Maajabu Yaliyoleta Baraka
Hizi
Nikiwa sina agenda ya
siri wala kinyongo cha kuelezea, na bila ya dhamira ya moyoni, nina bahati ya
kuchambua kwa uwazi maajabu hayo yasiyoshikika, kitu kinachochanganya sana ambacho hutupatia baraka hizo
zilizotangulia kutajwa, fursa za kukusanya utajiri na uhuru wa kila aina.
Ninayo haki ya
kuchambua chanzo na asili ya hii nguvu
isiyoonekana kwasababu nafahamu na nimekuwa nikifahamu kwa zaidi ya robo
karne wengi wa watu ambao walitumia nguvu hiyo na wengi ambao sasa wanahusika
kuiendeleza. Jina la mfadhili huyu wa ajabu ni MTAJI. Mtaji hauhusishi pesa tu
peke yake, lakini zaidi sanasana ni makundi ya watu waliojipanga vizuri sana, ambao hupanga njia
na namna ya kutumia pesa kwa ufanisi kwa manufaa ya jamii na kwa faida yao
wenyewe.
Makundi hayo
hujumuisha wanasayansi, waelimishaji, wafamasia, wagunduzi, wataalamu wa
biashara, wataalamu wa mahusiano ya jamii, wataalamu wa usafirishaji, wahasibu,
wanasheria, madaktari na wote manaume na wanawake waliokuwa na ujuzi wa kipekee
sana katika nyanja zote za viwanda na biashara.
Huongoza, kufanya majaribio, na kuweka alama katika nyanja mpya za ubunifu. Wanasaidia vyuo, mahospitali na shule, kujenga barabara nzuri, kuchapisha magazeti, kulipa nyingi ya gharama za serikali na kulinda mahitaji mengi makubwa na madogo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.
Huongoza, kufanya majaribio, na kuweka alama katika nyanja mpya za ubunifu. Wanasaidia vyuo, mahospitali na shule, kujenga barabara nzuri, kuchapisha magazeti, kulipa nyingi ya gharama za serikali na kulinda mahitaji mengi makubwa na madogo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.
Kwa kifupi Mabepari
ndio vichwa vya ustaarabu kwa sababu ndio huweka mfumo mzima uliobeba elimu
yote, mwangaza na maendeleo ya binadamu. Pesa bila akili mara zote ni hatari.
Ikiwa zitatumika vizuri, ni nyenzo muhimu zaidi ya ustaarabu.
Kifungua kinywa
rahisi kwa familia katika jiji huwa na juisi ya chungwa, nafaka, mayai, mkate
na siagi na chai yenye sukari. Kisingeliweza kutolewa kwa bei inayolipika ikiwa
kama mtaji uliopangiliwa haukutolewa kwa kiwanda, kwenye meli, katika reli na
kwa jeshi la watu waliofunzwa kuviendesha. Unaweza kupata picha kidogo juu ya
umuhimu wa mtaji uliopangiliwa kwa
kujaribu kufikiria wewe mwenyewe kama uliye na mzigo wa jukumu la kukusanya na
kutoa kifungua kinywa rahisi kwa familia ya mjini iliyotajwa hapo juu pasipo
msaada wa mtaji.
Kupata chai ungepaswa
kufanya safari ya China au India. Ikiwa kama wewe siyo muogeleaji mahiri, ungeliweza
kuchoka hata kabla ya kwenda na kurudi. Halafu tatizo jingine lingeweza kukukumba.
Ungeliweza kutumia nini badala ya pesa hata kama ungelikuwa imara kuogelea
baharini?
Kupata sukari
ungepaswa kuogelea umbali mwingine mrefu kwenda visiwa vya Caribbean, au
matembezi marefu kwenda mashamba ya viazi sukari. Lakini hata hivyo ungeliweza
kurudi bila sukari kwasababu jitihada zilizopangiliwa na pesa ni muhimu
kuzalisha sukari, bila kusema chochote juu ya kinachohitajika kusafisha,
kusafirisha na kuifikisha kwenye meza ya kifungua kinywa.
Mayai ungeweza
kuyapata kirahisi vya kutosha lakini ungeweza kutembea umbali mrefu sana kabla
hujaweza kupata glasi mbili za juisi ya chungwa. Ungepaswa kutembea umbali mwingine
mrefu mpaka kwenye mashamba yanayolimwa ngano kupata vipande viwili vya mkate
wa ngano. Nafaka ingeliweza kuondolewa
kutoka kwenye menyu kwasababu isingeweza kupatikana isipokuwa kwa kutumia nguvu
za ushirika wa watu waliofunzwa na mfumo unaofaa, vyote vikihitaji mtaji.
