Wakoloni walichukia watu
wenye silaha kuandamana mbele yao. Watu walianza kuonyesha chuki yao wazi,
wakivurumisha mawe pamoja na maneno kwa wanajeshi waliokuwa wakitembea, mpaka
ofisa mwenye amri alipoamrisha, “Kaza singe…..Chomeka!
Mapambano yalianza. Yalizaa
vifo na majeruhi wengi. Tukio liliamsha chuki kiasi kwamba Baraza la
jimbo(lililoundwa na wakoloni mashuhuri) liliitisha mkutano kwa lengo la
kuchukua hatua madhubuti zinazostahili. Wawili kati ya wanachama wa Baraza hilo
walikuwa ni John Hancock na Samuel Adams. Walizungumza kwa ujasiri na kutangaza
kwamba hatua ni lazima ichukuliwe kuondoa wanajeshi wote wa Uingereza kutoka
Boston.
Kumbuka huu- uamuzi, katika
akili ya watu wawili, ungeweza vizuri kuitwa mwanzo wa uhuru ambao Wamarekani
sasa wanaufurahia. Kumbuka pia kwamba uamuzi
wa watu hawa wawili ulihitaji imani
na ujasiri, kwasababu ulikuwa hatari.
Kabla ya Baraza kuahirishwa,
Samuel Adams alichaguliwa kumuona Gavana wa jimbo, Huchinson, na kutaka
kuondolewa kwa vikosi vya majeshi ya Uingereza. Ombi lilikubaliwa na vikosi
viliondolewa kutoka Boston, lakini tukio halikufikia tamati. Lilikuwa
linasababisha hali iliyotaka kubadilisha mwenendo mzima wa ustaarabu.
Ajabu, siyo kwamba ni ukubwa
kiasi gani wa mabadiliko kama yale ya Mapinduzi ya Marekani na vita vingine
vingi mara kwa mara vilivyo na mianzo yao katika mazingira yanayoonekana kuwa siyo
muhimu?. Inavutia pia kuona kwamba mabadiliko haya muhimu mara nyingi huanza
katika hali ya uamuzi dhahiri katika
akili za idadi ndogo sana ya watu.
Wachache wetu tunafahamu historia
ya Marekani vizuri vyakutosha kutambua kwamba John Hancock, Samuel Adams na
Richard Henry Lee(wa jimbo la Virginia) walikuwa mababa wa kweli wan chi.
Richard Henry Lee alikuwa
kigezo muhimu katika simulizi hii kutokana na sababu kwamba yeye na Samuel
Adams waliwasiliana mara kwa mara(kwa maandishi), walibadilishana kwa uhuru,
wasiwasi na matumaini yao kuhusiana na masilahi ya watu wa jimbo lao. Kutokana
na kitendo hiki, Adams alipata wazo kuwa mabadilishano ya pamoja ya barua kati
ya makoloni 13 yanaweza kusaidia kuleta uratibu wa nguvu iliyohitajika sana
kuhusiana na suluhisho la matatizo yao.
Mnamo Machi 1772, miaka
miwili baada ya makabiliano na wanajeshi Boston, Adams aliliwasilisha wazo
hili kwenye baraza katika mfumo wa hoja
kwamba kamati ya Uhusiano ianzishwe ikiwa na wajumbe kamili waliochaguliwa
katika kila koloni “kwa lengo la ushirikiano wa kirafiki kwa manufaa ya
makoloni ya Uingereza Marekani”
Zingatia vizuri tukio hili!
Ulikuwa ni mwanzo wa muungano wa nguvu
kubwa sana iliyohitajika kutoa uhuru kwa Wamarekani. Ushirika tayari ulikuwa
umekwishaundwa, ulimjumuisha Adams, Lee na Hancock. Kamati ya Mahusiano iliundwa.
Shuhudia kwamba kitendo hiki kilitoa njia ya kuongeza nguvu ya ushirika kwa
kuongeza watu kutoka makoloni yote. Zingatia kwamba utaratibu huu ulibeba
mpango madhubuti wa kwanza kabisa wa wakoloni waliokuwa wamegadhabika
Katika Umoja kuna nguvu!
