Ni watu wengi hawafahamu, kilichojificha kuhusiana na
ufugaji wa kuku wa asili au wa kienyeji, wanabakia tu kuvutiwa na kushawishika
kwamba kuku wa kienyeji wanalipa, kuku wa kienyeji wana soko kubwa, kuku wa
kienyeji nyama yake ni tamu sana na ukitaka kudhibitisha hilo, hebu pata supu
ya kuku wa kienyeji ujionee mwenyewe nk.
Lakini kabla sijakwenda kukudondolea hicho kilichomo
nyuma ya pazia hilo zito, siwezi kujizuia kukuibia siri japo kidogo tu juu ya
yale yanayoendelea kujiri katika darasa letu la Michanganuo ya biashara
linaloendelea kwenye whatsapp sambamba na blogu yetu maalumu ya michanganuo na
kwa njia ya email pia. Nji zote hizo zinatumika kwani kila mtu huamua menyewe
njia yake inayomfaa zaidi.
Ikiwa ni siku ya pili jana, kuna jambo moja
lilinishangaza sana, kilichonishangaza ni mwanachama mmoja kutoa wazo kuwa wale
wanaopendelea wajitambulishe wao, biashara ama shughuli zao na ni wapi
wanapatikana kwa malengo ya kufahamiana zaidi na hata ikiwezekana kuja kushirikishana
baadae fursa mbalimbali za kimasoko kwa bidhaa ama huduma wanazozitoa. Kwa
asiyependa kujitambulisha uhuru wake uliheshimiwa.
Kwa kweli sikutegemea kumbe asilimia kubwa ya watu licha
ya kuwa wana taaluma zao mbalimbali kama, vile Ualimu, Uuguzi, Udaktari, IT,
Wanahabari, Wajasiriamali, na hata Wanasheria pia walikuwa na kitu cha pamoja
ambacho aidha ni wafugaji wa kuku au walio na shauku ‘interest’ na masuala ya
ufugaji wa kuku.
Sikuamini hata kidogo, lakini nikakumbuka kwamba katika
matangazo ya semina hiyo mwanzoni tulitangaza kuwa mwezi Januari tutakuwa na
semina ya kujadili mchanganuo bunifu wa kipekee unaohusiana na kuku ila ‘hatukuspecify’
kufafanua kama ni sekta ipi ya kuku, kuku wa mayai, kuku wa nyama, wa kienyeji
au wa kisasa.
Ukweli nilistaajabu pamoja na kwamba wapo wengine pia
waliojiunga na semina hii kwa nia ya kujifunza namna ya kuandaa mpango wa
biashara, na wale pia waliojiunga kwa lengo la kujifunza mbinu mbalimbali za
kuboresha mzunguko wa fedha binafsi na katika biashara zao.
Tukirudi katika mada yetu ya leo, Kilicho nyuma ya pazia, ufugaji wa
kuku wa asili au wa kienyeji ukipenda, kumekuwa na masimulizi mengi
sana juu ya miradi ya kuku hawa wanaofugwa na karibu kila familia nchini
Tanzania, chini ya jangwa la Sahara na Afrika kwa ujumla.
Kiukweli kuku hawa wana faida nyingi kiufugaji lakini siyo
faida kibiashara, tofautisha hapo, ‘faida kiufugaji na faida kibiashara’ .
Unapotaja faida kiufugaji maana yake ni kwamba kuku hawa ni rahisi sana
kuwafuga kwa sababu kwanza hawaumwi umwi ovyo kama walivyokuwa wenzao wa
kisasa, hujitafutia vyakula wenyewe, hulishwa madawa kidogo sana hivyo nyama
yake na mayai havina kemikali nyingi, supu yake ni tamu sana na iliyo na ladha
maridhawa, ni wakakamavu nk. Sasa sababu nilizozitaja kwa kiasi kikubwa ndizo
huwafanya watu wengi kiasi hicho kuvutiwa na suala la ufugaji wa kuku wa
kienyeji.
