Jitathmini
wewe Mwenyewe
Maswali
28 Unayopaswa Kujibu
Tathmini ya mwaka ni
muhimu katika kutafuta soko la huduma kikamilifu kama ilivyokuwa katika
tathmini ya mwaka kwa bidhaa. Na zaidi, tathmini ya mwaka inatakiwa ibainishe
kupungua kwa makosa na kuongezeka kwa mema. Mtu husonga mbele, kusimama pale
alipo au kurudi nyuma katika maisha. Lengo la mtu linapaswa bila shaka liwe ni
kusonga mbele. Tathmini ya mwaka itabainisha ikiwa hatua imepigwa, na kama
hivyo ndivyo, ni kwa kiasi gani. Itabainisha pia hatua zozote zilizopigwa
kurudi nyuma mtu anazoweza kuwa amepiga.Utafutaji kikamilifu wa soko la huduma
humtaka mtu kupiga hatua hata kama maendeleo ni ya taratibu.
Tathmini yako ya
mwaka inapaswa kufanywa mwishoni mwa kila mwaka kusudi uweze kujumuisha katika
maazimio yako ya mwaka mpya maboresho yeyote ambayo tathmini inaonyesha
yanatakiwa kufanywa. Fanya tathmini hii kwa kujiuliza mwenyewe maswali
yafuatayo na kuhakikisha usahihi wa majibu yako kwa msaada wa mtu mwingine
ambaye hatakuruhusu kujidanganya mwenyewe.
Maswali ya tathmini binafsi
kwa ajili ya kujichunguza.
1. Nimetimiza kile nilichoazimia
kama lengo langu kwa mwaka huu?(Unapaswa kufanya kazi na lengo la mwaka
lililokuwa dhahiri litakalotimizwa kama sehemu ya lengo lako kubwa la maisha .
2. Nimetoa huduma
katika ubora wa hali ya juu kabisa
ambao nilikuwa na uwezo nao au ningeliweza kuboresha zaidi sehemu yeyote ya
huduma hizi?
3. Nimetoa huduma kwa kiasi kikubwa kadiri inavyowezekana
nilichokuwa na uwezo nacho?
4. Dhamira ya matendo
yangu imekuwa linganifu na shirikishi muda wote?
5. Nimeruhusu tabia
ya kuahirisha kupunguza ufanisi
wangu, na kama ndiyo ni kwa kiasi gani?
6. Nimeboresha haiba yangu, na kama ndiyo ni kwa njia
zipi?
7. Nimekuwa na msimamo katika kufuatilia mipango yangu?
8. Nimefikia maamuzi mara moja na kwa ukamilifu
katika matukio yote?
9. Nimeruhusu hofu
yeyote au zaidi ya zile hofu sita za msingi (angalia sura ya 15), kupunguza
ufanisi wangu?
10. Nimekuwa aidha
muangalifu kupita kiasi au muangalifu chini ya kiasi?
11. Uhusiano wangu na
wenzangu kazini umekuwa mzuri au mbaya ? kama umekuwa mbaya, kosa ni la kwangu
kwa sehemu au ni la kwangu lote?
12. Nimetawanya nguvu
zangu zozote kupitia kukosa umakini wa kukusanya nguvu sehemu moja?
13. Nimekuwa muelewa
na mvumilivu katika mambo yote?
14. Ni katika njia
ipi nimeboresha uwezo wangu wa kutoa huduma?
15. Nimekuwa mlafi
katika tabia zangu zozote?
16. Nimejieleza aidha
kwa uwazi au kwa siri, aina yeyote ya majivuno?
17. Matendo yangu kwa
wenzangu yamekuwa ni ya kuwashawishi kuniheshimu?
18. Maoni yangu na
maamuzi yamekuwa yakizingatia utabiri au usahihi wa tathmini na fikra?
19. Nimekuwa
nikifuata tabia ya kuweka bajeti ya muda wangu, matumizi yangu, na kipato
changu na nimekuwa nikizilinda bajeti hizi?
20.Ni muda kisi gani
nimepoteza katika juhudi zisizokuwa na faida, ambao ningeliweza kuutumia kwa
faida zaidi?
