16. UANGALIFU
ULIOPINDUKIA
Mtu Asiyechukua
hatari kwa ujumla huchukua chochote kile kinachosalia baada ya wengine kumaliza
kuchagua. Kuwa mwangalif kupita kiasi ni mbaya sawa tu na ilivyokuwa kutokuwa
mwangalifu vya kutosha. Vyote ni kupindukia kiasi kusikokuwa salama. Maisha
yenyewe yamejazwa kwa viasili vya bahati.
17. UCHAGUZI MBAYA WA
MSHIRIKA KATIKA BIASHARA
Hii ni moja kati ya
sababu kubwa zaidi ya kuanguka katika biashara. Katika kutafuta soko la bidhaa
zako, unapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu kuchagua mwajiri ambaye
atakuwa mtu wa kukutia moyo, na ambaye ni mwerefu na aliyefanikiwa. Tuna iga
mifano ya wale tunaoshirikiana nao zaidi kwa karibu. Chukua mfanyakazi yule
aliye na sifa zinazostahili kuigwa.
18. USHIRIKINA NA
CHUKI.
Ushirikina ni aina ya
hofu, pia ni dalili ya ujinga. Watu wanaofanikiwa ni waungwana na hawaogopi
chochote.
19. UCHAGUZI MBAYA WA
KAZI.
Hakuna mtu anayeweza
kufanikiwa katika kufuata fani asiyoipenda. Hatua muhimu zaidi katika kutafuta
soko la huduma zako ni kuchagua kazi ambazo unaweza ukajizamisha mwenyewe kwa
moyo wako wote.
20. KUTOKUELEKEZA
NGUVU ZAKO ZOTE KATIKA LENGO MOJA.
Mtu anayejaribu
kufanya kila kitu ni mara chache hufanikiwa kwenye chochote. Elekeza nguvu zako
zote katika lengo moja kuu lililokuwa
dhahiri.
21. TABIA YA
KUTOKUJALI MATUMIZI
Wafujaji wa mali
hawawezi kufanikiwa, kwa kiasi kikubwa kutokana na sabababu kwamba wanasimama
kwenye hofu ya umasikini daima. Jenga
tabia ya kuweka akiba kwa mpangilio kwa
kuweka kando asilimia fulani ya kipato chako. Fedha katika benki hukupa msingi
salama wa ujasiri wakati unafanya mapatano kwa ajili ya mauzo ya huduma zako.
Bila pesa ni lazima utachukua kile unachopewa na kufurahia kukipata.
22. KUKOSA SHAUKU
Pasipo shauku mtu
hawezi kushawishi zaidi, shauku huambukiza na mtu aliye nayo kwa kiasi kikubwa
hukaribishwa katika kundi lolote lile la watu.
23. KUKOSA UVUMILIVU
Mtu aliye na akili
iliyojifungia katika jambo lolote ni mara chache sana husonga mbele. Kutokuwa
na uvumilivu maana yake ni kwamba mtu ameacha kujifunza maarifa. Aina haribifu
zaidi za kukosa uvumilivu ni zile zinazohusiana na dini, kabila, na tofauti za
mawazo ya kisiasa.
24. ULAFI
Aina haribifu zaidi
ya ulafi inahusiana na kula, vinywaji vikali na shughuli za mapenzi. Kuendekeza
kupita kiasi katika moja ya vitu hivi ni hatari kwa mafanikio.
25. KUKOSA
USHIRIKIANO NA WENGINE
Watu wengi hupoteza
nafasi zao na fursa zao kubwa maishani kutokana na kosa hili kuliko kutokana na
sababu nyingine zote ukiziweka pamoja. Ni kosa ambalo hakuna kiongozi au
mmiliki wa biashara aliyefunzwa vyema atakayelivumilia.
26. KUMILIKI UWEZO
AMBAO MTU HAKUUPATA KUPITIA JUHUDI BINAFSI.
(Wavulana na mabinti
wa familia zenye uwezo na wengine wanaorithi pesa ambazo hawakuzifanyia kazi)
Uwezo katika mikono ya mtu ambaye hakuupata taratibu mara nyingi ni hatari kwa
mafanikio. Utajiri wa haraka ni hatari zaidi kushinda umasikini.
27. KUDANGANYA KWA
MAKUSUDI
Hakuna mbadala kwa
uaminifu. Mtu anaweza kukosa uaminifu kwa muda kwa kusukumwa na mazingira
ambayo hawezi kuyazuia pasipokuwa na madhara ya kudumu. Lakini hakuna matumaini
kwa watu wasiokuwa na uaminifu kwa makusudi. Ipo siku matendo yao yatabainika
na watalipa kwa kukosa heshima, na pengine hata kukosa uhuru.