Lakini nyuma ya pazia, kibiashara kuku hawa ni mtihani
mkubwa endapo hawatafugwa katika mfumo huria, nikimaanisha kuku wa kienyeji
kuachiwa wazurure ili kujitafutia chakula wenyewe. Nyuma ya pazia vile vile
kuku hawa kibiashara ni janga hasa utakapoamua kuwafungia ndani kama wafugaji
wengi wa Dar es salaam wanafyofanya kutokana na ufinyu wa maeneo. Kule Singida,
Morogoro na hata Mikoa ya kusini na Kanda ya ziwa kama Ruvuma, Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mbeya sina shaka
sana nao kwani maeneo ni makubwa.
Nyuma ya pazia kuku wa kienyeji utagaji wake ni wa
kustaajabisha, kuku anaweza akataga mayai 45 mpaka 60 tu kwa mwaka mzima wakati
dada zao wa kisasa hufikisha mpaka mayai 300 kwa mwaka, sasa hebu niambie ikiwa
umeamua kuwafuga kwa lengo la kuuza mayai hapo utafanyaje?
Lakini habari njema ni kwamba pamoja na sababu zote hizo nyuma
ya pazia, lipo suluhisho. Kuku hawa watamu haiwezekani zikakosekana mbinu za
kuwafanya wawe na faida kibiashara nyakati hizi za sayansi na teknolojia.
Hakuna lisilowezekana chini ya jua, kama Wamarekani waliweza kukanyaga ardhi ya
mwezi tunaouona mamilioni ya maili juu angani, sembuse kukifanya kitoweo hiki
kitamu namna hii kiweze kuwa na tija?
Hakuna tena sababu ya wafugaji wa kuku wa kienyeji kuwa
na mashaka, sijui, oo… kuku wangu wakitotoa mwewe, vicheche na mapaka
hunibakizia viwili tu kati ya 15, sijui kuku wangu wa kienyeji hufa ovyo ovyo,
sijui kuku wangu wa kienyeji akitaga jumapili ni mpaka jumapili nyingine tena
ndio utaokota yai bandani nk.
Peter A. Tarimo kwa ushirikiano na kundi lake la
kushauriana(Master mind Group) la kampuni ya self help, kama alivyogundua ile
Kanuni nyingine mashuhuri uliyoisoma
katika kitabu cha “SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO” safari hii
amekuja na ugunduzi mwingine wa teknolojia mbili rahisi, ambazo zitakuwa
muarobaini wa matatizo yote yaliyo nyuma ya pazia katika ufugaji wa kuku hawa
wa asili.
Ndani ya Mpango kamili wa Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji,
teknolojia au mbinu hizi 2 zinatambulishwa kwa mara ya kwanza kabisa Tanzania
kukabiliana na matatizo hayo.
Hazipo mahali pengine popote pale, ni mpya, kama huamini
wewe njoo, ukikuta ni za uwongo niumbue mbele za kadamnasi. Sina kawaida ya
kusema uwongo.
Ikiwa utapenda kujiunga na mpango huu ni rahisi sana,
siyo lazima uwe kwenye Whatsapp ingawa pia ukiwa huko ni vizuri kwani mafunzo
haya tunayatoa kupitia njia kuu 3 tofauti, Whatsapp, kwa email na
kwenye blogu maalumu ya michanganuo ya biashara ambapo huwa tunaweka
kumbukumbu na masomo yote ya semina kwa ajili ya wale washiriki wapya au wale
wa zamani watakapo kufanya marejeo ya vitu vya nyuma.
KUJIUNGA,
Tuma anuani yako ya GMAIL, isiwe
yahoo wala aina nyinginezo, Namba yako ya Whatsapp
kama upo whatsapp, kama haupo huko hamna shida utapata mafunzo kama kawaida.
Kiingilio ambacho ni Tsh. Elfu 10
kupitia namba za simu 0712202244 au 0765553030. Jina ni Peter Augustino Tarimo
Vitabu vya self help books pia vyote vinapatikana
softcopy na hardcopy.
0 Response to "KILICHOKUWA NYUMA YA PAZIA, UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI(KUKU WA ASILI)."
Post a Comment