapema wakati pesa zinapoingia kwako, ikiwa wewe ni mmoja wa wale
wanaoamini katika kuuza kura zao kwa wanasiasa kwa malipo ya kupitisha sheria
zinazoruhusu kupora hazina ya umma, unaweza ukatulia bila bughudha katika imani
yako kwa utambuzi kuwa hakuna mtu atakayekuhangaisha kwa sababu hii ni nchi huru ambapo kila mtu anaweza
akafikiri kama atakavyo, ambapo karibu kila mtu anaweza akaishi kwa juhudi
kidogo, ambapo wengi wanaweza kuishi vizuri bila ya kufanya kazi yeyote.
Hata hivyo unapaswa kutambua
ukweli mzima kuhusu uhuru huu ambao
watu wengi kiasi hicho hujivunia na wachache kiasi hicho kuutambua. Mkubwa kama
ulivyokuwa, mbali kama unavyofika, faida nyingi kama unavyoweza kutoa, hauleti na wala hauwezi kuleta utajiri bila
jitihada
Ipo, lakini njia moja ya
kutegemewa ya kupata na kushikilia
utajiri kihalali, na hiyo ni kwa kutoa huduma zenye thamani. Hakuna mfumo
uliowahi kuundwa ambao watu wanaweza kisheria kupata utajiri kupitia nguvu ya
namba yao tu peke yake, au bila ya kutoa kama malipo thamani iliyokuwa sawa ya
aina moja ama nyingine.
Kuna kanuni ijulikanayo kama
Sheria ya uchumi, hii ni zaidi ya
nadharia. Ni kanuni mtu yeyote hawezi kuipinga. Tia alama vizuri jina la kanuni
hii na ikumbukwe kwasababu ina nguvu zaidi kushinda wanasiasa wote na mifumo ya
kisiasa. Ipo juu na zaidi ya udhibiti wa vyama vya wafanyakazi. Haiwezi
ikayumbishwa au kuhongwa na wapigadili au viongozi waliojichagua wenyewe katika
tasnia yeyote.
Zaidi ina vyote, jicho la kuona na mfumo kamili wa hesabu za biashara ambao
unatunza hesabu sahihi za miamala ya binadamu wote wanaojihusisha katika
biashara ya kujaribu kupata pasipo kutoa. Muda wowote wakaguzi wake huja kuangalia
kumbukumbu za watu zote kubwana ndogo na kudai hesabu.
‘Biashara kubwa’, ‘ulanguzi’
au jina lolote lile unalochagua kuupa mfumo uliotupatia uhuru, unawakilisha kundi la watu wanaofahamu, kuheshimu na
kujifungamanisha wenyewe na hii sheria ya uchumi yenye nguvu. Uendelevu wao wa
kiuchumi hutegemea kuheshimu kwao hii sheria.
Kumbuka pia kwamba hii
ndiyo, lakini mwanzo wa vyanzo vilivyokuwepo kwa ajili ya ulimbikizaji wa
utajiri. Ni kiasi kidogo tu cha vitu vya anasa na vitu visivyokuwa muhimu
vilivyotajwa. Lakini kumbuka kwamba biashara ya kuzalisha, kusafirisha na
kutafuta soko la hizi bidhaa chache hutoa ajira ya kawaida kwa mamilioni ya
wanaume na wanawake wanaolipwa kwa huduma zao milioni nyingi za dolla kwa mwezi na kuzitumia kwa uhuru katika
vitu vyote, vya anasa na mahitaji muhimu
ya lazima.
Sanasana kumbuka kwamba nyuma
ya ubadilishanaji wote huu wa bidhaa na
huduma binafsi unaweza kupatikana wingi wa fursa
za kujikusanyia utajiri. Hapa uhuru
wetu unatusaidia. Hakuna kitu chochote kitakachokuzuia wala mtu yeyote
kushiriki katika nafasi yeyote ya juhudi zinazohitajika kufanya hizi biashara. Ikiwa
mtu atakuwa na kipaji cha kipekee, mafunzo au uzoefu, mtu huyo anaweza
kujilimbikizia utajiri kwa kisi kikubwa . Wale wasiokuwa na bahati wanaweza
kujilimbikizia utajiri kiasi kidogo. Mtu yeyote anaweza kuendesha maisha kwa
malipo ya kiasi kidogo sana cha nguvu kazi.
