SURA YA 8
MAAMUZI
Kiboko ya Kusitasita
(Hatua
ya 7 kuelekea utajiri)
Uchanganuzi sahihi wa
wanaume na wanawake zaidi ya 25,000 ambao walipata uzoefu wa kuanguka walisema
ukweli kwamba ukosefu
wa maamuzi ulikuwa karibu na mwanzo wa orodha ya sababu kuu 30 za kuanguka.
Hii siyo kauli ya kinadharia tu – ni ukweli kuahirisha
au kinyume cha maamuzi ni adui wa wote ambaye karibu kila mtu ni lazima amshinde.
Utakuwa na fursa ya kujaribu
uwezo wako wa kufikia maamuzi kamili na yaharaka wakati utakapomaliza kusoma
kitabu hiki na kuwa tayari kuanza kutia katika vitendo kanuni kinachoelezea.
Uchunguzi wa mamia ya watu waliojikusanyia utajiri zaidi ya dola milioni moja
walifichua ukweli kwamba kila mmoja wao alikuwa na tabia ya kufikia maamui haraka na ya
kuyabadilisha hayo maamuzi polepole
ikiwa waliyabadilisha.
Watu walioshindwa
kujikusanyia utajiri, bila ya kisingizio, walikuwa na tabia ya kufikia maamuzi
ikiwa waliyafikia, polepole sana na kuyabadilisha maamuzi hayo haraka na kila
mara.
Moja ya sifa bora zaidi ya
Henry Ford ilikuwa ni tabia yake ya kufikia maamuzi haraka na kwa ukamilifu, na
kuyabadilisha taratibu. Sifa hii ilivuma sana kwa Bwana Ford kiasi kwamba
ilimpa hadhi ya kuitwa mbishi sugu. Ilikuwa ni tabia hii iliyomchochea Bwana
Ford kuendelea kuzalisha gari lake maarufu Model ‘T’(gari baya zaidi duniani),
wakati washauri wake wote na wengi wa wateja wa gari hilo walikuwa wakimshauri
kulibadilisha.
Pengine Bwana Ford
alichelewa sana kufanya mabadiliko, lakini upande mwingine wa shilingi ni
kwamba msimamo wa maamuzi ya Bwana Ford ulizaa utajiri mkubwa kabla ya
mabadiliko katika Model T hayajafanyika.Yapo mashaka kakini kidogo sana kwamba tabia
ya Ford katika msimamo wa kufanya uamuzi ilimfanya adhaniwe kuwa ni mkaidi,
lakini tabia hii ni hitaji katika kufikia maamuzi taratibu na uharaka katia
kuyabadilisha.
Wengi wa watu wanaoshindwa
kujipatia pesa za kutosha kwa mahitaji yao kwa ujumla huathiriwa kirahisi na
maoni ya wengine. Huruhusu magazeti na majirani wambea ‘kufikiria’ badala yao.
‘Maoni’ ndiyo bidhaa rahisi zaidi hapa duniani. Kila mtu ana lundo la maoni
tayari kumpatia mtu yeyote atakayeyakubali. Kama unaathiria na ‘maoni’
unapofikia maamuzi, hautafanikiwa katika shughuli yeyote, na zaidi katika kazi
ya kugeuza shauku yako mwenyewe kuwa
pesa.
Ikiwa unaathiriwa na maoni
ya wengine, hautakuwa na hamu ya maoni yako mwenyewe.
Tunza ushauri wako mwenyewe
wakati utakapoanza kutia katika vitendo kanuni zilizoelezwa hapa kwa kufikia
maamuzi yako mwenyewe na kuyafuata. Usimshirikishe yeyote isipokuwa wanachama
wa kundi lako la kushauriana(Master Mind Group), na uhakikishe katika uchaguzi wako wa kundi
hili, unachagua wale tu watakaokuwa katika huruma kamili na mapatano na lengo lako
Marafiki wa karibu na ndugu
wakati hawadhamirii kufanya hivyo, mara nyingi humlemaza mtu kupitia “maoni” na
wakati mwingine kupitia mzaha ambao unamaanisha kuwa ucheshi, maelfu ya wanaume
na wanawake hubeba hali ya kutojiamini maisha yao yote kwa sababu baadhi ya watu wenye maana
nzuri lakini wajinga waliharibu kujiamini kwao kupitia ‘maoni’ au mzaha.
Una ubongo na akili yako
mwenyewe. Uitumie na kufikia maamuzi yako mwenyewe. Ikiwa unahitaji ukweli ama
taarifa kutoka kwa watu wengine kukuwezesha kufikia maamuzi bila shaka kama
utakavyofanya mara nyingi, jipatie ukweli huo au tafuta taarifa unazohitaji
kimyakimya bila kufichua lengo lako.
Ni tabia ya watu walio na
ujuzi kidogo au wa bandia kujaribu kutoa taswira kwamba wana ujuzi mkubwa. Watu
hao kwa ujumla huongea sana na
kusikiliza kidogo sana. Fungua macho yako na masikio na kuufunga mdomo wako ikiwa unataka kuwa na tabia ya kufanya maamuzi
haraka. Wale wanaozungumza kupita kiasi, hawafanyi kitu kingine chochote. Ikiwa
unazungumza zaidi kuliko unavyosikiliza, hujinyimi tu mwenyewe fursa nyingi za
kujipatia ujuzi wenye manufaa, lakini pia unafichua mipango yako na malengo kwa watu watakaofurahia mno kukushinda,
kwasababu wanakuonea wivu.