28. UBINAFSI NA
MAJIVUNO
Tabia hizi hutumika
kama alama nyekundu inayowatahadharisha wengine kujiweka mbali. Ni hatari kwa
mafanikio.
29. KUKISIA BADALA YA
KUFIKIRI
Watu wengi hawajali
kabisa au ni wavivu kutafuta ukweli ambao watautumia kufikiria kwa usahihi.
Huamua kutenda kwa kutegemea maoni yaliyotokana na kubashiri au maamuzi ya
ghafla.
30. UKOSEFU WA MTAJI
Hii ni sababu kubwa
ya kuanguka miongoni mwa wale wanaoanza biashara kwa mara ya kwanza bila ya
kuwa na mtaji wa ziada wa kutosha kukabiliana na athari za makosa yao na
kuwawezesha kuendelea mbele mpaka wamejijengea
jina.
31. Chini yah ii, taja sababu yeyote ya
kuanguka ambayo umewahi kukumbana nayo ambayo haijawekwa kwenye orodha
iliyotajwa hivi punde.
Katika hizi sababu 30
za kuanguka, kunapatikana maelezo ya janga la maisha ambalo linaendana na
karibu kila mtu anayejaribu na kufeli. Itakuwa jambo la maana ikiwa
utamshawishi mtu mwingine anayekufahamu vizuri kuipitia orodha hii na wewe, na
kusaidia kukutathmini kwa kutumia sababu 30 za kuanguka. Laweza kuwa ni jambo
lenye faida zaidi kuliko kama utajaribu hili ukiwa mwenyewe. Watu wengi
hawawezi kujiona wenyewe kama wengine wanavyowaona. Unaweza kuwa miongoni mwa
wale wasioweza.
Usemi wa wahenga ni,
“Jifahamu mwenyewe kwanza” Ikiwa
unatafuta soko la bidhaa kwa mafanikio, ni lazima uzifahamu bidhaa hizo. Hali
ni hivyo hivyo ilivyo katika kutafuta soko la huduma. Unapaswa kufahamu
madhaifu yako yote kusudi uweze aidha kuyarekebisha au kuyaondoa kabisa .
Unapaswa kujua nguvu zako kusudi uweze kuzitumia wakati unapouza huduma zako.
Unaweza kujitambua mwenyewe tu kupiti tathmini sahihi.
Ujinga unaoambatana
na ubinafsi ulionyeshwa na kijana mdogo aliyeomba kazi kwa meneja wa kampuni inyofahamika vizuri. Alionyesha
muonekano mzuri sana mpaka meneja akamuuliza ni mshahara kiasi gani aliokuwa
akitegemea kupata. Alijibu kwamba hakua na kiwango maalumu akilini(kukosa lengo
lililokuwa wazi) Kisha meneja alisema, “tutakulipa kile unachostahili baada ya
kukujaribu kwa wiki moja” “Sitakubali” kijana alijibu “Kwasababu napata kiasi zaidi ya hicho kule
nilikoajiriwa sasa”
Kabla hata hujaanza maelewano
kwa ajili ya marekebisho ya mshahara wako katika nafasi yako uliyonayo sasa, au
kutafuta ajira mahali pengine, hakikisha thamani yako ni kubwa kushinda kile unachokipata
sasa.
Kutaka pesa ni kitu kimoja
– kila mtu hutaka zaidi – lakini ni kitu kingine tofauti kabisa kuwa na thamani
zaidi. Thamani yako inabainishwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wako wa kutoa huduma
zenye manufaa au uwezo wako wa kuwashawishi wengine kutoa huduma kama hizo.
Ndugu msomaji wa
tafsiri hii ya think & grow rich, tunaomba radhi kwani sehemu hii ya 4 ya sura
ya 7 ilikuwa iwekwe siku ya Jumatatu, ratiba yetu ya kuweka tafsiri kila Jumatatu
na Alhamisi sasa tumeanza kuiheshimu na ikiwezekana tutaongeza tena siku moja iwe
mara 3 kwa juma kutokana na maombi ya wasomaji wengi waliotaka kusoma sura zote
za kitabu kwa lugha ya Kiswahili, Usikose siku ya Alhamisi sehemu ya 5 ya sura hii.
Watu bado wanajiandikisha katika lile kundi la Whatsapp la
semina za michanganuo ya miradi bunifu kwa mwaka wote wa 2018, nafasi zimebaki
chache wahi, ni kwa ada ya sh elfu 10. tu unapewa na kitabu cha michanganuo
free, pamoja na kupata access ya kuingia blogu maalumu ya semina bila gharama zozote za ziada. Whatsapp: 0765553030
0 Response to "UTAJIRI WA HARAKA NI HATARI KUSHINDA UMASIKINI (SABABU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA)"
Post a Comment