Wananchi wa Makoloni walikuwa wamepigana
vita isiyokuwa rasmi dhidi ya Wanajeshi wa Uingereza kupitia matukio
yanayofanana na maandamano ya Boston lakini hakukuwa na la maana lililotimizwa.
Malalamiko yao mmojammoja hayakuwa yameunganishwa chini ya ushirika mmoja.
Hakukuwa na kundi la watu walioweka mioyo yao, akili, roho na mwili pamoja
katika uamuzi mmoja kamili kusuluhisha matatizo yao na Waingereza mara moja na
daima, mpaka pale Adams, Hancock na Lee walipokuja kukaa pamoja.
Wakati huohuo Waingereza
hawakuwa wamekaa kimya, wao pia walikuwa wakipanga mipango na kushirikiana
katika mambo yao wenyewe wakiwa na faida ya kuwa na pesa pamoja na jeshi
thabiti nyuma yao.
Ufalme ulimteua Gage
kuchukua nafasi ya Hutchinson kama Gavana wa Massachusetts. Moja kati ya
vitendo vya mwanzo vya Gavana ilikuwa ni kutuma ujumbe kumwambia Samuel Adams
kwa lengo la kujaribu kuzima upinzani wake kwa hofu. Tunaweza kuelewa vizuri
zaidi kiini cha kile kilichotokea kwa kunukuu mazungumzo kati ya Kanali
Fenton(mjumbe aliyetumwa na Gage) na Adams.
Kanali
Fenton: ‘Nimeruhusiwa na Gavana Gage kukuhakikishia wewe Bwana Adams, kwamba Gavana amepewa uwezo wa
kukutunukia zawadi kadiri itakavyofaa(akijaribu kumshawishi Adams kwa ahadi ya
hongo) kwa masharti kwamba uingie katika
kuzima upinzani wako kwa amri za serikali. Ni ushauri wa Gavana kwako Bwana,
kutokusababisha maudhi zaidi kwa Mheshimiwa. Mwenendo wako unakufanya uwajibike
kwa adhabu za kuvunja sheria ya Mfalme Henry viii, ambayo mtu anaweza kupelekwa
Uingereza kwa mashitaka ya Uhaini au kuficha kosa la uhaini kwa mamlaka ya
Gavana wa jimbo. Lakini kwa kubadilisha muelekeo wako kisiasa, siyo tu utapata
faida kubwa binafsi, lakini utatengeneza amani yako na mfalme!”
Samuel Adams alikuwa na
uchaguzi wa maamuzi mawili, angeweza kusitisha upinzani wake na kupata hongo
binafsi, au angeliweza kuendelea na kuwa
katika hatari ya kunyongwa!
Ukweli, muda ulikuwa umefika
wa Adams kulazimika kufikia mara moja uamuzi ambao ungeweza kuyagharimu maisha
yake. Wengi wa watu wangeliweza kuona ni vigumu kufikia uamuzi wa namna hiyo. Wengi
wangeweza kurudisha jibu la kukwepakwepa, lakini siyo Adams! Alimsisitizia Kanali
Fenton kumfikishia Gavana jibu kamili kama Adams alivyolitoa kwake.
Jibu
la Adams lilikuwa hivi; ‘Hivyo unaweza kumwambia Gavana Gage kuwa
natumaini ni muda mrefu tangu nifanye amani yangu na Mfalme wa Wafalme. Hakuna sababu
binafsi zitakazonisukuma mimi kuachana na mkondo wa maadili ya nchi yangu. Na mwambie
Gavana Gage ni ushauri wa Samuel Adams kwake,
aache kutukana hisia za watu waliogadhabishwa.’
Mpenzi
msomaji, usikose sehemu ya 3 ya sura hii ya 8 siku ya Jumatatu, pia zile semina
za michanganuo ya biashara bunifu kwa mwaka huu zinaanza rasmi kesho Ijumaa
katika darasa letu la mtandaoni kupitia Blogu maalumu, email na Whatsapp, ikiwa
bado hujatuma namba yako ya wassap fanya hivyo hujachelewa, usisahau pia kutoa
ada yako sh. 10,000/=. Namba zetu ni 0712202244
Whatsapp, 0765553030
0 Response to "UAMUZI HATARI WA KUSHANGAZA ULIO CHANZO CHA UHURU WA TAIFA LA MAREKANI"
Post a Comment