21. Nawezaje kubajeti upya muda angu na kubadilisha
tabia zangu kusudi niwe na ufanisi zaidi katika mwaka unaokuja?
22. Nimekuwa na hatia
ya tendo lolote ambalo halikupitishwa na dhamira yangu?
23. Ni kwa njia zipi
nimetoa huduma bora na nyingi zaidi kuliko nilivyolipwa?
24. Sijatenda haki
kwa mtu yeyote, na ikiwa ndiyo ni kwa namna gani?
25. Ikiwa ningekuwa
mnunuzi wa huduma zangu mwenyewe kwa mwaka mzima, ningeliweza kuridhika na
ununuzi wangu ?
26. Mnunuzi wa huduma
zangu anaridhika na huduma nilizotoa, na kama siyo, kwanini siyo?
27. Nipo kwenye
shughuli sahihi, na kama siyo ni kwanini?
28. Kiwango changu
katika kanuni za msingi za mafanikio ni kipi?(fanya tathmini hii bila upendeleo
kwa ukweli, na mpe mtu mwingine aipitie ambaye ni jasiri vya kutosha kuifanya
kwa usahihi).
Baada ya kusoma na
kushika taarifa zilizomo humu kwenye hii sura, sasa upo tayari kutengeneza
mpango wa kivitendo kwa ajili ya
kutafuta soko la huduma zako. Wale waliopoteza mali zao na wale ambao
ndio kwanza wanaanza kutafuta pesa, hawana chochote isipokuwa kuzitoa huduma
zao kwa malipo ya utajiri. Kwa hiyo ni muhimu kwamba wanazo tayari taarifa za
kivitendo zinazohitajika kutafuta soko
la huduma zao kwa faida nzuri kabisa.
Taarifa zilizomo
katika sura hizi zitakuwa za manufaa makubwa kwa wale wote wanaotamani kushika
uongozi katika nyanja yeyote. Itakuwa msaada hasahasa kwa wale wanaolenga
kutafuta soko la huduma zao kama biashara au watendaji wakuu wa viwanda.
Kushiriki moja kwa
moja na kuelewa juu ya taarifa zilizoelezwa hapa kutakuwa msaada katika
kutafuta soko la huduma za mtu, na pia kutamsaidia mtu kuwa mchanganuzi na
mwenye uwezo wa kuhoji watu. Taarifa zitakuwa na thamani isiyopimika kwa wakuu
wa utumishi, mameneja utumishi na watendaji wengine wenye majukumu ya kuchagua
wafanyakazi na ya kutunza ufanisi wa taasisi. Kama una mashaka na kauli hii,
ufanyie uhakiki kwa kujibu katika maandishi maswali 28 ya kujitathmini binafsi.
Kwa kweli , hilo linaweza kuwa jambo la kuvutia na wakati huhuo lenye faida
hata kama hautilii mashaka ukamilifu wa kauli hiyo.
Wapi na ni kwa jinsi gani
Unaweza kupata Fursa za kupata Utajiri
Sasa tayari
tumechanganua kanuni ambazo utajiri unaweza kupatikana, kwa asili tunauliza
hivi, “ Ni wapi mtu anaweza kupata fursa zinazofaa kutumia hizi kanuni?” Vizuri
sana, ngoja tufanye uchunguzi na kuona ni nini uchumi wa Kimagharibi unaweza
kumpa mtu anayetafuta utajiri mkubwa au mdogo.
Kwa kuanza, tukumbuke
sote kwamba tunaishi katika jamii ambamo kila raia mwema anafurahia uhuru wa
mawazo na uhuru wa vitendo. Wengi wetu hatujawahi kamwe kuchunguza faida za
uhuru huu. Hatujawahi kuulinganisha uhuru wetu usiokuwa na mipaka na uhuru
uliominywa katika baadhi ya jamii nyingine.
