Mwishowe baada ya siku
kadhaa za malumbano alisimama tena na kutamka kwa sauti thabiti iliyoeleweka.
“Bwana Rais tumejadili suala hili kwa siku kadhaa sasa. Ipo njia moja tu sisi
kuifuata. Kwanini sasa Mheshimiwa tunachelewa zaidi? Kwanini basi tulumbane?
Acha siku hii njema izae Jamhuri ya Amerika. Iache iinuke, na siyo kuteketea na
kutwaa kwa nguvu, bali kuanzisha upya utawala wa amani na wa kisheria. Macho ya
Ulaya yanatutazama sisi. Inataka kutoka kwetu mfano hai wa uhuru ambao unaweza
kuthibitisha tofauti katika furaha kuu ya mwananchi kwa uonevu unaozidi
kuongezeka.”
Kabla hoja yake mwishowe
haijapigiwa kura, Lee aliitwa kurudi Virginia kutokana na sababu nzito ya
kuuguliwa katika familia. Lakini kabla hajaondoka aliacha madaraka mikononi mwa
rafiki yake, Thomas Jefferson ambaye aliahidi kupigana mpaka hatua zinazofaa
zimechukuliwa. Muda mfupi baadae Rais wa Baraza (Hanckoc) alimchagua Jefferson
kama Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaaa tangazo la Uhuru.
Kwa udi na uvumba Kamati ililifanyia
kazi andiko ambalo lingeweza kumaanisha
wakati litakapokubaliwa na Baraza
kwamba, KILA MTU ALIYESAINI, INGELIWEZA KUWA ANASAINI HATI YAKE MWENYEWE YA
KIFO ikiwa makoloni yangeshindwa katika mapambano na Uingereza kitu ambacho
kilikuwa dhahiri kutokea.
Andiko liliandikwa na mnamo
tarehe 28 June rasimu ya awali ilisomwa mbele ya baraza. Kwa siku kadhaa
ilijadiliwa, kubadilishwa na kuwa tayari. Mnamo tarehe 4 Julai 1776, Thomas
Jefferson alisimama mbele ya baraza na bila ya woga akasoma uamuzi wa maana
zaidi kuwahi kuwekwa kwenye karatasi.
“Katika mwenendo wa matukio
ya binadamu ni muhimu kwa watu fulani kukata utepe wa kisiasa ambao
umewaunganisha pamoja na kuchukulia miongoni mwa tawala za dunia, kituo sawa na
kinachojitegemea ambacho sheria za asili, na za Mungu wa asili aliwapa, heshima
nzuri kwa maoni ya wanadamu huhitaji kwamba wanapaswa kutangaza sababu
inayowasukuma kwenye utengano…”
Jefferson alipomaliza,
mswada ulipigiwa kura, ukakubaliwa na kutiwa saini na watu 56, kila mmoja
akihatarisha maisha yake juu ya uamuzi
wake wa kuandika jina lake. Kwa uamuzi huo, lilizaliwa Taifa lililokusudia
kumletea binadamu daima upendeleo wa kufanya maamuzi. Kwa maamuzi
yanayofanywa katika roho kama hiyo ya
imani, na ni kwa maamuzi hayo tu, watu wanaweza wakatatua matatizo yao binafsi na
kujishindia wenyewe milki kubwa ya utajiri wa mali na roho, hebu tusilisahau hili!
Changanua matukio
yaliyosababisha tangazo la uhuru, na ushawishike kwamba Taifa la Marekani
lilizaliwa kutokana na uamuzi
uliofanywa na kundi la kushauriana lililokuwa na watu 56. Zingatia vizuri
ukweli kwamba ilikuwa ni uamuzi wao uliohakikisha mafanikio ya jeshi la Washington kwa sababu roho ya uamuzi ule
ilikuwa ndani ya moyo wa kila mwanajeshi aliyepigana pamoja naye na kuwa kama
nguvu ya kiroho isiyotambua kitu kinachoitwa kushindwa.
Zingatia pia(kwa faida
binafsi kubwa) kwamba nguvu iliyoipa Marekani Uhuru wake ni nguvu ileile ambayo
ni lazima itumike na kila mtu anayejitambua. Nguvu hii imetengenezwa kwa kanuni
zilizoelezwa kwenye hiki kitabu. Katika simulizi ya tangazo la Uhuru haitakuwa
vigumu kugundua angalao sita ya hizi kanuni: SHAUKU, UAMUZI, IMANI, UVUMILIVU,
KUSHAURIANA, na MPANGO MADHUBUTI.
0 Response to "UAMUZI UNAOTUMIKA KUJISHINDIA MILIKI KUBWA YA UTAJIRI WA MALI NA ROHO"
Post a Comment