BAADA YA KUFANYA UTAFITI, SASA NAANZA KUANDIKA MPANGO WANGU WA BIASHARA YA KUKU WA MAYAI YA KIENYEJI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BAADA YA KUFANYA UTAFITI, SASA NAANZA KUANDIKA MPANGO WANGU WA BIASHARA YA KUKU WA MAYAI YA KIENYEJI.

Kuandika mchanganuo wa kuku wa kienyeji wa mayai
Katika semina yetu juzi kwenye Whatsapp sambamba na Blog ya masomo na Email tulianza kuchambua utafiti wa biashara ya kuku wa kienyeji wa mayai, jana tulikuwa na somo jingine kuhusiana na mzunguko wa fedha katika biashara(SOKO, UZALISHAJI NA UENDESHAJI KIPI MUHIMU ZAIDI YA VINGINE), na leo hii tutarejea tena katika mchanganuo wetu ule wa kuku wa kienyeji wa mayai tukianza sasa kuandika rasmi baada ya kufanya ule utafiti.

Hamna formula uanze wapi au na kipengele gani, chochote kile unaweza ukaanza ilimradi tu ujue baada ya kumaliza kila kitu sasa unapanga vipengele au sura zako kulingana na mtiririko wa sura unavyotakiwa katika mpango rasmi wa biashara, hivyo ndivyo ilivyo popote pale duniani watu wanapoandika michanganuo ya biashara.

Kwa mfano mimi katika mchanganuo wangu huu leo nitaanza na kipengele cha BIASHAR/KAMPUNI, nitaelezea kila kitu nilivyochanganua mpaka nakamilisha sura hiyo, kwanini kuna vitu niliviacha na kwanini vingine niliviweka?. Mpango wa biashara pia vipengele vyake vinahusiana kwa hiyo nitaeleza kwa mfano kwanini katika maelezo hayo ya kampuni au biashara inashangaza kukuta namba zinahusika wakati maswala ya mahesabu pale siyo mahali pake yalitakiwa yawe katika kipengele au sura inayohusu FEDHA.

Nakukaribisha sana katika semina hizi za mwaka huu, kama nilivyotangulia kusema huko nyuma semina hizi sasa ni kila siku hata ikiwa wewe ni mvivu kiasi gani bado tunakupa fursa ya kuzisoma katika blogu yetu ya private ya michanganuo hivyo usije ukasingizia whatsap huna muda wa kushiriki kila siku au ukipenda pia tuambie masomo tukuwekee kwenye email yako huko yatakaa hata ukitaka mjukuu wako aje ayasome.

Ada ni sh. Elfu 10 tu! na unapewa ofa nyingi kikiwemo, kitabu cha michanganuo ya biashara cha Kiswahili na cha kiingereza free of charge, Templates mbalimbali za michanganuo ya biashara, Michanganuo kamili mbalimbali unayoweza kusoma kama mifano, masomo mbalimbali yaliyokwishapita semina za nyuma, pamoja na fursa ya kushiriki semina nyingine zote zijazo, unakuwa mwanachama wetu wa kudumu kwa gharama hiyo hiyo ya sh. Elfu 10 tu.

Lipia leo kupitia namba zetu za simu, 0712202244  au  0765553030, jina litokee Peter Augustino Tarimo. WHATSAP tunapatikana pia kwa namba, 0765553030


Kwa vitabu mbalimbali vya biashara na ujasiriamali tembelea; SMART BOOKSTANZANIA

0 Response to "BAADA YA KUFANYA UTAFITI, SASA NAANZA KUANDIKA MPANGO WANGU WA BIASHARA YA KUKU WA MAYAI YA KIENYEJI. "

Post a Comment