Hapa tuna uhuru wa
mawazo, uhuru wa kuchagua na kufurahia elimu, uhuru katika dini, uhuru katika
siasa, uhuru katika uchaguzi wa biashara, taaluma au kazi, uhuru wa
kujikusanyia na kumiliki bila kunyanganywa mali zote tunazoweza kukusanya,
uhuru wa kuchagua sehemu zetu za kuishi, uhuru katika ndoa, uhuru kupitia fursa
sawa kwa makabila yote, uhuru wa kusafiri, uhuru katika uchaguzi wetu wa
vyakula na uhuru wa kulenga kwenye hatua
yeyote maishani ambayo tumejiandaa wenyewe. Tuna aina nyingine za uhuru,
lakini orodha hii itatoa mtazamo wa jumla wa juu (mtazamo wa jicho la ndege)
muhimu zaidi ambao unajumuisha fursa ya kiwango cha hali ya juu kabisa.
Kisha ngoja tuhesabu
tena baadhi ya baraka ambazo uhuru wetu mpana umeweka mikononi mwetu. Chukua
familia ya kawaida katika jamii ya Kimagharibi kwa mfano(maana yake familia ya
kipato cha kawaida) na jumuisha faida zinazopatikana kwa kila mwanafamilia.
· CHAKULA.
Kutokana na uhuru wetu kwa watu wote familia ya kawaida mpaka mlamgoni mwake
inao uchaguzi wa chakula, na katika bei iliyo ndani ya uwezo wake kiuchumi.
· MALAZI. Familia hii huishi katika nyumba bora, iliyo
na gesi kwa ajili ya kupasha joto, umeme, pamoja na gesi kwa ajili ya kupikia.
Mkate kwa ajili ya kifungua kinywa umeokwa kwenye jiko la umeme, kapeti husafishwa
kwa mashine(vacuum cleaner) inayoendeshwa kwa umeme. Maji ya moto na ya baridi
yanapatikana muda wote jikoni na bafuni. Chakula huhifadhiwa na baridi katika
jokofu linaloendeshwa kwa umeme. Mke hutengeneza nywele zake, kufua nguo zake
na kuzinyoosha kwa pasi ya umeme iliyo rahisi kutumia kwenye nguvu ya umeme
inayopatikana kwa kupachika plagi ukutani. Mume hunyoa ndevu kwa kutumia
mashine ya umeme. Wanapata burudani kutoka pande zote za dunia, masaa 24 kwa
siku ikiwa watataka, kwa kitendo cha kuwasha tu luninga zao.
· MAVAZI.
Wanaume na wanawake katika jamii za Kimagharibi wanaweza kupata mahitaji yao ya
mavazi na kuvaa bila wasiwasi kwa bei mshahara wa familia ya kawaida unaoweza
kumudu.
Ni mahitaji ya msingi matatu
tu ya chakula, mavazi na malazi yaliyotajwa. Raia wa kawaida anazo stahili
zingine na faida anazopata kwa malipo ya jitihada za wastani zisizozidi masaa
manane kwa siku ya kazi. Miongoni mwake ni stahili ya kumiliki gari, ambalo mtu
anaweza akatoka na kurudi kwa hiyari yake kwa gharama kidogo sana.
……………………………………………
Ndugu
msomaji usikose sehemu ya sita ya sura hii ya 7 siku ya Jumatatu.
Pia niombe radhi kwa kutotimiza uzinduzi wa kundi la Whatsapp la semina za michanganuo
pamoja na semina yenyewe ya kuchanganua miradi ya kiubunifu iliyokuwa na uwezo mkubwa
wa kuzalisha faida haraka kama nilivyoahidi.
Sababu kubwa ni maandalizi ya group
lenyewe lakini karibu litakamilika naomba tuvute subira kidogo kwa wale waliokwisha
jiunga. Kwa wale ambao bado hawajajiunga nafasi bado ipo wazi KARIBUNI SANA! Tuma
ujumbe wa “NIUNGANISHE KUNDI LA WASAP SEMINA ZA MICHANGANUO” namba yetu wassap ni
0765553030
Wahi pia offa ya vitabu vitatu 3 vya self help books katika mfumo wa softcopy kwa bei ya sh 15,000/= badala ya elfu 18,000/= kabla haijamalizika tarehe 10 mwezi huu. Tuma pesa kwenye 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo utatumiwa vitabu muda huohuo.
0 Response to "MAAJABU YALIYOLETA BARAKA ZOTE HIZI KATIKA UCHUMI WA KIMAGHARIBI"
Post a Comment