Kumbuka pia kwamba kila wakati
unapofungua mdomo wako mbele ya mtu mwenye ujuzi mwingi, unafunua kwa huyo mtu
akiba yako kamili ya maarifa! Busara halisi kwa kawaida huonekana kupitia staha
na ukimya. Kumbuka ukweli kwamba kila mtu unayekutana naye ni kama wewe
mwenyewe, anatafuta fursa ya kujipatia pesa. Ikiwa utazungumzia kuhusu mipango
yako kwa uwazi mno, unaweza kuja kushangaa utakapokuta kwamba watu wengine wamekuzidi kete lengo lako kwa kuweka
katika vitendo kabla yako mipango
uliyozungumza bila tahadhari.
Acha moja kati ya uamuzi
wako wa kwanza kuwa ni kufunga mdomo
na kufungua macho na masikio. Kama
kumbukumbu kwako mwenyewe kufuata
ushauri huu, itapendeza ikiwa utanakili usemi ufuatao katika herufi kubwa na
uuweke mahali utakapouona kila siku:
IAMBIE
DUNIA KILE UNACHOPANGA KUFANYA, LAKINI KWANZA KIONYESHE.
Hii ni sawa na kusema
kwamba, “Vitendo na wala siyo maneno ndivyo vyenye maana zaidi”
Uhuru au Kifo Katika Maamuzi
Thamani ya maamuzi hutegemea
ujasiri unaohitajika kuyafanya. Maamuzi makubwa yaliyotumika kama msingi wa
ustaarabu yalifikiwa kwa kuchukua hatari kubwa ambayo mara nyingi ilimaanisha
uwezekano wa kifo.
Uamuzi wa Lincoln wa kutoa
tamko lake mashuhuri la Uhuru, lililotoa uhuru kwa watu wa Marekani,
ulichukuliwa kwa utambuzi kamili kwamba kitendo chake kingeliweza kuwafanya
maelfu ya marafiki na wafuasi wake kisiasa kumgeuka. Alfahamu pia kwamba kutoa
tangazo lile kungeweza kumaanisha vifo kwa maelfu ya watu katika uwanja wa
mapambano. Mwishowe, ulimgharimu Lincoln maisha yake. Hilo lilihitaji ujasiri.
Uamuzi wa Socrate wa kunywa
kikombe cha sumu kuliko kwenda kinyume na imani yake binafsi ulikuwa ni uamuzi
wa kijasiri, uligeuza muda mbele miaka elfu moja na kuwapa watu ambao hawakuwa
wamezaliwa bado, haki ya uhuru wa kufikiri na wa kuongea.
Uamuzi wa Generali Robert E.
Lee alipojitenga na Muungano na kuchukua uelekeo wa Kusini ilikuwa ni moja ya
ujasiri kwani alifahamu vizuri kuwa ungeliweza kugharimu maisha ya wengine.
Lakini uamuzi mkubwa wa wakati wote, kwa kadri raia yeyote yule wa Marekani anavyohusika,
ulifikiwa Philadelphia mnamo tarehe 4 Julai 1776, wakati watu 56 walipotia
saini majina yao kwenye andiko ambalo walifahamu vizuri lingeweza kuleta uhuru
kwa Wamarekani wote, au kuacha kila mmoja kati ya hao 56 wakinyongwa vitanzini.
Umewahi kusikia juu ya
andiko hili maarufu, lakini unaweza kuwa hujapata kutoka kwake somo kubwa
katika mafanikio binafsi liliyofunza dhahiri.
Sote tunakumbuka tarehe ya
uamuzi huu muhimu sana, lakini wachache wetu tunatambua ni ujasiri kiasi gani
uamuzi huo ulihitaji. Tunatambua historia kama ilivyofundishwa, tunakumbuka
tarehe na majina ya watu waliopigana, tunakumbuka Valley Forge na Yorktown,
tunawakumbuka George Washington na Lord Cornwallis. Lakini tunakumbuka machache
kuhusiana na nguvu halisi nyuma ya majina haya, tarehe na sehemu.
Bado tunafahamu kidogo juu
ya nguvu isiyoshikika, iliyohakikisha uhuru kwa Wamarekani zamani kabla majeshi
ya Washington kufika mji wa Yorktown.
Tunasoma historia ya
mapinduzi na kudhania uwongo kwamba George Washington alikuwa Baba wa Marekani,
kwamba ni yeye aliyewaletea Wamarekani uhuru wao. Ukweli ni kwamba Washington
alikuwa kiungo tu baada ya ukweli, kwasababu ushindi kwa majeshi yake ulikuwa
umehakikishwa kitambo kabla Lord Cornwallis hajajisalimisha. Hili halikusudii
kumnyang’anya Washington utukufu wowote anaostahili. Lengo lake badala yake ni
kutoa usikivu mkubwa kwa nguvu ya
kushangaza iliyokuwa sababu ya kweli ya ushindi wake.
Ilikuwa ni kama janga kwamba
waandishi wa historia wameruka kabisa hata kumbukumbu kidogo kwa nguvu hii isiyoshindwa iliyozaaa na kutoa
uhuru kwa Taifa lililokusudia kuweka vipimo vipya vya Uhuru kwa watu wote wa Dunia.
Nasema ni janga kwasababu ni nguvu ileile ambayo ni lazima itumike na kila mtu anayeshinda
magumu ya maisha, na kulazimisha maisha kulipa gharama iliyodaiwa.
0 Response to "IJUE BIDHAA YA BEI RAHISI KULIKO ZOTE DUNIANI, KILA MTU ANAMILIKI LUNDO!"
Post a Comment