Wakati ukiwa
umepumzika, ungeweza kuanza safari nyingine ya kuogelea kushuka chini kuelekea
Amerika ya Kusini ambapo ungeweza kuchukua ndizi kadhaa na wakati ukirudi
ungeliweza kutembea kidogo kuelekea shamba la ng’ombe wa maziwa na kuchukua
siagi na jibini kidogo. Hatimaye familia yako jijini ingeliweza kuwa tayari
kuketi chini na kufurahia kifungua kinywa.
Inaonekana kama
upuuzi, au siyo?
Vizuri, njia
iliyoelezwa ndiyo ambayo ingeliweza kuwa
njia pekee inayowezekana bidhaa hizo rahisi za chakula kuweza kupatikana
katikati ya jiji ikiwa hatukuwa na mfumo wa Kibepari.
Jumla ya pesa
zilizohitajika kwa ajili ya kujengea, kuendeleza reli na meli zilizotumika
katika usafirishaji wa kifungua kinywa hicho rahisi ni nyingi kiasi cha
kuduwaza akili ya mtu. Hufikia mamia ya mamilioni ya dola bila ya kutaja jeshi la wafanyakazi wenye ujuzi waliohitajika
kuendesha meli na treni hizo. Lakini usafirishaji ni sehemu tu ya mahitaji ya
ustaarabu wa kisasa.
Kabla hakujaweza kuwa
na kitu chochote cha kusafirisha, kitu fulani ni lazima kipandwe ardhini
kwanza, au kuzalishwa na kutayarishwa kwa ajili ya soko. Hii huhitaji mamilioni
ya dola zaidi kwa ajili ya vifaa, mitambo, ufungashaji, masoko, na kwa ajili ya
mishahara ya mamilioni ya wanaume na wanawake. Meli na barabara za garimoshi
havimei tu kutoka ardhini na kufanya kazi moja kwa moja. Huja baada ya mwito wa
ustaarabu, kupitia nguvukazi na uadilifu na uwezo wa kupangilia wa watu walio
na ubunifu, imani, shauku, maamuzi na
uvumilivu! Watu hawa hujulikana kama
mabepari(Wajasiriamali). Wanatiwa ari
kwa shauku ya kujenga, kutengeneza, kutimiza, kutoa huduma zenye manufaa,
kupata faida na kukusanya utajiri. Na kwasababu wanatoa huduma ambazo bila hizo kusingelikuwa na ustaarabu,
wanajiweka wenyewe katika njia ya utajiri mkubwa.
Kuweka tu kumbukumbu
kwa urahisi na zinazoeleweka, nitaongeza kwamba hawa mabepari(wajasiriamali)
ndio watu walewale ambao wengi wetu tumesikia wasemaji kwenye majukwaa
wakiwataja. Ni watu walewale ambao wenye misimamo mikali, walanguzi, wanasiasa
wasio waaminifu na viongozi wa vyama vya wafanyakazi huwaita “Wanyang’anyi”
Sijaribu kutetea au
kupinga kundi lolote la watu au mfumo wowote wa kiuchumi. Sijaribu kushutumu
majadiliano ya jumla pale ninapotaja ‘Viongozi wa ushirika’ wala sina lengo la kuwapatia
hati safi watu wote waitwao mabepari.
Lengo la kitabu hiki
– lengo ambalo kwa uaminifu nimejitolea zaidi ya robo karne nikiwasilisha kwa
wale wote wanaotaka maarifa, filosofia ya kutegemewa zaidi ambayo kupitia hiyo
watu wanaweza kupata utajiri kwa kiasi chochote kile wanachotamani.
Hapa nimechanganua
faida za kiuchumi za mfumo wa kibepari kwa malengo mawili ya kuonyesha,
1. Kwamba
wote wale wanaotafuta utajiri ni lazima watambue na kuendana wenyewe na mfumo
unaodhibiti njia zote za utajiri uwe mkubwa au mdogo na
2. Kwamba
ni lazima wawe upande wa picha kinyume na ule unaoonyeshwa na wanasiasa na
wafitini ambao huchukulia kupangilia mtaji kana kwamba ni kitu chenye sumu.
............................................................................
Ndugu msomaji wa tafsiri ya kitabu hiki cha Think & Grow Rich(Fikiri Utajirike), usikose sehemu ya mwisho ya Sura hii ya 7 siku ya Alhamisi. Pia ikiwa hukutuma namba yako kwa ajili ya kujiunga na kundi la Whatsapp la Semina za michanganuo ya biashara za kipekee mwaka huu, basi bado hujachelewa tuma ujumbe kwa whatsapp, namba 0765553030 ukisema 'NIUNGANISHE NA KUNDI LA WASSAP LA MICHANGANUO'
0 Response to "PESA BILA AKILI NI HATARI, NI NYENZO KUBWA YA MAFANIKIO IKITUMIKA VIZURI"
Post a Comment