Kwa hiyo, hivyo ndivyo
ilivyo!
Fursa zimetandaza bidhaa
zake mbele yako. Songa mbele chagua kile unachotaka , tengeneza mpango wako,
uweke mpango katika vitendo na
uufuatilie kwa uvumilivu. Jamii ya Kibepari itafanya yaliyobakia.
Unaweza ukategemea sana
katika hili, - JAMII YA KIBEPARI INAMHAKIKISHIA KILA MTU FURSA YA KUTOA HUDUMA
ZENYE THAMANI NA KUKUSANYA UTAJIRI KULINGANA NA THAMANI YA HUDUMA HIYO.
Mfumo huo haumnyimi mtu haki
hiyo, lakini hautoi ahadi wala hauwezi kuahidi kitu fulani bure. Sheria ya
uchumi yenyewe isiyobadilika hudhibiti mfumo huu, kwamba hautambui wala
kuvumilia kwa muda mrefu kupata pasipo
kutoa. Sheria ya uchumi ilipitishwa na ASILI! Hakuna mahakama ambayo
wavunjaji wa sheria hii wanaweza kukata rufaa. Sheria hutoa vyote viwili,
penati kwa uvunjifu wake na malipo
stahiki kwa utekelezaji wake bila
kuingiliwa au uwezekano wa kuingiliwa na binadamu yeyote.
Sheria hii haiwezi
kubadilishwa. Haibadiliki, ipo palepale kama nyota katika mbingu na huwajibika
kwa, na ni sehemu ya mfumo unaoziongoza nyota.
Mtu anaweza kukataa mwenyewe
kutii sheria ya uchumi?
Bila shaka! Hii ni jamii
huru ambapo wote huzaliwa na haki sawa, ikiwemo haki ya kutokutii sheria ya
uchumi.
Halafu ni kitu gani hufuata?
Vizuri, hakitatokea kitu
mpaka idadi kubwa ya watu wameunganisha nguvu kutamka wazi lengo la kuipuuza
sheria hii na kuchukua kile wakitakacho
kwa nguvu. Kisha huja dikteta, akiwa na vikosi vilivyojipanga vizuri na bunduki
za rashasha!.
Hatujafikia bado hatua hiyo,
lakini tumejifunza vyote tunavyotaka kujua kuhusu jinsi mfumo huu unavyofanya
kazi. Labda tutakuwa na bahati ya kutosha kutokutaka uzoefu binafsi wa ukweli
unaotisha. Bila shaka tutachagua kuendelea na uhuru wetu wa kusema, uhuru
wa vitendo, na uhuru wa kutoa huduma zenye thamani kwa malipo ya utajiri.
Matokeo haya hayapatikani
katika uzoefu wa muda mfupi. Ni matokeo ya miaka 25 ya uchanganuzi makini wa
njia za watu waliofanikiwa zaidi na watu wasiofanikiwa zaidi Marekani iliopata
kuwajua.
............................................................................................................................
Mpenzi msomaji unayefuatilia tafsiri
hii, na huo ndio mwisho wa Sura ya saba ya kitabu hiki, tafadhali nakusihi
usikose mwanzo wa sura mpya ya 8 siku ya Jumatatu.
Pia zile semina zetu kwa mwaka huu za
miradi yenye ubunifu itakayoboresha mizunguko yetu ya fedha, bado hazijaanza na
pindi zitakapoanza tutakujulisha, kama hukutuma namba yako ya Whatsapp tuma kwa namba 0765553030, muda
umebaki mchache sana.
Kupata vitabu bora kabisa vya biashara na ujasiriamali tembelea, SMART BOOKS TANZANIA.
0 Response to "FURSA ZIPO, CHAGUA UTAKACHO,TENGENEZA MPANGO, TEKELEZA NA KUFUATILIA KWA UVUMILIVU UTAFANIKIWA"
Post a Comment